Mishkaki ya Tsh.100 Dar

Mishkaki ya Tsh.100 Dar

aisee inawezekana nimeigongagonga sana ukiweka na ile pilipili yao ya kutengeneza ukirudi ni maji meengi"mmh
huko mashariki ya mbali mbona hizo ni misosi yao mikubwa, maadam sio sumu wacha waendelee kujinoma :flypig:
 
Kuna miguu na vichwa vya kuku hapo ubungo,ni vitamu balaa!vimenisukuma sana hapo pamoja na mihogo ya kukaanga

hahahaha safi sana mkuu, zile kunguru huwa nzuri sana maana siku hizi tukizikaanga ni kama kuku wa Sea Clif
 
nyama zingine .za mbwa au paka so hakuna hasara .....
 
Tena pale coco beach kwenye mihogo nahisi ni mbwa ile kwa aliyekula pale anajuwa
 
Acha uoga mdogo wangu, kula kitu roho inapenda. Kukimbia vitu kwa visingizio kuwa ni vya barabarani halafu ukenda kula kuku wa Shoprite ambao wamechomwa sindano za kutunzia maiti si ndio umburula huo?
Nyama bei ghali buchani, lakini ukienda machinjioni Vingunguti au Gombs nyama bei poa tu na nyama safi kabisa, na ndio hizo wanazonunua wanaotuuzia sisi mishkaki ya mia kwenye chelewa.
Ukishindwa kusthimili na kupenda kula tu huenda ukala hata visivyofaa maana mji huo una mambo sana hasa nyama zakukuta barabarani ni hatari sana.
 
Poleni mnaoamini katika bei, vyakula vya supamaketi vinavyotoka nje vina bei kubwa lakini pia vina hatari ya kuwa vimeharibika (si unajua bongo kwa magumashi). Kama ulishikwa na hamu we ungekula tu, mbona poa...
nasikia huwa ni vitamu hasa.......

ila hiyo bei mi ndo ilinidiscourge kuna mahala nilipita watoto wa shule wamejazana wanasubiria mishkaki yao
 
Wakuu,huwa najiuliza kila siku,hii mishkaki [ya ng'ombe] inayo uzwa sh.100 maeneo mbalimbali ya dsm,wauzaji wanapata faida gani?
Maana ni vipande 5 vya nyama,tena vitam tu,
sasa kama kilo ya nyama ni sh.5000 hadi 6000,hawa wandugu wanafanya biashara ya aina gani?

Mungu wangu sio nyama ya ng'ombe ile wale wanauza nyama yeyote ile iwe mbwa paka nk, na kama ni nyama ya ng'ombe huwa ni kibudu au nyama zile ambazo ni reject, usile tena zina madhara
 
Mungu wangu sio nyama ya ng'ombe ile wale wanauza nyama yeyote ile iwe mbwa paka nk, na kama ni nyama ya ng'ombe huwa ni kibudu au nyama zile ambazo ni reject, usile tena zina madhara

Duuh...watu huwa wanavishambulia Sana barabarani.
 
Back
Top Bottom