Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Wana JF nadhani wakati wa kipindi cha Mkapa cha mwanzo ilisemwa pahali kwamba mawaziri wakati ule walikuwa wanapata Laki Tatu na Rais laki 9 hivi. Kwa mawazo yangu ingekuwa mandatory walipa kodi jujue mishahara hiyo na marupurup/posha za kila waziri na rais. Ila hilo kwa sasa sidhani hadi katiba mpya ambayo huko 2030.

Nasikia watu wengine wanasema mshara wa rais ni "mdogo" ila tutambue kwamba yeye na familia yake wanagharimiwa kila kitu hata baada ya kuacha urais.
 

Ahsante Nsiande that is fact,delivery yako isipokidhi no renewal unakwenda zako,malipo yanatokana na uwezo wa tasisi yenyewe,hao waliotajwa mbona mishahara yao ni midogo,pia kuna ma CEO wanapata kidogo sana below 3.0m,so don't question about salaries.
 
Mimi nashindwa kuelewa tunakwenda wapi na hali ya watanzania itakapofika mwisho itakuaje kwani mpaka sasa walimu mbali na kuwa na mishahala midogo bado mikopo inabaniwabaniwa mfano kuna uhalali gani wa mwalimu kukaa miaka 3 ndio akopeshwe wakati probation period yake ni mwaka mmoja na viongozi wa juu wanalimbikiziwa mishahara na posho kubwakubwa
 
Kama itasaidia wanaJF kulinganisha, mshahara wangu nilipoteuliwa Gavana wa BoT Januari 1966 ulikuwa Shs 60,000 kwa mwaka: yaani Shs 5000 per month

Rais Mwalimu Nyerere alikuwa analipwa mshahara huo huo.

Lakini ikumbukwe kwamba wakati huo Dola moja ya Merikani ilikuwa sawa na Shs 7.00. Kwa hiyo mshahara wa Gavana ulikuwa US Dollars 712 per month ambao kwa kiwango cha sasa ungekuwa takriban Shs 1.1 milioni.

Rais Nyerere mnamo 1968 aliamua kupunguza mishahara ya viongozi Tanzania, na akapunguza mshahara wake kwa asilimia 10, kufikia Shs 54,000 kwa mwaka. Licha ya kwamba mkataba wangu wa Ugavana ulikuwa unatamka kwamba mshahara wangu hautapunguzwa, nilijitolea nikapunguzwa mshahara ili usizidi wa Mheshimiwa Rais. Kwa hiyo Mshahara wa Gavana kwa mwezi ulikuwa Shs 4'500.

Marupurupu mengine yalijazia mishahara hii, kama vile free housing, watumishi wawili nyumbani, gari pamoja na petroli na dereva.

Ingawa sikumbuki mishahara ya mawaziri wakati huo, ilikuwa chini ya ule wa Rais. Hata nilipoteuliwa Waziri wa Fedha 1977 mishahara ilikuwa midogo na tuliendelea hivyo hivyo hadi Mwalimu alipostaafu; ndipo milipuko hii inayatajwa na wachangiaji wa thread hii ilipoanza.
 

Asante sana kwa taarifa.

Ila kwenye red...> JK ajilipe chini ya 2M kwa mwezi.. 😛ray:
 
Kuna sheria iliyotungwa katika enzi za ukweli na uwazi inayokataza kuzungumzia mshahara wa rais, hivyo chukua tahadhari vinginevyo unaweza kupambana na mkono wa sheria.

Mkono wa sheria hauwezi kushindana na nguvu ya umma.Kwa kuwa sisi ndio waajiri tuna haki ya kujua mishahara yao na kuweka ukomo na sio kujiongezea kila wanapojisikia.
 
Kusema ukweli jambo muhimu sana hapa ni kuangalia manufaa ya taifa letu. Ni wazi kama wangefanya kazi iliyo safi, wasijihusishe kwa namna yoyote na ufisadi, wakahakikisha kila anayejihusisha anaondolewa mara moja, na wafanyakazi wengine wote wanapata haki zao.

Waalimu wakalipwa mishahara yao kwa wakati na posho zao. Madai yenye kutia kichefuchefu kama ya wazee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupata mafao yao haraka nk. Yaani kwa maana ya kusimamia haki na kutotumia hongo kurudi au kuingia madarakani, wananchi tusingeweza kuwalaumu sana.

Lakini pamoja na mishahara, marupurupu makubwa, magari ya gharama kubwa na safari nyingi za nje nk. bado watu hao hao wanashindwa kusimamia haki hata kushindwa kututajia ni nani amehusika na EPA, Deep Green, Kagoda, Dowans na mikataba lukuki feki kama ya rada, ndege ya raisi nk. Imegeuka kuwa laana ya taifa letu.

Wakiulizwa wanasema mtavuruga amani, nchi yetu ni ya amani. Wakiulizwa zaidi wanakimbilia tawi jingine-- mnaleta udini! Kweli tutafika?
 
nadhan kuna jambo limejificha, suala ni marupurupu nje ya mshahara ndio yanaleta shida kwani salarly nadhan ziko kweney range nzuri tu!
 
Nimeona breakdown ya miaka ya nyuma maana anasema mbunge anakopeshwa 40,000,000 ya gari lakini Godbless Lema alituambia wameandikiwa 90,000,000 ya gari

Mishahara ni mikubwa sana lakini mbaya zaidi viongozi wetu badala ya kutosheka ndiyo kwanza wanaingia ufisadi; hawa letu moja ni kuwakataa tu wasifike 2015 watatuumiza zaidi.
 
serikali ina siri kali, never expect them to mention their salaries, only yours 'll b heard, not theirs. Leave it and work on ur biznez.

serikali ina siri kali kwa sababu neno lenyewe "serikali" linatokana na neno "sirikali" hivyo ni lazima kuwe na siri kwenye serikali.
 
serikali ina siri kali, never expect them to mention their salaries, only yours 'll b heard, not theirs. Leave it and work on ur biznez.

serikali ina siri kali kwa sababu neno lenyewe "serikali" linatokana na neno "sirikali" hivyo ni lazima kuwe na siri kwenye serikali.
 
Nina uhakika wameacha kuzila mkuu wangu.
 
Ni 2011 na bado hakuna anayejua kwa uhakika mkuu wetu wa nchi analipwa mshahara kiasi gani! Hii ni aibu kubwa sana hususan ukizingatia kuwa walipa kodi hela zao ndiyo zinatumika.

Shameful!
 

kazi bado tunayo sana mbeleni, duh!
 
Nadhani hana fixed amount. Anajichotea tu, si shamba la bibi hili?
 
Ni 2011 na bado hakuna anayejua kwa uhakika mkuu wetu wa nchi analipwa mshahara kiasi gani! Hii ni aibu kubwa sana hususan ukizingatia kuwa walipa kodi hela zao ndiyo zinatumika.

Shameful!
Hata mimi nilishangazwa. Wenzetu hadi kodi wanazokatwa kwenye hiyo mishahara wanatangaza. Ukitaka kujuwa huu ni ummafia wenyewe.

Wanaiga mengine na mengine ya msingi wanaacha,wameingia madarakani kufanya uharamia na ufedhuli tu. Watalipa tu hawa.
 
kwahiyo hakuna mwenye data kamili za mshahara wa mkulu wetu waungwana? kwanini iwe siri kwa tanzania tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…