Mishahara ya watumishi wa umma inapaswa ifanyiwe mapitio, haiakisi uhalisia wa maisha ya sasa

Asilimia 90 ya watumishi wa umma Tanzania ni wa daraja la kati, wengi ni walio na diploma. Mishahara ghafi yao ina range laki 6 mpaka laki 8.

Baada ya makato, wanaondoka na kama laki 5. Hapo ni kwa wale ambao hawana mikopo. Ukijumlisha mikopo (ambao wengi wanayo) utakuta mtumishi anaondoka na laki 2, 3. Ukiangalia salary slip ya mtumishi wa umma wa sasa unaweza usiamini hayo makato yaliyomo humo ndani.

Utumishi wa umma wa sasa si kama wa zamani. Zamani watumishi wa umma ndiyo walikuwa wanaonekana wana chochote kitu mtaani. Ila kwa sasa watumishi wa umma ndiyo wamegeuka wasio na chochote mitaani. Wengi wanaishi kwa msaada wa mkopo wa mangi.

Mtumishi wa umma wa sasa anashindwa pesa hadi na boda boda. Kama boda boda anaingiza mkwanja mrefu zaidi kumshinda mtumishi wa umma tunategemea nini kama nchi? Thamani ya utumishi wa umma inabidi ilindwe.

Kama hadhi ya utumishi wa umma haitalindwa, basi tusitegemee watumishi wa umma ku-deliver vile inavyotakiwa, na kwa sababu ya mishahara kiduchu tutegemee hizo ripoti za CAG zikiendelea kuwa chafu kwa ubadhirifu wa pesa za miradi.

Pamoja na mishahara kiduchu ila serikali ikaona iwawekee na kikokotoo kiduchu kwenye kiinua mgongo. Yani ni full mateso.

Kingine kinachotia hasira ni kwamba wanasiasa wao wamejiwekea mishahara minono, na marupurupu lukuki. Na wakistaafu wanachukua viinua mgongo vyao kama vilivyo tena on time.
Watumishi wa umma ni wengi sana serikali ikisema kima chani kiwe 1.5M au 2M haitaweza kulipa hiyo mishahara

Labda waongeze privilege Kwa watumishi wa umma
 
Ukiona idara unayofanya kazi mshahara mdogo tambua wewe ni mtoa huduma huingizii chochote serikali unataka tukupe mshahara mkubwa kwa kipi mbona siye

TRA
TPA
TANESCO
TANAPA
Kwanini hatulalamiki tunaingizia serikali mapato kwaiyo inatujali sasa wewe mtendaji kata, afisa mifugo, mwalimu wa stadi za kazi unataka mshahara mkubwa wa nini kwa kipato kipi unachozalisha ebu muacheni mama afanye kazi
Khaa wewe vipi asee Taasisi karibia zote zinaingiza hela kupitia ukataji wa leseni, maduhuri, fees, sasa sijui unasemaje TRA na tanesco ndo wanaingizia hela wenyewe
 
🙂
 
Attachments

  • IMG-20240503-WA0000.jpg
    IMG-20240503-WA0000.jpg
    23.8 KB · Views: 12
Walipaswa waombe kupunguziwa mishahara, hivi uliona kule Longido Makonda anamuuliza msimamizi kituo cha afya eti hawafanyi kazi wanasubiri bajeti ya laki moja kuja kuweka mafuta na chumvi kwenye jenereta.
Sio sahihi aliyeshangaa ni RC Nawanda.alishangaa halmashaur wameshindwa hata kilo 5 za chumvi ilimkusudi wazimix na mafuta jenereta liwake wkakawa wameshidwa.
 
mimi nakula mshahara wa UMMA na naona siutendei haki, tunalipwa posho hata kikao cha kujadili kitasa cha elfu 10 posho elfu hamsini.
Nyumba na usafiri ninao wa umma.
Bado safari na likizo nalipiwa mimi na watoto wangu.
Huwezi kuwa kwenye level za watumishi wa umma wa halmashauri au walimu usijue nini kinaendelea kwenye maslahi yao ila sawa tu maisha hayajagqnda yanaendelea, hongera kwa unae kula keki ya nchi kwa kujinafasi ipo siku na sisi tutafika nchi ya ahadi.
 
