Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Kati ya Mishahara inayotia hasira na kufany anione hii nchi sio masikini ni ya CEO wa PPRA na PSPF. CEO wa PPRA Dr. Mlinga analipwa 7 Million, wakati mama Mmanga wa PSPF analipwa 6.7 Milion...!

Jamani hii inatisha...! Bado hawa watu wanamarupurupu ya kutisha, Gari, nyumba traveling allowance etc...! Leo hii tunaambiwa nchi ni masikini...!
inakupa hasira gani mishahara hiyo ?, most of these CEO's have perfomance based contracts and they negotiate their salaries, this is bcoz of the complexity of the job, magnitude and decision making @ that level,being contract based and renewed on perfomance, remuneration is commisurate(sp) to the risks taken to leave a healthy permanent job
 
Kati ya Mishahara inayotia hasira na kufany anione hii nchi sio masikini ni ya CEO wa PPRA na PSPF. CEO wa PPRA Dr. Mlinga analipwa 7 Million, wakati mama Mmanga wa PSPF analipwa 6.7 Milion...!

Jamani hii inatisha...! Bado hawa watu wanamarupurupu ya kutisha, Gari, nyumba traveling allowance etc...! Leo hii tunaambiwa nchi ni masikini...!

Kama kweli ni hiyo, basi wanalipwa kidogo sana ukilinganisha na majukumu waliyopewa. Siku ya kuacha kazi anapofanyiwa hesabu wanaangalia basic salary peke yake
 
Tangaza wako kwanza. Mshahara ni siri ya mwajiriwa na mwajiri.
 
QUOTE=terabojo;1308004]Wana JF leo napenda kuwakilisha hoja ya kutaka serikali na mashirika ya umma au yale ambamo serikali ina hisa nyingi itangaze/watangazie walipa kodi wa nchi hii mishahara na marupu rupu wanayowalipa hao mawaziri; makatibu wa Kuu na CEO's wa mashirika ya umma ili sis walala hoi tujue kwani ndo tunakamuliwa.

Je wewe uko tayari kutoa siri yako na mke wako ya ndani?:embarrassed:[/QUOTE]

Sina uhakika kama unamaanisha ulichoandika .... maana maneno haya yanadhihirisha uelewa wako kuwa jinsi ya kulinganisha mambo ulivyo kama Makamba
 
Utaambiwa mshahara ni siri ya mhusika.
Mishahara ya mawaziri na makatibu wakuu ni "siri ya mhusika", lakini ile ya walalahoi siyo siri. Siku wakiongeza senti moja huutangazia ulimwengu kuwa "tumeongeza mshahara wa kima cha chini kutoka 60,000 hadi 60,000.01. AIBU KWA MAANA YA KUWA SERIKALI HAIONI AIBU. Endeleeni kucheza na ustahamilivu wetu.
 
Serikali ina siri kali, never expect them to mention their salaries, only yours 'll b heard, not theirs. Leave it and work on ur biznez.
 
wansema kuwa ukichuku viongozi wote wa mashirika ya umma , mawaziri na wabunge(na wote unaowajua)...malipo yao hayana athari kiuchumi kwan hata elfu moja hawafiki.....
hebu lipa walimu na wauguzi milioni moja tu kila mwenzi usikia khabari yake...
 
mbona nchi za watu kila kitu kipo wazi............?....sisi tunaficha nini?

Kumbuka hizo ni nchi za "Watu", na sisi si kama wao. Zingewekwa hapa data za ma-CEOs wa bongo haki ya nani unaweza kuacha kazi na kuwa jambazi
 
But hakuna mtu aliyefuatiliwa swali ni mishahara ya mawaziri bila kumtaja mtu mbona mishahara ya walimu na idara zingine inajulikana?tunataka kujua coz ni kodi zetu
 
Mimi nahisi africa ni tabu kutatua tatizo la umaskini ikiwa viongozi wenyewe hawajuwi umaskini ni nini kutokana na kuto kukinai? viongozi wetu wa Tanzania ukiangalia walivyojikumbizia mali na kujenga makasiri kila kona hii inawafanya wasahau shida za watu wa Gongolamboto.

Viongozi wa Ulaya wengi wao huishi ktk nyumba za kawaida tu nitabu kujuwa hii ni nyumba ya Rais au waziri, na huingia madarakani wengine wakiwa vijana na wazuri warembo,lakini kipindi kifupi tu hukongoka na kuzeka haraka mno.

Na hutoka ktk madaraka haliyakuwa hawana chochote ispokuwa sifa za uchapaji kazi lakini sio kujilimbikizia mamali, muza dungule Ulaya anaweza kuwa tajiri kuliko waziri.

Lakini Tanzania sio hivyo uongozi ni uchumi wa kujitajirisha mara moja na kusahau waliokushagua na kila ukiwa fisadi mwizi ndio ilani ya chama inakulinda kwa vile washawi ni wengi na ilani ni moja. Mungu ibariki Tanzania.
 
Nchi yetu ni tajiri hivyo viongozi wake lazima walipwe kitita au walipwe kitajiri,pia inawezekana kusema Tanzania ni masikini tajiri.
 
Wana jamii naomba kujua kwa usahihi mishahara ya wabunge na posho za vikao vya kawaida na za kwenye kamati,na viongozi wengine kama vile Rais,Waziri Mkuu,mawaziri n.k.Na nipate kujua kama mishahara yao inakatwa kodi (income tax) kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine.

Lengo ni kutaka kulinganisha na wafanyakazi wengine. Maana inawezekana tukawa tunaishi katika nchi mbili tofauti ndani ya nchi moja.Na hapa chini ni mshahara wa mtumishi wa serikali (local government) mwenye TGS D1;

BASIC SALARY TSHS 401,880
TALGWU CONTRIBUTION TSHS 8,037
INCOME TAX TSHS 37,464
LAPF PENSION TSHS 20,094
NHI TSHS 12,056

Naomba kuwasilisha
 
Kuna sheria iliyotungwa katika enzi za ukweli na uwazi inayokataza kuzungumzia mshahara wa rais, hivyo chukua tahadhari vinginevyo unaweza kupambana na mkono wa sheria.
 
BASIC SALARY TSHS 401,880
TALGWU CONTRIBUTION TSHS 8,037
INCOME TAX TSHS 37,464
LAPF PENSION TSHS 20,094
NHI TSHS 12,056

kwa nini isiongezwe hii maana naona kama ndogo ukiangalia na idadi ya wachangiaji
 
Raisi analipwa lakini akitaka pesa yoyote anachukua tu hakuna wa kumzui
Af hao mawaziri wanakula ml 12@Month nao wakitaka zaidi wanasaini mikataba hewa, na kuhitaji pesa wizarani zisizo hitajika wanapata zaidi hata ya mishahara hao ma ceo ni kuanzia 5, 6 mpaka 7 mls @moth na bado wizi uko palepale.

In general hawa jamaa mishahara yao ni ya kawaida sema wana vyanzo vingi vya kupata pesa viwe halali au vya wizi na wanamake kuliko hiyo mishahara yao
 
Back
Top Bottom