Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Ibrah,
Asante. Sidhani kama nina ugomvi binafsi na Spika. Hoja ni kuwa niliousema ni mshahara na posho ya kwangu. Ni hiari yangu kuisema kwa yeyote na kwa wakati ninapopenda, na hasa kwa wale ambao wanalipa kodi ili nilipwe posho hizo. Nikihukumiwa kwa hilo niko tayari kwa hatua yeyote ile itakayoamuliwa. Lakini ukweli umesemwa.

Mbona hujaikataa? unaipokea kama kazi!
 
Ndo maana doctors, engineer na wengine wenye proffesional zao wameamua kukimbilia kwenye siasa maana huko ndiko kwenye pesa, na tusipo badilika tutajikuta hatuna hata mtaalamu yeyote wa maana wa kuleta maendeleo,na hii ni hatari mi naomba jamani hata sisi wataalamu tuna familia kama hao wabunge,ni kwanini pawepo na gepu kubwa namna hiyo?ina niuuma sana ila kwa mtaji huo rushwa hapa ndo nyumbani kwake,
 
Breakdown............

Bei ya Mafuta katika vituo vya mafuta ni kati ya shilingi 1,200 kwa jiji la Dar es Salaam na shiling 1,500 kwa mji wa Musoma, Mbunge amekuwa akipata lita moja ya mafuta kwa shilingi 2,500 ikiwa ni shilingi elfu moja juu zaidi kwa gharama ya Musoma ambayo ni mji wenye bei ya juu ya mafuta aina ya petroli.

Kama hiyo haitoshi, Mbunge mmoja anapatiwa Lita 1,000 za mafuta kila mwezi ambapo kiasi hicho ni sawa na Sh 2,500,000. Licha ya fedha hizo, kila Mbunge sasa anapewa asilimia 40 ya fedha hizo kwa ajili ya matengenezo ya magari yao, kiasi ambacho ni sawa na Sh 1,000,000.

Kiasi hicho cha fedha ni mbali na Sh 765,000 kwa ajili ya matumizi ya ofisi yake kwa mwezi, na pia anapatiwa mshahara wa dereva kiasi cha Sh 100,000 kila mwezi.

Malipo haya hayaisihii hapo, bali mbunge sasa anapata Sh 300,000 kama posho kwa ajili ya dereva wake kila mwezi kwa ajili ya kutembelea jimbo. Kwa maana hiyo dereva wa Mbunge anapaswa kulipwa Sh 400,000 kila mwezi kutoka kwa Mbunge.

Mbunge pia anapewa kiasi cha Sh 45,000 kila siku kwa muda wa siku 10, ambapo anapaswa kutumia fedha hizo kutembelea jimbo kila mwezi. Kwa ajili ya kazi hii jumla anapewa Sh 450,000 kila mwezi kwa ajili ya kutembeelea jimbo.

Mshahara wa mbunge nao umeogezeka sasa kutoka Sh 1,200,000 walizokuwa wanalipwa awali na kuwa Sh 1,800,000. Jumla kwa mwezi Mbunge anapata Sh 6,915,000 kutoka serikalini.

Magari hayo wanayoendesha wabunge kila miaka mitano huwa wanakopesha Sh 40,000,000 kwa ajili ya kununua gari analotumia kwa muda wote wa miaka mitano anayokuwa bungeni.

Hata hivyo, wabunge wanapata mafao zaidi ya hayo kwani kwa muda wanaokuwa bungeni hupata posho za vikao kwa wastani wa Sh 100,000 kila siku na hiyo haiesabiki katika sehemu ya malipo yaliyotajwa hapo juu.

Bunge linalipa $ 7,000 kila mwezi kwa ajili ya nyuimba anayoishi Spika wa Bunge, Samwel Sita. Nyumba ipo Masaki. Nyumba iliyokuwapo awali, ilinunuliwa na Spika wa Bunge aliyemaliza muda wake, Pius Msekwa.
 
Invisible shukrani kwa hizi data za Wabunge, inatia kichefuchefu kama sio kuudhi kabisa. Hivi mishahara ya wabunge wanakatwa kodi?

Lakini tuseme kweli hata wapinzani kwa hili WAMETOKOTA kama sio KUCHEMKA, hizi fedha ni nyingi sana kulipwa mtu mmoja, hakuna "justifications" kwa hilo, kwamba Mbunge apate fedha yote hiyo, halafu mwingine alipwe kima cha chini 100,000 kwa mwezi.
 
Kilichoniudhi ni nyumba ya spika?Yaani nyumba waliuza then wanarudi kupanga!Ama kweli hii serikali hii ilichemka!

