Tetesi: Mishahara mipya kwa watumishi wa umma imetoka?

Tetesi: Mishahara mipya kwa watumishi wa umma imetoka?

Hiyo ndo mishahara inayolipwa kwa sasa' ilianza kulipwa July 2015, hiyo unayoiona hapo n ya ngazi ya shahada(degree)-basic salary.Cha kusikitisha ilitakiwa ipande kuanzia July 2016 lakin mwenye nchi kaamua kukiuka mikataba ya watumishi wake.
 
Mbona sjaona ya ma engineer hapo ina mana hawana umuhimu kwenye serikali ?

Aliekuambia mainjinia tunakaa kusubiri TGS ni nani mkuu? Wengi tumejiajiri na hata wale walioajiriwa mishahara yao ni Siri Kwani ni mikubwa kiasi kwamba ikiandikwa humu walimu na madaktari watakata tamaa
 
Hiyo mishahara ni zile zilipendwa hamna mishahara mipya hapo
 
wandugu hili gazeti lina onesha tetesi kuhusu mishahara mipya ya watumishi na lina dai kua kuna waziri alilizungumzia jana bungeni mlo kua karibu na tv je kuna ukweli wowote ktk hili je range hiyo ya mishahara ina weza kua kweli au ni ndoto za mchana?

naambatanisha pichaView attachment 399871

NITAITISHA MAANDAMAO KAMA SISI SERIKALI KUU TUTAENDELEA KULIPWA KIDOGO HIVI KULIKO MANESI NA WALIMU..YAANI WALIMU WANAKULA UPEPO HIVI WAKATI ASILIMIA 50% YAO HAWAFANYI KAZI.HAWA NDO WNASABABISHA MH RAIS ASITE KUTUAJILIA WATU WA NYONGEZA
 
Kweli walimu ni wito yaani kufika tarakimu 7 uwe na umri wa 55+ sasa hapo si kuelekea kustaafu.
Nawapenda sana walimu wangu mlionifundisha pigeni Mungu atawalipa tu...
Nijuavyo mimi sio miaka 55 kama ulivyonaliri kwa mtoa comment hoja ya msingi ni kupanda madaraja kwa wakati mfano Mwl akitoka Daraja D yenye 716000 kwenda E kitu kama 940000 (sina uhakika) kila baada ya 3yrs, sasa Mwl huyu assume alianza kazi na miaka 25-26(ndio umri wa walimu wengi toka vyuo vikuu) kabla hata hajafikisha miaka 35 atakua amefikia Dara F na atalipwa kwa viwango vya Daraja F kikubwa ni kupanda kwa madaraja kwa wakati ndiko kunakowaumiza walimu au kuwafurahisha
 
Diploma inapoizidi degree ndio shida

hapo mi ndipo napoonaga kuwa hakuna fair,yaani mwenye degree ya aina nyingine isiyo ya afya alipwe chini ya diploma ya afya,noma sana aisee,morali kazini itapandaje kwa mfano
 
Kusema Kiswahili sahihi sio kigezo cha kumwajiri mtu ni makosa sana. Kama mtu hawezi kuandika vema Kiswahili ambacho ni lugha aliyokua nayo na anaitumia kila siku ataweza vipi kufanya jambo lolote lingine (ikiwa ni pamoja na ajira yake) vema?
 
NITAITISHA MAANDAMAO KAMA SISI SERIKALI KUU TUTAENDELEA KULIPWA KIDOGO HIVI KULIKO MANESI NA WALIMU..YAANI WALIMU WANAKULA UPEPO HIVI WAKATI ASILIMIA 50% YAO HAWAFANYI KAZI.HAWA NDO WNASABABISHA MH RAIS ASITE KUTUAJILIA WATU WA NYONGEZA
Wataje walimu wasiofanya kazi acha kulopoka lopoka Vila vielelezo Taja tuwajue Otherwise mshukuru Mwl wako kwan ni jitihada zake ndio zimewezesha mimi na wewe kukaa hapa kuwa kashifu if kwa taaluma ya uandishi waliyotuzawadia
 
wandugu hili gazeti lina onesha tetesi kuhusu mishahara mipya ya watumishi na lina dai kua kuna waziri alilizungumzia jana bungeni mlo kua karibu na tv je kuna ukweli wowote ktk hili je range hiyo ya mishahara ina weza kua kweli au ni ndoto za mchana?

naambatanisha pichaView attachment 399871
Huu ni ubakaji wa habari.hakuna kitu kama hicho.Kubwa zaidi alilozungumza waziri ni kuwa serikali inafanya UTAFITI WA TATHIMINI YA KAZI ili iweze kuwapanga watumishi na kuwapa mishahara wanayostahili.na katika hili hajasema kama tathimini imeshafanyika au la, na kama tathimini imefanyika hakusema kama utafiti WA hiyo tathimini umeshaanza au kama umeanza utaisha lini !!!!
 
Back
Top Bottom