90% ya watumishi wa umma ni walimu, watu wa afya.
Hao watu maisha yao ni magumu balaa. Mishahara midogo sana.
Wafanyakazi wote wa umma walioko kwenye wizara, halmashauri maisha yao ni magumu sana, mishahara midogo sana na hakuna posho wala marupurupu.
Ni asilimia chache sana ya watumishi wa umma wanaokula mema ya nchi mfano walioko TRA, Ewura, Tanesco, REA, NIC, TIRA, nk. Hao mishahara yao angalau ni mizuri na wengine ni mizuri sana.
Najua concern ya serikali ni kwamba kuongeza mishahara kwa hao 90% ya watumishi ita sky rocket wage bills or payroll cost na utajikuta makusanyo yote yanaishia kwenye payroll.
Serikali iangalie namna ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma.