Hivi watu ambao huwa wanavumisha haya mambo hawafahamu kuwa matumizi ya serikali ni lazima yawe yameidhinishwa na Bunge? Je, kama Bunge katika bajeti ya 2016/2017 halikuidhinisha bajeti yenye ongezeko la mishahara, fedha za kuongeza mishahara katikati ya mwaka wa fedha zinatoka wapi? Kabla ya kuandika unakuwa umejiuliza swali hili?? Na hata kama ingekuwa ni kweli, mbona ulichoweka ni karibia hicho hicho kinacholipwa kwa sasa? mabadiliko yako wapi?