Lord OSAGYEFO
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 3,079
- 4,893
Tanzania ni moja ya nchi masikini zilizojaliwa kuwa na utitiri wa viongozi kuanzia Wilaya mpaka Taifa viongozi hao waliligharimu taifa fedha nyingi sana kuliko hata za watumishi wote wa serikali tuna wakuu wa wilaya 140, Wakurugenzi 200 wakuu wa mikoa 26 makatibu tawala wa wilaya 140 makatibu tawala wa mikoa 26 wabunge 400 mshahara wa chini ni tsh. Milioni 3 na mshahara wa juu ni tsh. Mil.11 bado magari ya gharama n.K. Fedha zote hizi ni kodi za masikini wananchi.
Kutokana na hali hiyo wananchi wanakata tamaa ya kulipa kodi kwani kodi zao zinatumika na viongozi kujilipa mishahara mikubwa na magari ya gharama .Juzi kuna mbunge kasimama anadai wabunge waongozewe mishahara anasahau kuwa watumishi wa umma huu ni mwaka wa 6 hawajaongezewa mishahara hata sh.10,000/=.
Tunashauri utitiri wa viongozi upunguze na mishahara yao hasa ya wabunge nayo ipunguzwe ili wananchi wahamasike kulipa kodi kwa hiari.