Misingi, itikadi za dini na mabomu ya kujitoa mhanga

Misingi, itikadi za dini na mabomu ya kujitoa mhanga

Joined
Sep 17, 2016
Posts
72
Reaction score
22
Ugaidi wa kujitoa mhanga umekuwa janga kwa robo karne sasa. Shambuliz lakujitoa mhanga kwenye kambi ya U.S marine katika mji wa Beirut, ulimfanya raisi Ronald Rogan kuondoa jeshi lake la kulinda amani mjini Beirut.viongozi wa Palestina walitumia mashambulizi ya kujito mhanga ila kushinikiza makubaliano na Israel, na wapiganaji wa Iraq walitumia mabomu ya kujitoa mhanga kupinga utawala mpya wa kisiasa nchin mwao. Magaid wa Al-Qaeda walishambulia USS cole iliyoko Aden mnamo mwaka 2000, na 11 septemba 2001 kushambulia World Trading Center pamoja na Pentagon. Wakati baadhi ya wachambuzi wakiendelea kusema hakuna chembechembe za udini katika mashambulizi ya kujitoa mhanga, wakirejea kwa kikundi cha Sri Lanka, Tamil Tigers ambao sio waislamu, wanakua wanakosea. Waislamu wote wanaojitoa mhanga wanahalalisha matendo yao kupitia dini, na moja kwa moja kupitia dhana ya jihad.

Jihad ni nini haswa?
Ugaidi hujihalalishia ulipuaji wa kujito muhanga kupitia tafsiri ya jihad. Wakati wachambuzi wa kimagharibi wakisema jihad ni msingi wa mapambano ya nafsi (internal struggle), maandiko ya kiislamu yanahusisha jihad na vita ya kimwili (physical warfare). Mtaalam wa historia, Bernd Lewis katika kitabu chake cha Political Language of Islam amegundua kuwa '' idadi kubwa ya wanatheolojia, wanasheria na watu wa tamaduni walielewa jihad katika maana ya kijeshi''.

Falsafa ya sheria ya kiislamu imegawanya njia nne ambazo mwamini anaweza kupitia kutimiza wajibu wa jihad;
1) kwa kuamini ndani ya moyo
2) kwa kuhubiri na kuongoa kwa ulimi wake
3) kwa matendo mazuri kwa mikono yake
4) kwa kupambana na wasio amini au maadui kwa upanga.
Katika utendaji, njia tatu za mwanzo ni sehemu ya da'wa (matendo ya kimisionari), ila ni matendo ambayo utoa msaada (support) kwa jihad ya upanga (njia ya nne).

Wanatheolojia wa kiislamu wamekua wazi katika muunganiko wa jihad ya vurugu na ya amani katika kuueneza uislamu. Jihad ni kiini katika mtazamo wa waislamu kuhusu ulimwengu, wakiugawa mtazamo huo katika sehemu mbili; ''ldar al-islam'' (maskani ya uislamu) na ''dar al-harb'' (maskani ya vita) ambayo imehatimiwa kuwa chini ya utawala wa kiislamu. Jihad hutakatisha dar al-islam na pia ni zana ya kushusha na kutokomeza dar al-harb. Lakini katika mafundisho yake, dhima ya jihad iko wazi; kujenga utawala wa kiislam duniani na kulazimisha wasio waislamu kuukubali uislamu, au kukubali kukubaguliwa vinginevyo kutokomezwa kabisa. Uelewa kama huu ndio ulianzisha misingi mikuu ya itikadi za tawala mbalimbali zilizoongoza katika himaya za kiislamu kuanzia mwisho wa karne ya 7 mpaka zilipokuja kutokomezwa na himaya ya Mongol katika karne ya 13.

Ukilinganisha dhana ya martyrdom (ufia dini) upande mmoja katika uislamu na upande wa pili kwa ukristo, utaona ni kiasi gani falsafa ya sheria ya kiislamu ina shawishi zaidi katika jihadi ya vurugu. Katika uhalisia wa matendo, ndani ya uislamu, Martyr (mfia dini) ni yule anayekufa katika vita ya jihad. Mtu huyo siku ya hukumu anapewa nafasi maalumu paradiso. Katika ukristo mfia dini ni yule ambaye anavumilia mateso na kifo kuliko kuikana imani yake.



Nitaendelea.....
 
Mie nimependa hiyo definition Mpya ya ugaidi.

Mie awali nilijua ugaidi ni kuua Mtu Au kuhujumu mali bila ya Haki Kumbe ipo specific.
 
Jitahidi umalizie mada yako ila pia uwe tayari kujibu maswali kwa busara with reference kama ulivyotumia "Political Language of Islam"
 
Ukisikia Allah akbar sokoni we kimbia akuna kutafakari si dini si siasa we kimbiaaaaa[emoji23][emoji23]
Nimeipenda hiyo Idar-al-islam, ambayo ndiyo imezaa jina la Daresalaam.
Maana yake - maskani ya uislam.

Dola ya Kiislam haitofanikiwa kusimama, kama itataka kueneza Uislamu kwa nguvu.
Baadhi ya makundi ya Kigaidi kama ISS yanajipambanua wazi wazi kabisa katika kuonesha nia ya kueneza Uislamu kwa vita na kuwaua wasioamini.
Uislamu kama utaenezwa kwa Upendo na amani basi unaweza kujitanua na kuweza kujenga himaya au dola kubwa duniani katika kipindi kijacho.
Matendo ya Vurugu na Vita yanaleta matokeo hasi kwenye jamii iliyostaarabika na kuishia kudhoofisha imani husika.
 
Watu wasiokuwa na kazi ya kujishughulisha Mara nyingi ndo hukimbilia huko kwenye ugaidi ili mradi tu wasikose kazi ila hakuna cha maana chochote wanachofanya huko zaidi ya kudumaza fikra na kuamini vitu visivyokuwepo
Sio, Taasisi za kigaidi zinaajiri watu kama taasisi nyingine.
Tena utakuta taasisi kama za ISS zina mchanganyiko wa watu wenye imani tofauti kama za Kiislamu, Kikristo, Kibudha, Kihindu nk.
Ilimradi tu uwe mwenye kukubaliana na misimamo yao wanayoipigania.
 
Upo wrong mkuu,Jihad ipo ya (nafsi) ambayo ni kupambana na nafsi yako juu ya kutofanya mambo ya maasi.Pia ipo jihad ya vita(kital).
Nizungumzie jihad ya vita ambayo ndio msingi wa mada yako, hii jihad ikikuja miaka takriban 13 baada ya mtume kupewa utume,vita ya Badr ndo ilikuwa ya kwanza kupiganwa baina ya waislam na wasiokuwa waislam.Ndani ya miaka 13 waislam walitaabika kwa kuteswa na kuuliwa na makafiri wa Mecca ndipo ikipokuja ruhusa kuwa sasa waislam wajitetee kwa kupambana na adui yao.
Jihad haikuja kuwalazimisha watu kuwa waislam bali ilikuja kuutetea na kuulinda usilam,dini haienezwi kwa nguvu inaenezwa kwa hoja zisizo na mashaka.
Upanga au jihad ulikuja ku-defend uislam baada ya kuonewa sana na kwa kipindi kirefu.
Quran inasema ktk surat Albaqara kuwa hakuna kulazimishana ktk dini sasa ww umetoa wapi kwamba jihad ipo kulazimisha watu waingie ktk uislam?
 
Nimeipenda hiyo Idar-al-islam, ambayo ndiyo imezaa jina la Daresalaam.
Maana yake - maskani ya uislam.

