Mishahara ya wake zetu

Kong!!!!!!!!! Kwani kichwa cha nyumba ni nani? kama huwezi kuwa kichwa cha nyumba siyo bora usiwe na hiyo nyumba kuliko kutegemea mama na watoto wakuongozee nyumba.
 
Maisha kusaidiana na kujisaidia, hata kama huuoni mshahara wa mkeo ujue unamsaidia yeye mwenyewe kwa matumizi yake binafsi hivyo amekupunguzia gharama za shopping..
 
hata mwanamke awe waziri (mshahara mkubwa kiasi gani) na mwanamme awe mwendesha mkokoteni (mshahara mdogo kiasi gani), bado mwanaume ndie atakaewajibika kwa matumizi ya ndani! ni moja kati ya vitu vinavyosababisha migogoro ndani ya ndoa maana ni lazime utamuuliza, na ukishamuuliza huyo mwanamke atanuna wiki nzima na vyote likizo ie unyumba n.k.
ndoa za sasa ivi, Mungu ashushe rehema zake tu lakini kazi nzito!!!!
 

kuzaa kwa uchungu??? mtaalamu inaonekana upo nyuma kitechnolojia, binti gani wa kizazi hiki cha dotcom ambao hata kupika chai hawezi akazae kwa uchungu??????????
 
Mshahara ni mali ya anayelipwa wadau cha maana ni kujua jinsi ya ku strike a fine ballance ili mambo yaende kwa mujibu wa kipato............hakuna formula wala principles or rights za mume kuhoji kipato ya mkewe na jinsi anavyotumia it all depends on how you two guys makes it happen.......Ila ukiwa kama father house wakati mkeo kalala wewe unatunga mikakati ya kufanya mambo yaende sio ukorome kuliko watoto halafu uje utoe macho mwisho wa mwezi

Wao hutumia mioyo na miili yao kuweka nyumba sawa sisi wababa tutumie miili na akili zetu kuhakikisha usalama wao na watoto
 
kama ataki kushare salary, basi na wewe wako usitumia kila mtu ale mshaala wake

...................JINO..... kwa..........JINO bana......., ndiyo maisha ya Dot.COM

He jamani baba ni kichwa cha nyumba, mimi nasaidia tu palipopelea, mbona wakati hujanioa ulikuwa uantoa tu bila kuniambia nichangie bill, kwa kifupi mmetuzowesha wenyewe....
 
Anadamka asubuhi kwenda kibaruani, anachelewa kurudi kibaruani sababu ya foleni afu nisiujue mshahara wake na unatumikaje?....... I better marry my mom!

Othetwise akae nyumbani anilelee wanangu.... PERIOD!

Kumbe na wewe ni mkatili, kukaa nyumbani inachosha jamani...
 
duh . . . . .
Kuna wanawake wana properties za kufa mtu.


Sasa tufanyeje kama wana mali. sikia mkuu/sister iyo siyo issue kama una mali alafu upati chachandu/n'yan'ya chungu....................nitarudi badae........ngoja nipige mbizi kwanza

 

tena ukitaka kusimamngwa ulizia mshahara wake, mshahara wao wanjua wenyewe wanautumia kuufanyia nini na sio kuendeleza familia yenu
 
Maisha kusaidiana na kujisaidia, hata kama huuoni mshahara wa mkeo ujue unamsaidia yeye mwenyewe kwa matumizi yake binafsi hivyo amekupunguzia gharama za shopping..



Wewe akili yako ndogo kama "pelege" au "kamongo" maana unacho ongea ukielewi, kama unajuwa mshaala wako ni wako pee,

Qn. kwanini ulikubali kuolewa naye kwanini usingekaa alone ukafaidi matumizi yako pekee. iyo ndiyo akisawa mnayo lilia everday acha mbwembwe na acha tabiaya ya hooogoo?.

nakasubilia kwa haamu sana ikikupeni njoo tuongee
 
yesu na maria!!!!!!!!!!!!!!nilimuoa yeye si kwa uzuri wake alio nao ingawa compatibility ni kigezo.Nilimuoa kwa kuwa yupo wise kifikra,utashi,na wengi ni wafanyakazi.Hivyo basi mapato ya mshahara wake kama hayatumiki kwenye dhana nzima ya kuendeleza familia atakuwa anachezea pesa yangu kama wazee wa mjengoni wanavyochezea pesa za walipakodi asepe tena achape mwendo kama treni ya umeme
 
Kama ni hivi, Kwa sisi ambao bado hatujaoa inabidi tuanze kuwazoesha tulio nao sasa. Kuanzia kesho ntamwambia demu wangu mshahara wake aweke mezani nimpangie matumizi.
 
 
fuata ya maandiko uache kuchangia matumizi ya familia na kusomesha watoto kwa kushirikiana na mumeo ili uje ujionee vizuri mtakapo nyang'anyana hereni na mumeo matatizo yatakapomuelemea.jiangalie sana atashindwa kukuzalishia megawatts kwenye umeme wa grid ya taifa msongo wa kilovolts ulizozoea siku zote kwani bwawa la mtera litakuwa limeshajaa tope na mitambo ya kusukuma maji yaingie kwenye turbines itakuwa functionless na chakavu kabisa
 

pamoja mkuu, Jino KWA Jino ndyo mpango mzimaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!.

 

Dunia imebadilika kwanza hilo tulijue.
Hapo mwanzo Mungu alipoweka mgawanyiko wa majukumu-Adamu kwa jasho utakula na wewe Hawa kwa uchungu utazaa, mambo yalikuwa kama hivyo . Waume mashambani na wanawake majumbani kuzaa na kulea watoto. Ila ninaposema dunia imebadilika ni kwamba haya nayo yamebadilika.
Leo hii wanawake si lazima wazae kwa uchungu- Tunashuhudia operations nyingi wakati wa kujifungua , wasichana wengi wanazaa kwa visu. Hapo hakuna Uchungu uliosemwa na Muumba.
Hali ya maisha/Uchumi unamlazimisha mwanamke atafute kazi. Wengi wameenda shule na kupata nafasi/ madaraka makubwa.

Kwa maana hiyo basi Mshahara wa mwanamke unapaswa kuingia katika mipango mizima ya kuinua familia kiuchumi.Nasema hivi kwasababu zile roles zilizokuwepo zamani zimebadilishwa na binadamu kubadilishwa (kwa kupenda au kutokupenda) na mabadiliko ya dunia (ya kiuchumi, kijamii kama elimu n.k)

Kwa busara kabisa mshahara wa mwanamke lazima utumike kuijenga familia (kidole kimoja hakivunji chawa) Hii haimaanishi heshima ya baba kama kichwa cha nyumba itaondoka.
Ila cha kuzingatia mchango wa baba uonekane zaidi, siyo akae tu kusubiri mshahara wake na wa mkewe awe na akili ya ziada ya kujishughulisha na kuleta ziada nyumbani.Hii inatokana na ukweli kwamba physical ability alio pewa na Mungu unamfanya afanye zaidi kuliko mkewe.
Let say kama ni fundi ujenzi wa kulipwa anaweza kujishughulisha na ziada ya kubeba zege kama kibarua kingine kuleta ziada atleast na tofauti yake na mkewe.



 
Kama ni hivi, Kwa sisi ambao bado hatujaoa inabidi tuanze kuwazoesha tulio nao sasa. Kuanzia kesho ntamwambia demu wangu mshahara wake aweke mezani nimpangie matumizi.


Pomoja JEMBE LANGU, usikubali kulea uvundo, izo style zilikuwa inzi cha teacher(msoma)

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…