DOKEZO Mishahara kwa watumishi wa Umma Novemba 2024: Kwanini Serikali haikulipa mishahara kwa baadhi ya watumishi hadi leo?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mzee Kikowapi

Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
97
Reaction score
245
Moderators naomba msifuze au kuunganisha huu uzi.

Naamini JF ni Platform kubwa na hata Rais wa nchi na viongozi wengine wanapitia humu.

Naanza kwa kudeclare interest binafsi ni Mtumishi wa umma na mshahara ni haki yangu kama ninavyotimiza wajibu wangu. Nyie matajiri na mabilionea wa JF msiohitaji mshahara uacheni huu uzi na endeleeni na nyuzi zenu nyingine.

Kwa kawaida kuanzia tarehe 23 hadi 25 serikali hulipa mishahara watumishi wake. Kwa mwezi huu wa Novemba 2024, Serikali imelipa mishahara siku ya Ijumaa kwa watumishi wake na kwa wale wastaafu wanaopokea fedha zao.

Cha kusikizisha kuna baadhi ya watumishi wa umma nikiwepo mimi Binafsi sijapokea mshahara wangu. Sijajua changamoto ni nini. Watumishi wengi toka kada mbalimbali katika sekta ya umma kuanzia kwenye taasisi za umma, Mamlaka na bodi mbalimbali za serikali hadi kwenye Mamlaka za serikali za mitaa na mahospitalini hawajapokea mishahara hadi sasa na hakuna tamko wala maelekezo yanayoonesha shida nini. Pia hata baadhi ya wastaafu nao hawajapokea stahiki zao za kila mwezi.

Tafadhali tunaitaka serikali itoe tamko katika hilo kwani kama tulivyotimiza wajibu wetu kwa mwezi mzima, tunatakiwa tulipwe haki zetu.

Nawasilisha.
 
Yes ,watu wengi hawajapata mshahara . Tunasubiri taarifa rasmi Kuna tatizo Gani?
 
Kuweni na Subra..! Leo ni tarehe 25, mwezi bado haujaisha.

Kama mmebanwa sana kwenye familia fanyeni maarifa, ..Waoneni kina Mangi,mbona akina Mangi wenye maduka huwa wanasaidia sana mtaani.

Kopa kwa Mangi,Huwa wanaokoa jahazi hasa iwapo shida inahusu kibaba cha unga au maharage. Usiende kukopa school fees.

Au nyinyi hamuishi vizuri na Majirani.!
 
Wengi tu bado hawajapata salary, halafu wamekaa kimya tu
 
Moderators naomba msifuze au kuunganisha huu uzi.

Naamini JF ni Platform kubwa na hata Rais wa nchi na viongozi wengine wanapitia humu.

Naanza kwa kudeclare interest binafsi ni Mtumishi wa umma na mshahara ni haki yangu kama ninavyotimiza wajibu wangu. Nyie matajiri na mabilionea wa JF msiohitaji mshahara uacheni huu uzi na endeleeni na nyuzi zenu nyingine.

Kwa kawaida kuanzia tarehe 23 hadi 25 serikali hulipa mishahara watumishi wake. Kwa mwezi huu wa Novemba 2024, Serikali imelipa mishahara siku ya Ijumaa kwa watumishi wake na kwa wale wastaafu wanaopokea fedha zao.

Cha kusikizisha kuna baadhi ya watumishi wa umma nikiwepo mimi Binafsi sijapokea mshahara wangu. Sijajua changamoto ni nini. Watumishi wengi toka kada mbalimbali katika sekta ya umma kuanzia kwenye taasisi za umma, Mamlaka na bodi mbalimbali za serikali hadi kwenye Mamlaka za serikali za mitaa na mahospitalini hawajapokea mishahara hadi sasa na hakuna tamko wala maelekezo yanayoonesha shida nini. Pia hata baadhi ya wastaafu nao hawajapokea stahiki zao za kila mwezi.

Tafadhali tunaitaka serikali itoe tamko katika hilo kwani kama tulivyotimiza wajibu wetu kwa mwezi mzima, tunatakiwa tulipwe haki zetu.

Nawasilisha.
Nadhani hazina imeelemewa na mzigo wa uchaguzi was serikali za mitaa,kampeni kabla ya wakati ya mgombea wa CCM anaegawa pesa kila uchwao, ndio maana hata pesa za elimu bure zimeanza kutoka Kwa to mafungu!!!

Kifupi nanusa hali mbaya !!
 
Kama hujapata mshahara hadi sasa kunywa maji mengi kaa kwa kutulia mshahara utapata tu
 
Nadhani mleta mada umekurupuka labda ni kwa shida.
Leo ndio tarehe 25 na pengine Kuna tatizo au hakuna tatizo ungesubiri siku kadhaa upate uhakika kabla ya kulalamika
 
Moderators naomba msifuze au kuunganisha huu uzi.

Naamini JF ni Platform kubwa na hata Rais wa nchi na viongozi wengine wanapitia humu.

Naanza kwa kudeclare interest binafsi ni Mtumishi wa umma na mshahara ni haki yangu kama ninavyotimiza wajibu wangu. Nyie matajiri na mabilionea wa JF msiohitaji mshahara uacheni huu uzi na endeleeni na nyuzi zenu nyingine.

Kwa kawaida kuanzia tarehe 23 hadi 25 serikali hulipa mishahara watumishi wake. Kwa mwezi huu wa Novemba 2024, Serikali imelipa mishahara siku ya Ijumaa kwa watumishi wake na kwa wale wastaafu wanaopokea fedha zao.

Cha kusikizisha kuna baadhi ya watumishi wa umma nikiwepo mimi Binafsi sijapokea mshahara wangu. Sijajua changamoto ni nini. Watumishi wengi toka kada mbalimbali katika sekta ya umma kuanzia kwenye taasisi za umma, Mamlaka na bodi mbalimbali za serikali hadi kwenye Mamlaka za serikali za mitaa na mahospitalini hawajapokea mishahara hadi sasa na hakuna tamko wala maelekezo yanayoonesha shida nini. Pia hata baadhi ya wastaafu nao hawajapokea stahiki zao za kila mwezi.

Tafadhali tunaitaka serikali itoe tamko katika hilo kwani kama tulivyotimiza wajibu wetu kwa mwezi mzima, tunatakiwa tulipwe haki zetu.

Nawasilisha.
Waliokosa ni ajira mpya au hata watumishi wa muda mrefu?
 
Back
Top Bottom