Misri na Jordan ndio walinzi wa Israel ili isifutike

Kabla ya hapo Palestina ilikuwa ikitawaliwa na watawala tofauti tofauti na si lazima waitwe wafalme au maraisi.Mara ya mwisho ilikuwa ni sehemu ya utawala wa kiislamu wa Ottoman ambao ulianzia nchi za kiarabu mpaka Ulaya na Asia.
Nadhani point ya muuliza swali anataka umtajie majina ya watawala wa Palestine kabla ya mwaka 1947; mfano Israel unaweza kuwataja wafalme wao kama kina Joshua, Samuel, Sauli, Daudi, Suleiman nk, sasa je tunayajua majina ya watawala/wafalme wa Kipalestine walau 5 kabla ya mwaka 1947? Nipo interested kujua hata mimi brother.
 
Kuigawaje palestina Tena hakukua na nchi inayoitwa palestina Bali kulikua na jamii za warabu na waisrael

Kama kulikua na taifa la palestina ntajie wafalme angalau watano wa palestina waliotawala kabla ya 1947
Sielewi kwa nini unasisitiza kwenye nchi, hii jamii ilikuwepo tokea muda mrefu ni ilitawaliwa na dola mbalimbali kwa vipindi tofauti. Hata kama haikuwa nchi, bado ilikuwa na utaratibu wake wa uongozi.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Unalazimisha kosa jomba. Mwaka 1947 Palestine ilikuwa bado chini ya Uingereza. Alipouliza kabla ya 1947 maana yake ni kabla ya utawala wa uingereza, huwezi kujibu Uingereza wakati uingereza bado anatawala wakati huo.
 
Ntajie hawa viongozi, taifa lolote ambalo hakikukua na kiongozi ni halikuwepo, hata makabila yetu yalikua na machief na walijulikana na kulikua na Koo za kichief

Ukweli ni kwamba hakukua na nchi inayoitwa palestina kabla ya 1947, ndo maana hata yesse arafat rais wa palestina alizaliwa misri na ndo point wanayotumia wayahudi
 
Unalazimisha kosa jomba. Mwaka 1947 Palestine ilikuwa bado chini ya Uingereza. Alipouliza kabla ya 1947 maana yake ni kabla ya utawala wa uingereza, huwezi kujibu Uingereza wakati uingereza bado anatawala wakati huo.
Jibu ni kwamba hakukua na taifa la palestina kabla ya 1947 na hakukua na mfalme aliyetawala palestina na ukweli ni kwamba Hana majibu
 
Umeshusha kitu kweli kweli
 
kwa mujibu wako wa Israeli halisi ni wapi? Make umesha sema hao waliopo hapo ni walowezi wa kizungu, inamaana wapo wa Israeli org.
Hao org ni wapi kwa mujibu wako?
Shimon Peres rais na wazir mkuu wa Israel alizaliwa mwaka 1923 na hapo ni kabla ya mwaka 1947 mtu atasemaje hawakuwepo
 
Jibu ni kwamba hakukua na taifa la palestina kabla ya 1947 na hakukua na mfalme aliyetawala palestina na ukweli ni kwamba Hana majibu
Taifa la Palestine limeaanza hata kabla ya ukoloni wa Uingereza, punguza kula ugali mbichi.
 
Anayesema kuwa wapalestina hawajawahi kuwa na serikali yao kwa hiyo hawastahili kuwa nchi ni upuuzi.
Huwezi kuwapangia watu wa nchi husika lini wawe na self determination. Wao kama walikuwa chini ya ukoloni kwa mamia au hata maelfu ya miaka, Sasa wanataka kuwa na serikali yao na nchi yao!

By the way, lile eneo lote kabla ya 1948 officially liliitwa PALESTINE, japolilikuwa chini ya Muingereza na kabla ya hapo ottonans hivyo ndivyo documents zote za kiserikali zilivyokuwa zikiita hiyo nchi.

Kwa hiyo Jews na Arabs waliokuwa wakiishi eneo hilo wote walikuwa wakijulikana kama Wapalestina.

Baada ya kuanzishwa kwa Taifa la Israel siku hizi waarabu peke yao ndo wanaitwa Wapalestina au Israeli-Arabs(kwa wale waliobaki ndani ya Israel), Ila Wayahudi wao wanaitwa Israelis.
 
Nitajie Raisi wa Tanzania 1950 ni Nani? Ushaambiwa kulikuwa na Ottoman baadae Muingereza means na wao kama tulivyokuwa Sisi walikuwa wa kutafuta Uhuru wao.

1500 mpaka 1900 walitawaliwa na Ottoman, baada ya Vita vya Dunia mpaka miaka ya 1940s walitawaliwa na British, kuanzia hapo mpaka leo kuna waisrael.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…