Misemo maarufu zaidi ya Yesu

Misemo maarufu zaidi ya Yesu

Mt 9:13 SUV

Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.

Screenshot_20230309-205251.jpg
 
Yohana 4:22a
Ninyi mnaabudu msichokijua.

Yohana 4:23
Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
 
Mathayo 21:43

Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu(Israel), nao watapewa taifa lingine (Tanzania)lenye kuzaa matunda yake.
Huu unabii hautakiwi kabisa,utapewa tafsiri za ajabu ajabu hapo kukwepa waarabu
 
Yohana 15:1
Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

Mathayo 26:29
Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.
Qur'an pamoja na yesu,ni gamble tu huko ufalme wa milele
 
"Mama yangu na ndugu zangu ni wale wote wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.” - Luka 8:21
 
Mathayo 7:12
Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.
 
Binafsi napenda sana "mafundisho ya Mlimani na mafundisho ya Last Supper"
Mathayo 5: 13-14 Ninyi ni chumvi ya Dunia, lakini chumvi ikiwa imeharibikiwa itatiwa Nini hata ikolee? Haifai Tena kabisa ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Nini ni nuru ya Ulimwengu, mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya Mlima. Wala watu hawawashi taa na kuweka chini ya pishi Bali juu ya kiango nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu wapate kuyaona matendo yenu mema na wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
 
Back
Top Bottom