Elections 2010 Misikiti nayo yaanzisha mkakati kuhusu uchaguzi mkuu ujao!



Kalagabaho wao wako kwenye Meremeta, Kiwira, Richmond n.k mabilioni ya JK ya nini tena! (joke)
 
Sasa hawa jamaa wametolewa msamaha ya kodi na serikali ilijua kuwa kuweke mwanzo na kuwarudishia na watasema kuwa na kutuunga mkono, ukweli ni kwamba ni watu wangapi au kama wanaamua kupiga kampeni waseme ni mtu gani anafaa na baadae sio wanakuja kumlaumu mtu ambaye ni chaguo la Mungu
 
Misikiti nayo iwafundishe waumini haki zao katika kupiga kura na si uhasama au kujitoa mhanga.
 
Halafu ikisemwa hapa kuwa Tanzania kuna udini (hivyo watu watibu ugonjwa huu badala ya kujaribu kuuficha) mimacho na mipovu inawatokaaaa..... Phewwwww

Miafrika bana ndivyo tulivyo
 
Kalagabaho wao wako kwenye Meremeta, Kiwira, Richmond n.k mabilioni ya JK ya nini tena! (joke)
Ha ha ha ha ha kweli nimecheka kuna ukweli kidogo lakini wao walifikiri vyeo vya nyumba kumi ,madiwani ni za waislamu

mimi naona isiangaliwe dini uangaliwe uwezo na elimu ya uraia na uzalendo
 
hakuna kitu hapo porojo tu, nchi yangu naifahamu vizuri kwa unafiki.
 
Mimi nilisema hata kama kanisa lina nia nzuri hili jambo la elimu ya siasa litatafsiriwa vibaya
 
Kuna viongozi wa kidini wanaotumika katika siasa hawa ndio maadui ,mahubiri yao hujihusisha sana na siasa wengine kufikia kusema kuwa fulani ni chaguo la Mungu ,sasa ukifikia kusema hivyo ni sawa na kuwaelekeza wafuasi wa dini wakumchagua.
 

Taabu ya Lusekelo ni elimu kiduchu mkuu!
 
Waongo wakubwa.
Wamefulia; maana watu wameshawabaini.
Kwani ile hoja ya dini ilikuwa inatafuta nini kwenye ilani yao ya chama?
Alafu kwa kujua wanachama wa chama chao hawasomi hata hiyo wanaita ilani walikuwa wanawatajia hizo ilani zingine lakini hii walikuwa hawaisemi labda kule kwenye nyumba ya sala. Nadhani na wao wako kati ya hivo viwili!
 
...
a)Kazi ya kutoa elimu ya uraia siyo ya Kanisa wala msikti ni Tume ya uchaguzi (serikali)
Nadhani utakuja kusema pia kwamba kazi ya kutoa huduma za afya na elimu ya sekondari na vyuo ni ya serikali tu!!
 

Mkuu hapo awali ulishasema kuwa tunahitaji kiongozi ambae atakubalika na wote bila kujali dini halafu unakuja kusema tusichague mkatoliki wala muislamu. Sasa hapo si umesha jicontradict? Halafu you go farther to say inabidi tuchague orthodox. Sasa where do you stand mkuu? Utasemaje watu wasichague viongozi on the basis of religion halafu unatutajia dini ambayo tunapaswa kuchagua mtu ambae ni muumini wake? Huwo sasa utakuwa unafiki mkuu.
 
Asma ya Kanisa Katoliki kuelimisha waumini kuhusu namna ya kuchagua viongozi bora imewaogopesha wengi. Kuna ubaya gani waumini wakielimishwa kuhusu namna ya:

1. Kuchagua kiongozi bora
2. Kukataa hongo na kuuza kura zao.
3. Kulinda kura zao zisiibiwe
4. Kutambua ahadi za uongo
5. Kujiandiksha kuwa mpiga kura.
6. Kupiga kura?

CCM imeogopeshwa sana na mkakatai huu wa Kanisa Katoliki kwani inategemea mno kuwarubuni wapiga kura. Haitaki wapiga kura walioelimishwa kuhusu haki zao.

Kama Waislamu wanataka kutoa elimu kwa wapiga kura hilo ni sawa vile vile.

Kanisa wala Waislamu hawaruhusiwi kumwambia mtu amchague nani. Lakini ni haki yao kuwafundisha Watanzania wawachague watu wa aina gani.
 
Hii concept ya ndg zetu waislamu kabla hata haija-mature mijitu tiyari mimacho imewatoka kwa chuki zao..Yaani hawataki hata kupata full story tayari wameshatoa hukumu!

Ukisoma muelekeo wa thread utagundua watu wengi humu wanakosa objectivity kwa kiwango cha kusikitisha. Nijuavyo JF ni ile cream ya waTz ambao wamefuta ujinga. Kujua kutumia PC na kutuma post ni dalili umepitia phases basic za kufuta ujinga..Sasa kama top cream can think this low, nadhani hali ni mbaya zaidi kule vijijini na majiani..

Mungu atunusuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…