Chikumba one
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 1,009
- 1,642
Kuna kitu watu hawakijui kuhusu wachezaji na timu zao! Kuanzia kwenye usajili mpaka mishahara ya wachezaji ma star wa Simba na Yanga huwa wanagawana na baadhi ya viongozi wa hizo timu hasa wanaofanikisha usajili wao!
Hapo kwenye mshahara wa Niyonzima si ajabu pesa yake ni milioni 5 ama 6. Nyingine ni mali ya viongozi waliomsaidia kupata kazi hapo Simba!
Mchezo huu upo hadi kwa timu za mikoani!
Mmoja wa waathirika wa mchezo huu ni Mdogo wangu mwenyewe! Aliponieleza hili nilisita kumwelewa, lkn baada ya kunionyesha ushahidi wa miamala ya mgao aliotoa kwa viongozi wake nikabaki nashangaa!
Mwanzoni nilikuwa najiuliza, ukiacha wafadhili wa kihindi kwenye timu zetu, hawa viongozi waswahili huwa wanagombania nini kwenye hizi timu?
Kwa sasa nawaelewa! Ukiwa na mgao wako kwa wachezaji watatu tu huitaji kufanya kazi nyingine!
Ndo sababu inapotokea mchezaji flani haelewani na Kiongozi flani, hata kama ana kiwango uwanjani, atafukuzwa pasipo heshima!
Ukiwa mchezaji ukapingana na hii tabia katika hizi timu, kamwe hutoendelea kuzichezea!