Pia hawa wabunge wanapewa posho ya kutembelea bunge kila mwezi! MBUNGE wetu mzee wa vijisenti sijawahi muona kila mwezi akiwa Bariadi!

Pia wabunge wengi wanaishi bongo tu!hiyo hela ya mafuta wanatanulia bongo tu!
Inauma sana!
 
Yaani pose hii karibu yote ni tax free!

Inayokatwa kodi ni 1,800,000 Tu ya mshahara.. na hii hukatwa 30-35%

Yaani mbunge wa Tanzania ktk 7.000.000 Tshs hulipa kodi kama 350.000 Tu au 05% ya mapato

Taabu ya Tz posho/masurufu ni mara 3 ya mshahara na sheria inasema posho isitozwe kodi!

Muhim hapo ni kubadili sheria ili posho nazo zitozwe kodi!
 
Haya,haya wandugu wenye nazo,wekeza katika kugombea ubunge 2010.Mimi Makalangilo nafikiria kuwania nafasi hiyo katika Wilaya ya Ilemela hapa Mwanza,lakini Diallo ana mihela ya kuhonga na Tv ya kumtangazia,hapo sina ubavu.Sijui nigombee udiwani?Najua nako kuna hela ingawa si kama za wabunge!

Na wale wa Ng'wana Lipumba,Maalim Seif,Mbowe na wengine achana na Urais! Pigania ubunge bwana ndiko kwenye hela!

Na wananchi nyinyi bakini na umasikini wenu kwa maana mnjitakia wenyewe.Mnachagua mafisadi wanajazana bungeni!
 
WAKATI Bunge zima likimwandama Mbunge wa Karatu, Dk. Wilibrod Slaa (CHADEMA), kutokana na msimamo wake kuwa posho za wabunge ni kubwa na kutaka zipunguzwe, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameungana na wabunge wengine kwa kusema kuwa posho hizo ni ndogo na kutaka ziongezwe.

Ingawa hakutaja jina, lakini kauli hiyo ya Waziri Mkuu imeonekana dhahiri kumjibu Dk. Slaa anayetaka mishahara na posho za wabunge zipunguzwe, kwamba ni kubwa mno ukilinganisha na watumishi wengine wa umma.

Pinda aliyasema hayo jana mjini hapa wakati akizindua mpango mkakati wa Bunge wa miaka mitano, wenye nia ya kulifikisha Bunge katika kiwango cha juu cha ufanisi.

Katika uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa mjini hapa, Pinda alitumia mwanya huo kuchomeka suala la posho za wabunge, ambalo limekuwa agenda kubwa katika mkutano wa 15 wa Bunge unaomalizika leo.

Akielezea hatua ambazo serikali imekuwa ikizifanya kwa upande wa Bunge, Pinda ambaye aliorodhesha hatua kadhaa za kuboresha maslahi ya Bunge, alisema lengo la serikali ni kuboresha maslahi na posho za wabunge ambazo kwa sasa bado ni ndogo.

“Lengo la serikali kwa Bunge ni kuboresha maslahi na posho za wabunge ambazo kwa kweli kwa sasa hazifikii stahiki, lengo ni kuhakikisha Bunge linaboreshewa maslahi ili liweze kufanya kazi yake stahiki na kwa kiwango cha kuridhisha,” alisema Pinda.

Awali, akizungumzia malengo makubwa saba ya mpango mkakati huo, alisema moja ya malengo hayo ni kuboresha maslahi na stahiki za wabunge ili kuliwezesha Bunge kutekeleza majukumu yake ya kikatiba ipasavyo.

Mbali na malengo hayo, mengine ya mkakati huo ni kuboresha muundo na utendaji wa ofisi za Bunge ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji, pia kuboresha mazingira ya utendaji kazi ya sekretarieti ya Bunge.

Limo pia suala la kukuza na kuimarisha ushiriki wa Bunge kuwafikia wadau mbalimbali kupitia mikutano, machapisho, vyombo vya habari na njia nyingine ya mawasiliano, pamoja na kukuza na kuinua vipaji vya wabunge.

Kwa upande wa serikali, mbali na malengo ya kuboresha maslahi na posho za wabunge kwa kuzingatia mazingira ya utendaji wao wa kazi, na hali ya uchumi, Pinda pia aliyataja malengo mengine kuwa ni kuwezesha Bunge kuwa na ukumbi mzuri wa kisasa unaotosheleza mahitaji, lengo ambalo kwa sasa tayari limekwishatekelezwa.

Kwa mujibu wa Pinda, lengo lingine ni kuanzishwa kwa mfuko maalumu wa Bunge ambao ulianza kutumika mwaka 2007/08, kuwashirikisha katika ziara za nje za viongozi wa kitaifa, lakini pia kuharakisha ujenzi wa ofisi za wabunge katika majimbo yao.

