Mishahara ya watumishi wa umma inapaswa ifanyiwe mapitio, haiakisi uhalisia wa maisha ya sasa

Aramun

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2023
Posts
461
Reaction score
2,213
Asilimia 90 ya watumishi wa umma Tanzania ni wa daraja la kati, wengi ni walio na diploma. Mishahara ghafi yao ina range laki 6 mpaka laki 8.

Baada ya makato, wanaondoka na kama laki 5. Hapo ni kwa wale ambao hawana mikopo. Ukijumlisha mikopo (ambao wengi wanayo) utakuta mtumishi anaondoka na laki 2, 3. Ukiangalia salary slip ya mtumishi wa umma wa sasa unaweza usiamini hayo makato yaliyomo humo ndani.

Utumishi wa umma wa sasa si kama wa zamani. Zamani watumishi wa umma ndiyo walikuwa wanaonekana wana chochote kitu mtaani. Ila kwa sasa watumishi wa umma ndiyo wamegeuka wasio na chochote mitaani. Wengi wanaishi kwa msaada wa mkopo wa mangi.

Mtumishi wa umma wa sasa anashindwa pesa hadi na boda boda. Kama boda boda anaingiza mkwanja mrefu zaidi kumshinda mtumishi wa umma tunategemea nini kama nchi? Thamani ya utumishi wa umma inabidi ilindwe.

Kama hadhi ya utumishi wa umma haitalindwa, basi tusitegemee watumishi wa umma ku-deliver vile inavyotakiwa, na kwa sababu ya mishahara kiduchu tutegemee hizo ripoti za CAG zikiendelea kuwa chafu kwa ubadhirifu wa pesa za miradi.

Pamoja na mishahara kiduchu ila serikali ikaona iwawekee na kikokotoo kiduchu kwenye kiinua mgongo. Yani ni full mateso.

Kingine kinachotia hasira ni kwamba wanasiasa wao wamejiwekea mishahara minono, na marupurupu lukuki. Na wakistaafu wanachukua viinua mgongo vyao kama vilivyo tena on time.
 
Mama e kuliko kuongeza mishahara sibora waongeze ajira mtu unalialia na lak 5,8,Wakati watu wapo tu naajira ata ya cent mokon awajapata.
 
Imeshapitiwa na Bodi ya Mishahara, ni mkikubwa kulinganisha na sekta binafsi wakati utendaji ni chini ya 60%, walipaswa kupunguziwa mishahara.
 
Hizo ni tamaa Sasa.
Kwanza wapo wengi sana mshahara ikipanda itasababisha wengine wasiajiliwe maana hela itakuwa hamna.
Hivi kweli kabisa tangu aondoke JK mshahara wa mtumishi wa umma haijawahi kuongezeka? Nasikia hivyo na Kama ni kweli basi tatizo ni kubwa
 
Mshara unapanda karibu kila mwaka, haitangaZwi ili wafanya biashara wasipandishe bidhaa.
Wafanyakazi wa serikali wana marupurupu, wana nyumba, wana likizo zinalipwa, wana simu za bure na vocha bado hawaridhiki.
 
Achana na ile annual incriment Kuna kitu huitwa Salary incriment hii aliiweza JK peke yake.
Hiyo annual incriment tangu awamu ya tano hadi leo imetokea sio zaidi ya Mara tatu
 
Asilimia 90 ya watumishi wa umma Tanzania ni wa daraja la kati, wengi ni walio na diploma. Mishahara ghafi yao ina range laki 6 mpaka laki 8.

Baada ya makato, wanaondoka na kama laki 5. Hapo ni kwa wale ambao hawana mikopo. Ukijumlisha mikopo (ambao wengi wanayo) utakuta mtumishi anaondoka na laki 2, 3. Ukiangalia salary slip ya mtumishi wa umma wa sasa unaweza usiamini hayo makato yaliyomo humo ndani.

Utumishi wa umma wa sasa si kama wa zamani. Zamani watumishi wa umma ndiyo walikuwa wanaonekana wana chochote kitu mtaani. Ila kwa sasa watumishi wa umma ndiyo wamegeuka wasio na chochote mitaani. Wengi wanaishi kwa msaada wa mkopo wa mangi.

Mtumishi wa umma wa sasa anashindwa pesa hadi na boda boda. Kama boda boda anaingiza mkwanja mrefu zaidi kumshinda mtumishi wa umma tunategemea nini kama nchi? Thamani ya utumishi wa umma inabidi ilindwe.

Kama hadhi ya utumishi wa umma haitalindwa, basi tusitegemee watumishi wa umma ku-deliver vile inavyotakiwa, na kwa sababu ya mishahara kiduchu tutegemee hizo ripoti za CAG zikiendelea kuwa chafu kwa ubadhirifu wa pesa za miradi.

Pamoja na mishahara kiduchu ila serikali ikaona iwawekee na kikokotoo kiduchu kwenye kiinua mgongo. Yani ni full mateso.

Kingine kinachotia hasira ni kwamba wanasiasa wao wamejiwekea mishahara minono, na marupurupu lukuki. Na wakistaafu wanachukua viinua mgongo vyao kama vilivyo tena on time.
Usishangae hata unaowatetea watakupinga na kukushambulia
Uchawa mbaya sana
 
Kazi hamfanyi mkifika ofisini mpo busy kuchat arafu mnadai mishahara iongezwe kwa kazi ipi mnazofanya
Walipaswa waombe kupunguziwa mishahara, hivi uliona kule Longido Makonda anamuuliza msimamizi kituo cha afya eti hawafanyi kazi wanasubiri bajeti ya laki moja kuja kuweka mafuta na chumvi kwenye jenereta.
 
Fanya kazi acha kulialia...ukipata mshahara tafuta chanzo kingine cha mapato, ukiona huwezi acha kazi
Kutafuta chanzo kingine cha mapato ndio hatari zaidi katika utumishi wa umma. Huwezi kutumikia sehemu mbili na zote zikawa na ufanisi mkubwa, hivyo kazi ya utumishi wa umma utakuwa na ufanisi mdogo kuliko kazi yako uliyoiwekea hela/uwekezaji.
 
90% ya watumishi wa umma ni walimu, watu wa afya.

Hao watu maisha yao ni magumu balaa. Mishahara midogo sana.

Wafanyakazi wote wa umma walioko kwenye wizara, halmashauri maisha yao ni magumu sana, mishahara midogo sana na hakuna posho wala marupurupu.

Ni asilimia chache sana ya watumishi wa umma wanaokula mema ya nchi mfano walioko TRA, Ewura, Tanesco, REA, NIC, TIRA, nk. Hao mishahara yao angalau ni mizuri na wengine ni mizuri sana.

Najua concern ya serikali ni kwamba kuongeza mishahara kwa hao 90% ya watumishi ita sky rocket wage bills or payroll cost na utajikuta makusanyo yote yanaishia kwenye payroll.

Serikali iangalie namna ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma.
 
Back
Top Bottom