Ukiona idara unayofanya kazi mshahara mdogo tambua wewe ni mtoa huduma huingizii chochote serikali unataka tukupe mshahara mkubwa kwa kipi mbona siye

TRA
TPA
TANESCO
TANAPA
Kwanini hatulalamiki tunaingizia serikali mapato kwaiyo inatujali sasa wewe mtendaji kata, afisa mifugo, mwalimu wa stadi za kazi unataka mshahara mkubwa wa nini kwa kipato kipi unachozalisha ebu muacheni mama afanye kazi
Wabunge wanaingiza nn? yapo mashirika yanaleta hasara miaka nenda rudi ila bado wanalipwa pesa ndefu ...Mishahara mikubwa inatokana uendeshaji na majukumu ya taasisi husika sio wnaaingiza kitu gani.

LATRA wana miashahara mikubwa kuliko TRA,. Je , nani anaingiza pesa kweny makusanyo? Zipo taasisi ndogo kama MSCL (shirika la meli ila wana pesa ndefu )
 
Watumishi wa umma ni wengi sana serikali ikisema kima chani kiwe 1.5M au 2M haitaweza kulipa hiyo mishahara

Labda waongeze privilege Kwa watumishi wa umma
Serikali inaweza kulipa kabisa , kama watakuwa na mipango madhubuti ...Zipo nchi zinalipa vizuri hata wastaafu wanalipwa bila ya kchangia mifuko
 
Asilimia 90 ya watumishi wa umma Tanzania ni wa daraja la kati, wengi ni walio na diploma. Mishahara ghafi yao ina range laki 6 mpaka laki 8.

Baada ya makato, wanaondoka na kama laki 5. Hapo ni kwa wale ambao hawana mikopo. Ukijumlisha mikopo (ambao wengi wanayo) utakuta mtumishi anaondoka na laki 2, 3. Ukiangalia salary slip ya mtumishi wa umma wa sasa unaweza usiamini hayo makato yaliyomo humo ndani.

Utumishi wa umma wa sasa si kama wa zamani. Zamani watumishi wa umma ndiyo walikuwa wanaonekana wana chochote kitu mtaani. Ila kwa sasa watumishi wa umma ndiyo wamegeuka wasio na chochote mitaani. Wengi wanaishi kwa msaada wa mkopo wa mangi.

Mtumishi wa umma wa sasa anashindwa pesa hadi na boda boda. Kama boda boda anaingiza mkwanja mrefu zaidi kumshinda mtumishi wa umma tunategemea nini kama nchi? Thamani ya utumishi wa umma inabidi ilindwe.

Kama hadhi ya utumishi wa umma haitalindwa, basi tusitegemee watumishi wa umma ku-deliver vile inavyotakiwa, na kwa sababu ya mishahara kiduchu tutegemee hizo ripoti za CAG zikiendelea kuwa chafu kwa ubadhirifu wa pesa za miradi.

Pamoja na mishahara kiduchu ila serikali ikaona iwawekee na kikokotoo kiduchu kwenye kiinua mgongo. Yani ni full mateso.

Kingine kinachotia hasira ni kwamba wanasiasa wao wamejiwekea mishahara minono, na marupurupu lukuki. Na wakistaafu wanachukua viinua mgongo vyao kama vilivyo tena on time.
Hao wana siasa, wengi walikuwa watumishi, Waka jamp upande wa pili, na wewe nenda kawe mwanasiasa,JPM, alikuwa mwalimu, Majaliwa mwalimu, Mama Sita mwalimu, na kuna mqprofesa kibaooo,
Hawapo pale kushufhulikia jinsi yq kuboresha maisha ya wananchi, wapo pale ku "improve" Level ya maisha Yao tu period! Sheria inapitishwa, wao wakiwepo, wananchi wakilalamika, na wao wanakuja wanashqngaa wanananza kuilaumu serikali!
Huwa, naangalia picha za Yule mbunge Kijana,Sanga anazo post mitandaoni! Hutaona akipost akiwa may be kwenye mafunzo ya kilimo Cha mpunga Japan, au USA, au kwenye shamba darasa pale SuA, au akitoa elimu ya kilimo Bora jimboni kwake, zaidi an akipost akiwa kapiga bring bring, kaegemea ndinga ya pesa mbaya,au akiwa mitaani huko majuu! Anatonyesha jinsi alivyofanikiwa kwa pesa ya umma/posho!
Kwa ufupi angefanya kama Ali hapi, anavyopost picha akiwa shambani!
 
Back
Top Bottom