Dola ya Kiislam haitofanikiwa kusimama, kama itataka kueneza Uislamu kwa nguvu.
Baadhi ya makundi ya Kigaidi kama ISS yanajipambanua wazi wazi kabisa katika kuonesha nia ya kueneza Uislamu kwa vita na kuwaua wasioamini.
Uislamu kama utaenezwa kwa Upendo na amani basi unaweza kujitanua na kuweza kujenga himaya au dola kubwa duniani katika kipindi kijacho.
Matendo ya Vurugu na Vita yanaleta matokeo hasi kwenye jamii iliyostaarabika na kuishia kudhoofisha imani husika.
Tatizo watu wanachagua pa kuamini na wanataka waelewe kama akili yao inavyojitaka ielewe. Hata ulete tani na tani za ushahidi kamwe hawatokuelewa. Kwa nini? Kwa sababu wameshajichagulia mahala pa kuamini na akili yao inataka ielewe kama inavyojitaka ielewe.

Uislam ni dini yenye misingi yake, nguzo zake na taratibu zake. Na kama unataka kuuhoji uislam basi uhoji kutokana na uislam wenyewe na wala si kwa kupitia muislam. Kwa sababu mfumo na anayeufuta mfumo ni njia moja ila wapita njia ni tofauti.

Uislam haujaimiza kujieneza kwa kutumia mapambano ya kumwaga damu au kwa njia yoyote ile ya vurugu. Kwa nini? Kwa sababu uislam wenyewe unasema " Laa ik' raha fii ddin" hakuna kulazimishana katika dini. Na hii ni aya katika suratul Baqarah. Nafahamu katika Qur'an zipo aya za vita. Swali la kujiuliza kwa nini zipo aya za vita. Ukitaka kulijua hili lazima urudi katika historia ya uislam kipindi cha Muhammad. Kwa nini? Kwa sababu Qur'an imeshuka kutokana na matukio na katika historia tunapata matukio husika.

Uislam haukuanzisha vita, isipokuwa wao walianzishiwa vita. Walinyimwa Uhuru wa kuabudu, walipokonywa Mali zao zote walizomiliki, walitengwa na jamii na wakawa wanauliwa kisa tu ni Muislam. Iliwalazimu mpaka kuhamia mji mwengine. Na licha ya hayo njiani wakawa wanawindwa kama wanyama na wakawa wanauliwa. Wakaanzisha makazi katika mji waliyoufikia nao ni Madinah. Wakafuatwa huko huko wakawa wanaendelea kufanyiwa dhulma. Na Maswahaba wakimuuliza mtume Muhammad s.a.w, mtume anawajibu kwa kuwaambia msiwadhuru waacheni lakini bado walikuwa ni wenye kuonewa. Na baada ya hapo ndipo zikashuka aya zinazoruhusu wapigane " wameruhusuwa kuzichapa wale wanaodhulumiwa; na mpambane nao mithili ya wao wanavyopambana na ninyi. Na wakaambiwa wasiwapige watoto, wanawake na wazee na wala wasiharibu vyanzo ambavyo vina manufaa kwa binadamu wote; Kwani Mungu hawapendi wanochupa mipaka".

Sasa fananisha wanayoyafanya Isis, al Qaeda, Boko haram na Alsha bbab. Tujiulize wanapigana kwa misingi ip?

Aya na hadithi za vita zimebaki ni ," Defensive " tu kama nchi zilivyojiwekea mipaka yake kwamba ukivuka tu mipaka yake basi umeingia kwenye vita na hiyo nchi, kadhalika na uislam vilevile. Sihofii watu kuja na tofauti na haya, kwa sababu wameshachagua mahala pa kuamini na akili yao inavyotaka ielewe kama inavyojitaka ielewe. Na hayo makundi yote ya kigaida yameondolewa na wanawazuoni wa kislam kwamba si waislam.
 
Sio, Taasisi za kigaidi zinaajiri watu kama taasisi nyingine.
Tena utakuta taasisi kama za ISS zina mchanganyiko wa watu wenye imani tofauti kama za Kiislamu, Kikristo, Kibudha, Kihindu nk.
Ilimradi tu uwe mwenye kukubaliana na misimamo yao wanayoipigania.
Vipi we unaona wanayoyapigania yana make sense?
 
Back
Top Bottom