Misemo ya watu wenye wivu ongezea yako

Misemo ya watu wenye wivu ongezea yako

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,399
Reaction score
3,666
1.Siwezi nunua gari kwa mkopo

2.Huyo bwana wake mkubwa kuliko yeye, alifuata pesa tuu

3.Iphone kitu gani, simu simu tuu bora mawasiliano

4.Siwezi kula chakula cha kwenye fridge

5.Anajifanya amesoma lakini hata haolewi

6.Siwezi endesha Vits bora nitembee kwa miguu

7.Kuolewa ni stress tuu bora nikae single

8.Microwave inaleta cancer
9.Anaendesha V8 halafu anaishi uswazi
10.Hiyo nguo anajifanya amenunua laki tatu wakati ni elfu thelathini tuu kariakoo
11.Hiyo Kazi aliipata baada ya kutembea na bosi

12.Hata kama ana degree, maisha yake sawa tuu na yetu
13.Kwani Mercedes ina miguu mitano, gari gari tuu
14.Siwezi nunua gari wakati sina nyumba

15.Anaenda gym kila siku lakini ana umbo bayaa
16.Anajifanya kuongea kizungu wakati kwao shamba tuu
17.Anaringaaa, Ataachwa tuu
18.Ana umbo zuri lakini hajui kuvaa
19.Usione amenenepa hivyo anatumia ARV
20.Hakuna jipya kwenye ndoa
ONGEZEZEA NILIYOISAHA
 
13.Kwani Mercedes ina miguu mitano, gari gari tuu
14.Siwezi nunua gari wakati sina nyumba
Mkuu hizi zimekaa kimtizamo zaidi, si suala la wivu, mathalani mtu anajipangia kuwa hata kama pesa anayo si lazima anunue Mercedes, mwingine amelenga kuwa na nyumba kwanza kabla ya gari, sidhani hapa kunaweza kuwa na element za wivu.
 
Wengine wanajidai kusema watajenga kwanza halafu kutwa kuomba lift kwa wenye magari na wakiachwa wanalalama.
 
Wengine wanajidai kusema watajenga kwanza halafu kutwa kuomba lift kwa wenye magari na wakiachwa wanalalama.
Asee, huyo atakuwa anajiriwadha kabla ya kupata pesa, hakuna mtu anapenda shida, japo enzi za arobaini na saba, tulikuwa na mjomba wetu nyamihela lakini alikuwa anakaa guest, Magari alikuwa na nayo na mapesa alikuwa nayo.
 
demu mwenyewe ana sura ya baba yake

demu gani ana matege kama banio la ugali
 
Namba 5 na 7 vimenichekesha.

Ila kwa namba 14, siwezi kununua gari wakati sijajenga-Naunga hoja.
 
Milion 900 itapendeza

Huwezi kunijibu mimi hivyo
 
Back
Top Bottom