Tetesi: Mishahara kupanda maradufu!

Tetesi: Mishahara kupanda maradufu!

Status
Not open for further replies.
Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Watumishi wa umma kaeni mkao wa kupokea mishahara minene. Kwa muda mrefu sasa tangu Dr Magufuri aanze kurekebisha mifumo ya utawala wa nchi, watumishi wa umma walionekana kama wametengwa sana hadi baadhi yao kupelekea kukata tamaa ya maisha. Sasa mkae mtulie…mambo yenu yameiva!


Kuna taarifa kwamba Serikali imepanga kuongeza mishahara ya umma maradufu ifikapo September baada ya kufanikiwa kuwaondoa watumishi na wanafunzi hewa na kupunguza mishahara ya baadhi ya watumishi waliokuwa wakilipwa mamilioni ya shilingi huku wengine wakilipwa mishahara uchwara, hivyo fedha zote zilizookolewa zimeelekezwa kuongeza mishahara ya watumishi wa umma ambao wamekuwa wakilalamikia udogo wa mishahara kwa muda mrefu. Aidha, taarifa zinadai kuwa watumishi wote wanaostahili kupanda vyeo/madaraja watapandishwa na kuanza kulipwa mishahara mipya mara moja.


Ifahamike kwamba wakati Dr Magufuri anaomba ridhaa ya kuongoza nchi hii aliwaahidi maslahi bora watumishi wa umma, hivyo ahadi yake ndio inaanza kutekelezwa sasa. Kumbe lilikuwa ni suala la wakati tu. Sasa civil service imeanza kupata mwanga uliokuwa umekosekana kwa muda mrefu na kupelekea watumishi wa umma kuvunjika mioyo ya kuwatumikia wananchi. Hongerza sana Dr Magufuri kwa kuwajali watumishi wa umma.
hakuna kitu kama hicho,sijui umetoa wapi
 
Kwa bajeti ipi iliyopitishwa na bunge, itakuwa ni kuingilia muhimili mungine wa dola
Hivi kila kitu kipitishwe na bunge... Mbona huulize kwanini bunge wasiingile hilo tatizo la wafanya kazi hewa, au wakati Raisi anaingilia suala la wafanyakazi hewa mbona hamku sema hilo suala halikujadiliwa bado bungeni na anaingilia muhimili wa dola?
Tukae kwanza tuangalie kama hili suala litakua la kwali,
 
niliwahi kupita sehemu nikamkuta kichaa kalala na ilivyoekekea alikuwa kwenye usingizi mzito,hata hivyo cha ajabu alikuwa anatabasamu Mara kwa Mara.Hii ikanikumbusha kuwa wote huota njozi/ndoto.
 
Kwa bajeti ipi iliyopitishwa na bunge, itakuwa ni kuingilia muhimili mungine wa dola
Kwani wabunge ndio hutupangia mshahara? Kwa taarifa yako serikali ndiyo hupanga mishahara na bajeti yote ya serikali. Bunge kazi yake ni kuidhinisha tu na likikataa kuidhinisha raisi huvunja bunge na uchaguzi mkuu mpya kufanyika ndani ya miezi 6.

Hivyo bunge litaidhinisha baadaye huku mishahara ilishapanda kuanzia siku ya tarehe 1 Septemba, siku ambayo wengine watakuwa barabarani wakichapwa virungu vya washawasha! Siasa mchezo mtamu na mchungu at the same time if you know how to play it.
 
Kwani wabunge ndio hutupangia mshahara? Kwa taarifa yako serikali ndiyo hupanga mishahara na bajeti yote ya serikali. Bunge kazi yake ni kuidhinisha tu na likikataa kuidhinisha raisi huvunja bunge na uchaguzi mkuu mpya kufanyika ndani ya miezi 6.

Hivyo bunge litaidhinisha baadaye huku mishahara ilishapanda kuanzia siku ya tarehe 1 Septemba, siku ambayo wengine watakuwa barabarani wakichapwa virungu vya washawasha! Siasa mchezo mtamu na mchungu at the same time if you know how to play it.
Usitegemee mtumishi wa umma kuandamana siku hiyo.
Hayupo na hatapatikana
 
Kindly let me confirm your thread is true I think all of us we will praise Dr Magufuli. kutokusafiri nakukaa ikulu muda mrefu ni siri ya hayo uio andika
Kama ni kweli ni jambo jema. Lakini Septemba Mosi kwa maana Mshahara utatoka mwishoni mwa Sept au Mwanzoni mwa Oktoba, maana wa mwez wa nane watumishi walishapokea na ulibaki kama ulivyo.
 
Hadi nione pesa ikiwa kwenye akaunti, vinginevyo Porojo tu. Pia niitoe niihesabu ndio niamini
 
Mkuu tpaul hiyo hela yenyewe ya kuongeza mishahara mara mbili itatoka wapi? Ni jambo zuri kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wa umma hata mara tatu, lakini Serikali hii haina pesa na mapato ya Serikali yanaanguka kwa kasi ya kutisha labda wakaombe mkopo mwingine wa trilioni kadhaa Exim Bank ya kule China ili waweze kufanya hivyo.
 
Mhh sasa mbna kutakua na mbanano wa matukio mengi sana hio tarehe moja
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom