Misri (Egypt) most powerful country in Africa Tanzania we are 17

Kama walivyosema wadau wengi, hizo ranking ni mbinu Za kuuza bidhaa zao na vifaa vya kijeshi. Kwani ukiwekwa wa kwanza au mwisho Kuna faida gani?
 
Mbona mwaka jana tulinunua magar yakivita na tukayatawanya kila kituo kuzuia nguvu ya Edo.
 
Eti Uganda wametupita? Na zambia na zimbabwe? Congo vikundi vya waasi tu vinawazingua, duuu ila hizi ranking

Kuna vigezo vingi vinavyoangaliwa, huku bajeti (bajeti ya jeshi) ikichukua nafasi muhimu
 
Duu, nilidhani Tanzania iko vizuri sana
 
Eti Uganda wametupita? Na zambia na zimbabwe? Congo vikundi vya waasi tu vinawazingua, duuu ila hizi ranking
Wenzetu wanapigana kila kukicha ndo maana kuna reference ktk ranking..Sisi hata hivyo vikundi vya waasi hatujavijaribu...!!.. Hili nalo halihitaji Propaganda babu, Tuache mambo ya kujisifu wenyewe
 
fafanua namba 10 na namba 27 sijajua tofauti
 
Huu upuuzi bado mnauamini, mfano mwaka jana Tanzania ilikuwa ya 24, leo ghafla imepanda 17, kuzipita Ghana n.k,
Vigezo wanavyotumia ni idadi ya silaha, idadi ya wapiganaji (active personnel), n.k swali rahisi tu je, neshi la Congo linaweledi kiasi gani mpaka kupewa chapuo vile kama tunavyoshuhudia kwao, pia ni moja ya majeshi yasiyo na nidhamu ndio maana uasi ni mwingi sana.

Kuwa na silaha nyingi bila weledi wa maaskari ni sawa na bure, mfano Kenya wana silaha nyingi sana kwa mjibu wa hizo ranking of military lakini mafanikio yao yako wapi? Pia Nigeria
 
fafanua namba 10 na namba 27 sijajua tofauti
Namba 10 ni jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo (DRC) au Kongo kinshasa chini ya Joseph kabila na namba 27 ni Kongo Brazzaville ambayo rais wake ni Don sasu ngwaso. Ni nchi mbili tofauti ila zimepakana. Miji yao mkuu yaani kinshasa na Brazzaville imetenganishwa na mto Kongo.
 
Sipendi silaha wala vita....Baada ya Vita....
Hakuna mshindi....bali nani kapona....
.....Na mwisho wa siku hata waliobaki watakufa tu...muda ukifika.....
 
Zambia,Zimbabwe,Uganda na Kenya?ni upuuzi kufikiria kirahisi kwenye karne hii
 
Mungu ibariki Tanzania,Mungu libariki jeshi letu tukufu Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
 
Huu ni uongo, kwa vigezo gani hadi s. Sudan kuwa na rank nzuri hivi!
 
 
Uongo mtupu,wanaosemwa kutupita ndio huomba msaada kwetu,misri ndio wanatupita but the rest wapo nyuma yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…