Zamaulid
JF-Expert Member
- May 25, 2009
- 19,697
- 15,497
Aiss wewe kweli Mtoboa siriNyama ambazo wanatengeneza hizo mishikaki zinaitwa Salala, zinapatikana baada ya kuchuna ngozi ya ngo'ombe maana huwa zipo kwenye ngozi. Nyama yake ilivyo ni kama bapa hivi.Huwezi kuzipata Buchani lazima uende machinjioni.
Bei yake ni nafuu sio kama nyama ya kawaidia ndio maana hata mishikaki ya nyama hiyo ni nafuu.
Ukiacha hiyo mishikaki kwenye hivyo vijiwe unaweza kujipatia korodani za kuchoma za Ng'ombe, Nundu ya kuchoma ya Ng'ombe pamoja na Sabuufa ambayo ni mkusanyiko wa nyama nyingi zilizofungwa sehemu moja.