Mzee Kikowapi
Member
- Sep 21, 2024
- 97
- 245
Moderators naomba msifuze au kuunganisha huu uzi.
Naamini JF ni Platform kubwa na hata Rais wa nchi na viongozi wengine wanapitia humu.
Naanza kwa kudeclare interest binafsi ni Mtumishi wa umma na mshahara ni haki yangu kama ninavyotimiza wajibu wangu. Nyie matajiri na mabilionea wa JF msiohitaji mshahara uacheni huu uzi na endeleeni na nyuzi zenu nyingine.
Kwa kawaida kuanzia tarehe 23 hadi 25 serikali hulipa mishahara watumishi wake. Kwa mwezi huu wa Novemba 2024, Serikali imelipa mishahara siku ya Ijumaa kwa watumishi wake na kwa wale wastaafu wanaopokea fedha zao.
Cha kusikizisha kuna baadhi ya watumishi wa umma nikiwepo mimi Binafsi sijapokea mshahara wangu. Sijajua changamoto ni nini. Watumishi wengi toka kada mbalimbali katika sekta ya umma kuanzia kwenye taasisi za umma, Mamlaka na bodi mbalimbali za serikali hadi kwenye Mamlaka za serikali za mitaa na mahospitalini hawajapokea mishahara hadi sasa na hakuna tamko wala maelekezo yanayoonesha shida nini. Pia hata baadhi ya wastaafu nao hawajapokea stahiki zao za kila mwezi.
Tafadhali tunaitaka serikali itoe tamko katika hilo kwani kama tulivyotimiza wajibu wetu kwa mwezi mzima, tunatakiwa tulipwe haki zetu.
Nawasilisha.