Tangu alipotoa kauli hiyo akiwa kwenye moja ya mikutano ya chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, amekuwa akiandamwa na wabunge wenzake katika mkutano huu wa 15, wakipinga hoja hiyo kwa madai kuwa inawachonganisha wabunge na jamii.

Hali hiyo ilisababisha Dk. Slaa afikie hatua ya kuzomewa mara kadhaa kila jina lake linapotajwa kwenye vikao vya ndani na nje.

Mbunge huyo, hata hivyo, alisisitiza kwamba anasimama katika hoja zake, ikiwamo ya posho za wabunge kutaka kutazamwa upya.

Alisema ataendelea kuisimamia hoja hiyo kwa sababu anataka kuwapo kwa uwazi katika mishahara wanayolipwa viongozi mbalimbali wakiwamo wabunge.

source;Tanzania Daima.

My take
Hivi ni kweli Pinda ni mtoto wa mkulima?
Ameacha kutetea mishahara ya watumishi wa ngazi za chini ambao maisha yao yamekuwa ya kukopa kopa na mshahara unaishia kulipa madeni ya mwezi uliopita..watumishi hawa ambao kwa kweli wanaishi maisha ya hali ya nchi sana kulingana na mishahara wanayo pata serikalini kama walimu,manesi,polisi na wengine neo.
Pinda umeshindwa kuwatetea hawa wanyonge umeamua kutetea ulaji wa tumbo lako,hivi haya mamilioni mnayo pewa kwa mwezi ukigawa utawalipa walimu wangapi kwa hiyo milioni 7? kwa mshahara wa 200,000/= naamini Pinda umepotoka na nina amini wewe sasa ni mtoto wa Bepari si mkulima tena.
 
Baada ya hayo matamshi ya Pinda, ninahamu ya kujua manesi, polisi, walimu watamwambia nini. Watanywea au watamtolea uvivu?
 
“Lengo la serikali kwa Bunge ni kuboresha maslahi na posho za wabunge ambazo kwa kweli kwa sasa hazifikii stahiki, lengo ni kuhakikisha Bunge linaboreshewa maslahi ili liweze kufanya kazi yake stahiki na kwa kiwango cha kuridhisha,” alisema Pinda.

Sawasawa mheshimiwa. Lakini tukumbuke money is never enough in any situation. Hakuna mtu duniani aliyewahi kujitokeza akasema mimi nina hela za kutosha.

Kwa hapa Tanzania, kuna watu wengi sana wanaohitaji nyongeza ya kipato kuliko wabunge. Kwanini hawa wasifikiriwe kwanza?

Kwa mtazamo wangu, wabunge ndo wawe watu wa mwisho kabisa nchini kupata nyongeza ya kipato.
 
Pinda sio tu kwamba haelewi bali hajui wala hafahamu. Tatizo hapa sio kwamba hiyo mishahara ya wabunge ni mikubwa bali ni mikubwa mno ukilinganisha na mishahara ya wafanyakazi wengine wa serikali. hasa madaktari, waalimu, polisi, jeshi, na watumishi wengine wengi serikalini.

Vile vile haina uwiano na mapato ya nchi na haizingatii maisha ya mtanzania wala pato halali la mtanzania. sasa kama mbunge hawezi kuishi kutokana na pato la nchi kweli ataweza kuwa na fikra za kuisaidia nchi yake. Hili ni tatizo la watu kugeuza siasa ndio ajira.

Pale wanapo fanya utafiti wa mishahara yabunge wakilinganisha na lile la uingereza nafikiri tunaona jinsi gani bunge limekuwa la kifisadi. bunge na wabunge wameamua kumfanyia mwananchi ufisadi kwenye kodi zake.
Ama kweli kila kitu chini ya jua ni ubatili mtupu.Ubatili ubatili mtu.

Sioni sababu gani , Polisi, wanajeshi, waalimu, madaktari,manesi,nk wasigome kudai nyongeza ya mishahara kwani wanayolipwa huwezi kuishi hata wiki moja. Waitishe migomo ya kitaifa kudai nao walipwe angalau robo ya mishahara ya wabunge wao na kuzingatia hali halisi ya maisha ya tanzania na bei na mifumoko yake.
 
Baada ya hayo matamshi ya Pinda, ninahamu ya kujua manesi, polisi, walimu watamwambia nini. Watanywea au watamtolea uvivu?

