MISRI: Al Masry 0 - 0 Simba SC! Simba ametolewa katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika

MISRI: Al Masry 0 - 0 Simba SC! Simba ametolewa katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
IMG_20180317_205635.jpg
IMG_20180317_205629.jpg





Al Masry 0 - 0 Simba SC
(Agg: 2 - 2)

01': Mechi imeanza na Masry wamekuwa wa kwanza kufika katika lango la Simba. Manula yuko makini

03': Simba wanamuachia Mohammed kupiga kichwa akiwa peke yake, hakulenga

06': Kuna faulo karibu kabisa na lango la Simba, ni hatariDk 6 sasa, Simba wamerudi nyuma na wanalinda zaidi ya kushambulia

07': pira mkali wa faulo, Kapombe anaokoa kwa kichwa na sasa yuko chini pale, anaanza kutibiwa

08': Kapombe anatolewa nje kwa ajili ya kutibiwa zaidi

09': Kuna mchezaji wa Al Masry yuko chini, tatizo la nyama, MPIRA UMESIMAMA

11': Bado mchezaji yule hajatolewa na Manula amekuwa akimulikwa na mwanga wa kijani ili kumchanganya, hawa ni mashabiki

12': Mpira umeanza na yule mchezaji ametolewa
SUB: Anaingia Bance kuchukua nafasi ya Ahmed Gomaa aliyeumia

15': Okwi alimchambua beki na kutoa pasi kwa Kapombe lakini alikuwa amevutwa na kuangushwa

17': Krosi safi ndani ya lango la Simba lakini Simba wako makini, mpira ni goal kick

20': Manula analala chini pale inaonekana aliumia wakati aliporuka kuokoa

21': Bocco anaingiza krosi safi kabisa lakini Okwi anachelewa na mpira unakuwa goal kick

23': Mpira umesimama, Gyan amegongana na Hamty wa Al Masry na wote wanatibiwa

25': Hatari kwenye lango la Simba lakini Manula anaruka na kudaka mbele ya Bance

26': Manula anafanya kazi ya ziada kudaka mpira mbele ya Mustapha, ilikuwa krosi hatari ndani ya lango la Simba

27': Okwi anawekwa chini hapa na mpira unapigwa kwenda Masry

28': Kipa wa Masry anaruka juu na kuudaka mpira kama nyani baada ya krosi ya Gyan

29':Bance anakwenda vizuri lakini Mkude anamuwahi na kuchukua mpira

30': Masry wanapata kona ya kwanza, inachongwa hatariiii, goal kick

34': Bado Masry wanapata kona baada ya krosi hatari kabisa

35': Kona inachongwa Kwasi anaruka na kuokoa, kona tena inachongwa Simba wanaokoa

36': Bance anawachomoka Simba, anaachia mkwaju mkali hapa, Manula anadaka kwa ustadi

39': Mlipili analazimika kumlza chini Salam katika eneo hatari baada ya Gyan kupoteza mpira

41': Kuna vurugu zinaendelea na wachezaji wanafukuzana na kurushiana mikono mpira umezimama

43': Kuna faulo karibu kabisa na Simba baada Kotei kugongana na Gomaa wakati wakiwania mpira

44': Nyoni analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Glindo

45': Dakika 3 za Nyongeza nimeonyeshwa

MPIRA MAPUMZIKO (AL MASRY 0 - 0 SIMBA)

Timu zimerudi uwanjani

45': Kipindi cha pili kinaanza hapa

48': Masry wanapata faulo karibu kabisa na lango la Simba, si eneo salama

49': Manula anaruka na kuokoa, ilikuwa hatari kabisa

51': sasa, Masry wanaonekana kuwa na kasi lakini bado Simba wanalinda zaidi
Manula anafanya kazi ya ziada kuruka na kuokoa mpira juu ya kichwa cha Mustapha

53': Mkude anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumuangusha Mohammed

54': Inachongwa faulo, Gyan anaokoa na kuwa kona ya kwanza kipindi cha pili

55': Hatari kwenye lango la Simba, Manula anagongwa lakini mwamuzi hakuona huenda, mpira unapigwa lango la Simba likiwa tupu, goal kick

56': Gyan anaachia mkwaju mkali kabisa, unatoka pembeni kidogo ya lango la Masry, ilikuwa hatari

59: Mohammed wa Masry anajiangusha na mwamuzi anasema faulo
Hatari kwenye lango la Simba, mpira unatoka pembeni kidogo

61': Kwasi anajaribu mkwaju, goal kick

63': Manula anagonjwa wakati akijaribu kuokoa na sasa yuko chini na mchezaji mmoja wa Masry yuko chini pia

SUB. 66': Simba wanafanya mabadiliko, anaingia Mavugo kuchukua nafasi ya Mlipili

67': Okwi anawekwa chini, mwamuzi anasema twende, sijaona
Kotei naye anafanyiwa madhambi, mwamuzi anasema sijaona twende. Wachezaji wa Simba wanaonekana kukasirishwa wanamfuata mwamuzi na yeye anamuita Okwi na kumuonya asiendele kumlaumu. Kotei bado anatibiwa

68': Sasa, Gyan naye yuko chini pale akitibiwa huku mashabiki wa Masri wakiendelea kuzomea

69': Okwi anaingia vizuri na kuachia mkwaju mzuri hapa, mabeki wa masry wanaondosha hatari

71': Simba wanaonekana kuanza kufunguka na kushambulia

72': Kotei anafanya kazi ya ziada kumzia bance na mpira unakuwa wa kurushwa

SUB! 73': Simba wanamtoa Kotei na nafasi yake inachukuliwa na Shiza Kichuya

75': Simba wanaonekana kuanza kufunguka, wanashambulia na Gyan anaachia mkwaju mkali hapa lakini goal kick

78': Mkude anaachia mkwaju mkali hapa lakini hakulenga

79': Mavugo ndani ya 18, anaachia mkwaju mkali lakini kipa anaonyesha ujuzi mkubwa anadaka ilikuwa nafasi nzuri zaidi kwa Simba katika mchezo huu

80': Bocco anaruka vizuri hapa lakini kipa anaokoa hapa
KADI: Juuko analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Gomaa ambaye bado yuko cchini pale

81': Bance anapiga kichwa hapa na Manula anadaka vizuri

85': Yusuf Otara anaingia kuchukua nafasi ya Islam Issa

87': Wachezaji wa Al Masry wanajilaza chini ila mara kwa sasa. Inaonekana ni jaja yao ya kupoteza muda
KADI: Bocco anapewa kadi ya njano

88': Okwi anaaachia mkwaju unawababatiza mabeki na kuokolewa

90': OKwi anajaribu kuingia anazuiwDk 89 kipa kajilaza pale kupoteza muda
Dakika 5 zimeongezwa kwenye mchezo hii

MPIRA UMEKWISHA: Al Masry 0 - 0 Simba SC
 
Aishi kaumia kweli au anazuga kupunguza mashambulizi?
 
AZAM SPORT2 WAMEAMUA KUTANGAZA BADALA YAKUONYESHA
 
Back
Top Bottom