Tetesi: Mishahara kupanda maradufu!

Tetesi: Mishahara kupanda maradufu!

Status
Not open for further replies.
Na sisi wakulima jeee
Kilimo n uti wa mgongo wa taifa
 
Pamoja na hayo, alisema Serikali inaendelea na utafiti wa tathmini ya kazi na itakapokamilika, itapanga upya mishahara na motisha kwa watumishi wote wa umma ikiwamo sekta hiyo.

SOURCE:Mtanzania
[/SIZE]

Kwahiyo zile tetesi za mishahara kupanda mwezi huu si kweli maana bado tafiti zinaendelea na uhakiki hadi mwezi......
 
Katika mawaziri wasiofaa ni huyu sababu ni muongo kupindukia na anaendelea sana siasa
 
Haaaa huo ni uongo acha kuwapa watu matumaini, acha waendelee kukipigia bajeti kile walichokizoea na vip kuhusu mishahara kutoka billion 520 hadi 570 wakati walikuwa wametoa wafanyakazi hewa.
Hizo billion 50 ni kwa ajili ya nini wakati wafanyakazi hewa zaidi ya 10,000 waliondolewa kazini, wengine walisuiwa kupandishwa madaraja ilihali waliokuwa wamepanda walirejeshwa kwenye madaraja na mishahara ya awali, na pia ajira mpya kusitishwa?
 
Hizo billion 50 ni kwa ajili ya nini wakati wafanyakazi hewa zaidi ya 10,000 waliondolewa kazini, wengine walisuiwa kupandishwa madaraja ilihali waliokuwa wamepanda walirejeshwa kwenye madaraja na mishahara ya awali, na pia ajira mpya kusitishwa?
mtu wewe unajua kuchungulia! Umeona ndani eeh? Kam hewa 17000+ hazipo kwenye payroll na mkwere alikuwa analipa 520 bln na hewa ikiwamo na bangosha ameovrexceed hiyo up to 570bln bila hewa. Ni nini kimetokea katika ukokotozi huu? Zingatieni hakuna ajira mpya wala replacement yoyote iliyofanyika. Kwa maana hiyo maelezo ya kina ni muhimu juu ya hiyo ziada ya 20bln hapo inakovujia. Vinginevyo panya watabaki kuwa panya na yabia yao ya uharibifu itabaki kuwa ileile.
 
Hilo swala bado ni nyeti ndugu zangu tumesubili had tumepoteza matumain
 
wingi wa pesa si ufumbuzi wa uchumi. hamasisha uzalishaji bidhaa vwandani, ufugaji na kilimo , dhibiti ufisadi na fedha haramu. kifupi imarisha thamani ya fedha yako ambapo sh 50 itapokelewa dukani na kupewa sabuni, au sokoni na ukapewa samaki au unga wa mahindi, hapo hata ukiweka kima cha chini sh 50,000 mfanyakazi ataishi.
 
Waache ving'ang'anizi waendelee kukamua jiwe wakitaraji kunywa maziwa !
 
Nimepewa taarifa kuwa mwezi huu hio mshahara mpya hakuna! amini nakwambieni ndugu zangu.endeleeni na mambo yenu mengine na si suala la salary mpya.
 
Hivi ikiongelewa mishahara inawataja walimu na kada ya afya tuu. Je, watumishi wengine hawafanyi kazi tena ngumu sana zinazohitaji kutumia akili kudeal na pyschosocial problems?

Je, mishahara itaongezwa kuziba mianya ya maisha tunayoikabili ili kuweza kufikia malengo ya nchi na ya mtu mmoja mmoja?
 
At least kada zingine hata kuwa kuna per diem, safari, seminars, house allowance n.k walimu Sasa ha ha ha nicheke kama mazuri
 
Hivi ikiongelewa mishahara inawataja walimu na kada ya afya tuu. Je, watumishi wengine hawafanyi kazi tena ngumu sana zinazohitaji kutumia akili kudeal na pyschosocial problems?

Je, mishahara itaongezwa kuziba mianya ya maisha tunayoikabili ili kuweza kufikia malengo ya nchi na ya mtu mmoja mmoja?
Kama mishahara itaongozwa kwa sababu hizo, Jee maisha yakiboreka kiasi kufanya mianya ya maisha kupotea mishahara ipunguzwe?????. Ninavyoelewa mishahara ni matokeo ya tija ipatikanayo kutokana ufanisi wa kazi. Jee humu kwenye mashirika yetu ambayo tunatumia saa 1 kunywa chai asubuhi, tunatumia saa 1 kusoma magazeti ya siku, tunatumia saa 1 kuzungumzia mambo ya jana[hasa siku ya jtatu], tunatumia saa 1 ku-brouse, tunatumia saa 1 kwenda lanchi. Hivi mwisho wa siku tunatarajia nini???
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom