Mishkaki ya Tsh.100 Dar

Eeh mi nikiziona napenda harufu yake but kula sijawahi naziogopa.

kuna sku nilitoka mbez beach usk nkakwama mwenge usku sa 4 narud tabata njaa ikanisakama hamad nkakutana na hzo nyama loh nilizila mpka bhaas tamu na skupata madhara na huwa nazila,ajabu nazpenda kuliko mishkak ya ukweli hahaha
 

mic u mume wangu
 
Dogo, machinjioni Vingunguti kuna nyama inauzwa kwa mafuku hadi buku. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi na hiyo nyama, ni nyama poa kabisa na salama kwa matumizi ya binadamu.
 
Kwa wanaoamini kwamba mishikaki ni ya Mbwa na Paka...., Hizi story kwa lugha ya kitaalamu ndio zinaitwa "Old Wives Tales..." Hivi kwa logic ya kawaida tu.., ni rahisi hivyo kumshika paka na kumchinja au ku-maintan supply ya nyama ya mbwa kila siku ili uweze ku-supply demand?

Utaona kwamba ni vigumu sana na kama ukibadilisha leo mbwa, kesho paka na keshokutwa nyama yoyote utakayoiona huoni kwamba mwisho wa siku watu watagundua taste ni tofauti..., ? Acheni utani, wewe mwenyewe jaribu kumshika paka let alone kumchinja ndio utagundua kwamba hizi story hazina logic...
 
hata mkisema mishkaki ya bundi hatuachi mnataka kutupa hasara kwenye mishkaki ya mia tano
 
Mungu wangu sio nyama ya ng'ombe ile wale wanauza nyama yeyote ile iwe mbwa paka nk, na kama ni nyama ya ng'ombe huwa ni kibudu au nyama zile ambazo ni reject, usile tena zina madhara
Umewahi kusikia yupi kapata madhara kwahizo nyama!? Acha kuponda kabiashara kawatu nao wanasaka tonge. Nasiyo ya paka au mbwa kama unavosema, wengi wao wanakuwa na oda toka machinjioni kwa bei so usiulize kwaswala la bei wanajua wao wauzaji amenunuaje na auzeje.
Kama wee huli sawa ila sikukamia biashara ya mtu hiyo ni dharau.
 
Umenikumbusha mbali mtoa mada niliwahi wauzia watu mshikaki wa nyama ya paka na mbwa lakin nlkuwa nkitia vitunguu swaumu kwa sana ili isigundilike wateja wangu waliisifia sana na nlipata faida kubwa .kuna siku kuna ng'ombe alkuwa amekiwa infection na bacillus anthrax sjajua kama nimepatia jina alikuwa ng'ombe wa jirani basi bwana mfugo aliagiza afukiwe Mara moja kwani ni hatar kwa afya basi mi nlkuwa nayasikia Yale maelezo maana nyumba zetu zipo karbu basi baada ya kufikiwa yule ng'ombe usiku nlienda mfukua nkamuosha nikamkata vipande vizur nkamuweka kweny freezer la jamaa ambaye anatuchaj kwa kuweka nyama kwa siku maana mm skuwa na freezer nilitumia umakin wa hali ya juu ktk kui handle ile nyamaa maana anthrax sio poa kesho nkaanga vipande vikubwa nikawa nauza mia mshikaki watu wakaanza jazana wengi punde si punde baada ya watu kula wakaanza kuharisha na kuumwa matumbo wengine kutoka na damu puani ilinibid nikimbie na pesa nikachukua wakati nakimbia jamaa RFK wa yule nlioweka nyama kwake akapiga simu akidai yule jamaa anaumwa mbaya sababu aliniibia kdogo nyama yangu nikakata Sm sikujibu chochote nikatafuta roli la mizigo nikaongea na dereva nkadandia sjui lilikuwa linaelekea kijiji gani wakat huo mama mwenye nyumba ananipigia Sm kuna migambo IPO kweny nyumba hapa inakuulizia ..
 
Ukamfukua ng'ombe mzima peke yako, ukamuosha peke yako, ukamchuna peke yako!Alikua na ukubwa wa kuku eeeh
 
Chunga sana ndugu ulaji wa mishikaji,huku kwetu kuna mzee alikuwa anauza mishikaji kwa 50/= amefungwa,kumbe alikuwa anachinja mmbwwaa!!
Bora mm nikajua kware
 
Nyama ya dogi hiyo [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nashangaa mpk leo 100,nakumbuka miaka 20 imepita siku nimetwanga nyagi usiku kucha siku ya pili nimeshinda ndani tu natema nyongo,best akaja kanikurupua kwenda hapo m,nyamala a ,ilikua 100,tukagonga ya kama 2000 hivi,pilipili na ndizi choma za kutosha.
Basi aaah pombe yote iliisha, tukarudi bar tena kula bapa.
 
Dogo, machinjioni Vingunguti kuna nyama inauzwa kwa mafuku hadi buku. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi na hiyo nyama, ni nyama poa kabisa na salama kwa matumizi ya binadamu.
Jamaa hajui, kuna nyama za kuokoteza zile vipande vinavyonyofoka wakati wa kuchuna na kukata kata.
 
aisee inawezekana nimeigongagonga sana ukiweka na ile pilipili yao ya kutengeneza ukirudi ni maji meengi"mmh
Tena unajikuta unachovyea kamshikaki kako kwenye pilipili huku unaandaa mate uuuwih 😄
 
Hivi ichi kipaji cha utunzi wa soga huwa mnazaliwa nacho au mnasomea?

..................................
 
Dogo, machinjioni Vingunguti kuna nyama inauzwa kwa mafuku hadi buku. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi na hiyo nyama, ni nyama poa kabisa na salama kwa matumizi ya binadamu.
Ni kweli wale jamaa hawanunui buchani..wanaenda machinjioni kabisa kule kuna kila aina ya nyama,mpaka za mafungu! Na ni nyama nzuri tu hazina shida..kumbuka mpaka ng'ombe anachinjwa bwana nyama/afya wanakua washajiridhisha..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…