ameshakwambia hata wewe cha kufanya miaka mingi tu. hata tz alishasema kama tunataka maji mbona tunaweza kuchimba visima tukapata underground, kutumia maji ya victoria tunafanya mto nile upungue na yeye anautumia kule kwao. kuna mikoa mingi tu inazunguka ziwa hawana maji hadi leo, hata Mara kuna vijiji havina maji, ila ziwa lipo pale. kutoa maji toka mwanza kuja Dodoma ni kwa mbinde, Misri hataki. ajabu yake, sisi ndio tunapanda miti inaleta mvua ziwa linaendelea kujaa, the same applies to Ethiopia, tukiamua kuacha kutunza mazingira ni kwamba NIle itakauka automatikally, au hata tukiamua kuyachafua wataenda kule watakula uchafu na sumu tu. kwa ethiopia hatakiwi kuleta kibesi kwasababu hata hamisha mto ule toka ethiopia hata baada ya kuwapiga, bado mto utaendelea kuwa nchini ethiopia na waethiopia wakiamua kutia sumu waarabu wafe wanaweza. asione yeye ndio mbabe wa kuonea wengine.
though on the other hand, NIle kwa Misri imekuwepo karne, uchumi wake mkubwa sana umejijenga kwenye mto huo, hivyo kupungua kwa maji kutakata mapato makubwa na nchi itatikisika sana kwasababu ilishajiimarishia humo, hapo cha muhimu ni kwenda kwa mazungumzo na maelewano, na kama ikiwezekana basi misri waangalie kama watagharimia vitu ambavyo ethiopia au hata sisi tutapata nje ya maji ya mto. angewajengea mfumo mwingine wa kupata umeme ethiopia tena kwa kutumia pesa zao zinazotokana na mto nile kule kwao kama mbadala wa Ethiopia kutumia maji. hapo wangeeleweka. ila kuzuia kwamba kwasababu yeye ndio alijijenga kwenye mto tangu zamani hivyo wengine wasitumie wakati maji yanatoka nchini kwao, haitakuja kukubalika.