Tatizo watu wanachagua pa kuamini na wanataka waelewe kama akili yao inavyojitaka ielewe. Hata ulete tani na tani za ushahidi kamwe hawatokuelewa. Kwa nini? Kwa sababu wameshajichagulia mahala pa kuamini na akili yao inataka ielewe kama inavyojitaka ielewe.
Uislam ni dini yenye misingi yake, nguzo zake na taratibu zake. Na kama unataka kuuhoji uislam basi uhoji kutokana na uislam wenyewe na wala si kwa kupitia muislam. Kwa sababu mfumo na anayeufuta mfumo ni njia moja ila wapita njia ni tofauti.
Uislam haujaimiza kujieneza kwa kutumia mapambano ya kumwaga damu au kwa njia yoyote ile ya vurugu. Kwa nini? Kwa sababu uislam wenyewe unasema " Laa ik' raha fii ddin" hakuna kulazimishana katika dini. Na hii ni aya katika suratul Baqarah. Nafahamu katika Qur'an zipo aya za vita. Swali la kujiuliza kwa nini zipo aya za vita. Ukitaka kulijua hili lazima urudi katika historia ya uislam kipindi cha Muhammad. Kwa nini? Kwa sababu Qur'an imeshuka kutokana na matukio na katika historia tunapata matukio husika.
Uislam haukuanzisha vita, isipokuwa wao walianzishiwa vita. Walinyimwa Uhuru wa kuabudu, walipokonywa Mali zao zote walizomiliki, walitengwa na jamii na wakawa wanauliwa kisa tu ni Muislam. Iliwalazimu mpaka kuhamia mji mwengine. Na licha ya hayo njiani wakawa wanawindwa kama wanyama na wakawa wanauliwa. Wakaanzisha makazi katika mji waliyoufikia nao ni Madinah. Wakafuatwa huko huko wakawa wanaendelea kufanyiwa dhulma. Na Maswahaba wakimuuliza mtume Muhammad s.a.w, mtume anawajibu kwa kuwaambia msiwadhuru waacheni lakini bado walikuwa ni wenye kuonewa. Na baada ya hapo ndipo zikashuka aya zinazoruhusu wapigane " wameruhusuwa kuzichapa wale wanaodhulumiwa; na mpambane nao mithili ya wao wanavyopambana na ninyi. Na wakaambiwa wasiwapige watoto, wanawake na wazee na wala wasiharibu vyanzo ambavyo vina manufaa kwa binadamu wote; Kwani Mungu hawapendi wanochupa mipaka".
Sasa fananisha wanayoyafanya Isis, al Qaeda, Boko haram na Alsha bbab. Tujiulize wanapigana kwa misingi ip?
Aya na hadithi za vita zimebaki ni ," Defensive " tu kama nchi zilivyojiwekea mipaka yake kwamba ukivuka tu mipaka yake basi umeingia kwenye vita na hiyo nchi, kadhalika na uislam vilevile. Sihofii watu kuja na tofauti na haya, kwa sababu wameshachagua mahala pa kuamini na akili yao inavyotaka ielewe kama inavyojitaka ielewe. Na hayo makundi yote ya kigaida yameondolewa na wanawazuoni wa kislam kwamba si waislam.