Hawa watu mi siku zote iwa nawaonea huruma sana wanaishi maisha ya chini mshahara wenyewe ndo kama hivi mwalimu hata malupulupu hapewi na ndo hawa hawa kipindi cha uchaguzi wanawatumia ili wapite na kwenda kuongeza miili na matumbo yao sehemu ya kupigia porojo bungeni inauma sana.,
 
Pinda sio tu kwamba haelewi bali hajui wala hafahamu.

Anaelewa na anafahamu sana. Ila ni mtumwa tu.

sasa kama mbunge hawezi kuishi kutokana na pato la nchi kweli ataweza kuwa na fikra za kuisaidia nchi yake. Hili ni tatizo la watu kugeuza siasa ndio ajira.

Hapana mkuu, hili ni tatizo la watu kutowasimamia na kuwawajibisha wanasiasa. Watu wanadhani wanasiasa ni baba na mama zao. Ngoja uone 2010.

Sioni sababu gani , Polisi, wanajeshi, waalimu, madaktari,manesi,nk wasigome kudai nyongeza ya mishahara kwani wanayolipwa huwezi kuishi hata wiki moja. Waitishe migomo ya kitaifa kudai nao walipwe angalau robo ya mishahara ya wabunge wao na kuzingatia hali halisi ya maisha ya tanzania na bei na mifumoko yake.

Hapa ndipo tatizo jingine lilipo. Either hawa watu bongo zao zimelala au wanaridhika na rushwa/hongo wanazotukamua.
 
Hawa watu mi siku zote iwa nawaonea huruma sana wanaishi maisha ya chini mshahara wenyewe ndo kama hivi mwalimu hata malupulupu hapewi na ndo hawa hawa kipindi cha uchaguzi wanawatumia ili wapite na kwenda kuongeza miili na matumbo yao sehemu ya kupigia porojo bungeni inauma sana.,

Labda wanastahili kutumiwa na kupewa mishahara ya chini. Afterall, wanasema "you get what you bargain for".
 
Baada ya hayo matamshi ya Pinda, ninahamu ya kujua manesi, polisi, walimu watamwambia nini. Watanywea au watamtolea uvivu?

Mkuu heshima mbele, mimi nafikiri hiyo kusema kwamba mishahara haitoshi inataka kuongezwa ni issue ya kisiasa tuu na kumkandamiza Slaa iliaonekane kituko kwa sasa mbele ya wabunge wenzie
 
Labda wanastahili kutumiwa na kupewa mishahara ya chini. Afterall, wanasema "you get what you bargain for".

Mi nakwambia ili tuendelee na tupige hatua inatupasa tukipotezee kizazi hiki kilichopo kwenye siasa sasa hivi..vinginevyo tutaendelea kufanya maigizo na kuchekwa na nchi jilani.
 
Mkuu heshima mbele, mimi nafikiri hiyo kusema kwamba mishahara haitoshi inataka kuongezwa ni issue ya kisiasa tuu na kumkandamiza Slaa iliaonekane kituko kwa sasa mbele ya wabunge wenzie

True ni ishu ya kisiasa. Haina ukweli wowote. Ndo maana ni hoja dhaifu sana. Na inazidi kumuongezea Slaa umaarufu.

Tatizo wale walengwa wenye vipato vya chini wako kimyaaaaa!! Wanalalamika chinichini tuu! Mpaka hali ikiwa mbaya saaaaana ndo wanagoma. Kisha wataongezewa makombo afu watatulia huku wakiendelea kunung'unika chinichini.
 
True ni ishu ya kisiasa. Haina ukweli wowote. Ndo maana ni hoja dhaifu sana. Na inazidi kumuongezea Slaa umaarufu.

Tatizo wale walengwa wenye vipato vya chini wako kimyaaaaa!! Wanalalamika chinichini tuu! Mpaka hali ikiwa mbaya saaaaana ndo wanagoma. Kisha wataongezewa makombo afu watatulia huku wakiendelea kunung'unika chinichini.

Hawa jamaa wanacho kifanya sasa ni kucheza rafu mbaya ambayo wengine watapewa kadi nyekundu majimboni mwao zaidi zaidi wanamwongezea umaarufu Slaa na kufanya akubalike zaidi mi nashangaa huyu mtoto wa Mkulima naye anapigia debe posho ziongezwe kweli pesa tamu.
 
Duh, si utani kweli "Mwamba ngoma, ngozi huivutia kwake"... Yaani wakuu wetu badala ya kuangalia namna ya kusazisha vipato (wao wana pocket 7m plus, as per some thread in here) mwalimu, polisi, daktari etc etc etc wengi tupo huku kwenye kajilaki kamoja na ushee, wao wanabakia kujiongezea maradufu??

Priorities, priorities, priorities......
 
Back
Top Bottom