KERO Mishahara inachelewa kwa Watumishi wa hospitali ya St. John Paul II ya Kaliua, Tabora

KERO Mishahara inachelewa kwa Watumishi wa hospitali ya St. John Paul II ya Kaliua, Tabora

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba kuwasilisha malalamiko kuhusu ucheleweshwaji wa mishahara kwa watumishi wa Hospitali ya St. John Paul II iliyopo Kaliua, Tabora.

Kuna madai kwamba watumishi wa hospitali hiyo wamekuwa wakicheleweshewa mishahara yao bila sababu za msingi na bila kupewa taarifa kuhusu sababu za kuchelewa kwa malipo hayo. Hali hii imewasababishia changamoto za kiuchumi na kuathiri ustawi wao pamoja na mazingira ya kazi.

Aidha, changamoto hizo zinaweza kuathiri utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili kwa kina ili kubaini chanzo cha tatizo na kuchukua hatua zinazofaa, kwa lengo la kuhakikisha watumishi wanapata stahiki zao kwa wakati na huduma za afya zinaendelea kutolewa kwa ufanisi.
 
Kibaya zaidi, hii inconsistency inaenda kuwaathiri zaidi wagonjwa ambao ndiyo wahanga wakuu.

Lakini hili wala hawalifikiriii kabisa.
 
Back
Top Bottom