Maslahi mojawapo ni yale ya Marekani kumiliki uchumi wa mafuta ya Iraq
Ukweli kwamba Iraq haikuwa na silaha za maangamizi kama ilivyodaiwa na Marekani na washirika wake.
Marekani umejuta, kwani, hadi sasa Marekani imeshindwa kuthibitisha hizo silaha za maangamizi za Iraq, hivyo kuonekana na dunia kuwa iliipiga Irak kwa kuitungia sababu za uongo tu.
Pia kuanguka kwa utawala wa Saadam Hussein ambako kumesababishwa na hila za Marekani, ndio chanzo cha machafuko mengi huko mashariki ya kati, na ndiko kuliko ibua vikundi vya kigaidi kama Islamic State (ISS)
ambavyo vimeleta uhalibifu mkubwa wa jamii na mali zao.
Machafuko haya yanaleta madhara makubwa katika dunia, hasa eneo la mashariki ya kati na kusababisha jamii za huko kusambaratika na kuzaa wakimbizi wasio na njia za kujipatia mahitaji muhimu ya kibinadamu.
Hadi hii leo mapigano yanaendelea na njia za kuyadhibiti bado haijapatikana.
Marekani ndio chanzo.