Ukomo wake ni kuacha kuwadhulumu waislam maana waaislam wanatakiwa watete haki zao.
Hayo maslahi, ndio inabidi yawekwe hadharani ili jamii nzima iyajue na kuona kama ni ya kweli, na kama ni ya kweli basi yatatuliwe kijamii.
Utakuta baadhi ya vikundi vya kigaidi vinakiri wazi kuwa vinapigania maslahi ya waislam na wao ndio hasa wanaofuata misingi ya kiislam kuliko waislam wasioyapigania.
Kwa mfano hivi vikundi vinapowakuta Waislam na Wakristo na kuwatenga na kuwaua Wakristo na Kuwaacha Waislam, je hapo inamaana Sera yao ni kuwaangamiza Wakristo wote duniani ?
Mbona mimi ni Kristo na sijamdhurumu mwislamu yeyote na nina marafiki na ndugu wa Kiislam na tunaishi kwa upendo na amani muda wote.
Sasa Al- Shabab anaponiua mimi kwakuwa tu ni Mkristo kwani nimewahujumu nini ?
Iko hivi,
Baadhi ya Makundi ya Kiislam yanaiona nia yao nzuri ni ya kuifanya dunia yote iwe ya Kiislam.
Kikwazo chao kikubwa ni kuwepo kwa Ukristo ambao wanauona kama ni Ukafiri. Ndio maana inakuja nia ya kuuangamiza Ukristo na Wakristo, iwe kwa Amani au kwa Vita.
Mfano, ISS wakifanikiwa kuitawala dunia, watawasilimisha watu wote duniani kwa Lazima, atakaye kataa kusilimu ni wazi watamkatilia mbali.
ISS wako radhi kumuua Mwislamu mwenzao kama hakubaliani na matendo yao au lengo lao la kuuangamiza Ukristo duniani, huyo naye wanamwita Kafiri tu.
Hivyo basi Magaidi wanawachukia Waislamu wasiopenda vita ya kuwaangamiza Wakristo ili kuueneza Uislam na huwa nao wanawaua pia kama watakutana nao kwenye uwanja wa vita.
Kuna waislamu wengi wanaamini kuwa maslahi yao yanadhulumiwa sana na Mfumo Kristo, mojawapo ni huyo bwana niliye mnukuu.
Tatizo kubwa hawasemi ni maslahi gani ili kwa pamoja tujumuike kuyatatua.
Kama hayasemwi hadharani basi inawezekana kuna mambo mawili ya msingi.
La kwanza ni kuwa hayo maslahi ni siri yao na hayatakiwi kufahamika kwa mtu asiye Mwislam, maana yanalenga kuwapendelea Waislam na kuwanyima haki watu wa Imani nyingine.
Na pili hakuna cha maslahi wala nini, ila ni visingizio singizio tu vya kutaka kutimiza nia yao ya kuitawala dunia na kuangamiza watu wa imani nyingine. Tumejionea vita ya Rolinga na Wabudha, na ile ya Afrika ya kati iliyoibua kundi la Antibaraka ambazo zilileta madhara makubwa sana kwa jamii ya Kiislamu na jamii nyingine.
Kama kweli kuna maslahi ambayo jamii ya kiislamu inanyimwa hadi inafikia baadhi yao kuyaunga mkono makundi ya kigaidi, basi yawekwe hata hapa kwenye JF ili sisi sote tuyajadili kwa pamoja.
Dunia ni yetu sote na sisi sote tuna haki ya kuishi kwa furaha na amani.
Ukandamizaji wa aina yoyote au dhuruma na uangamizaji kwa visingizio singizio tu, katu havitakubaliki na havitashinda.