Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uko sahihi kabisa, juzi kati waliwatengenezea parade majeneza yenye maiti za mafarao wao, mummies, leo hichi ni kuongezea kuvutia watalii, niliona wanalalamika utalii umeshuka 90%. Si ajabu hata kunasa kwa lile meli kubwa, walihusika ili kupata attention ya dunia. Desperate times calls for desperate measures.Propaganda ya kutibu ukame wa watalii uliosababishws na covid19
mji ulikuwa mavumbini, ni kama makaburi ya wafalme tu, mpaka sasa mengine hawajayagundua licha ya kwamba yana ukubwa hata wa ghorofa tatu ila yamefichwa na mchangaYaani unagunduaje mji mfano. Kwamba mlikua mkipita hamuuoni au? Archeologists mnafeli wapi?
[emoji23][emoji23][emoji23]ukuta mbona ni tope Kama nyumba za wasukuma watani zangu [emoji23][emoji23]zile za hovyo hovyo Sana [emoji23][emoji23][emoji23]nimecheka kinomaWataalamu wa historia ya nchini Misri wamefanya ugunduzi wa kushangaza wa mji ambao ulikuwepo zaidi ya miaka 3,400 wakati wa muda wa farao.
![]()
Uzinduzi huo umetajwa kuwa muhimu tangu kugunduliwa kwa kaburi la kale la Tutankhamun.
Wana akiolojia hao ambao walikuwa wakitafuta hekalu katika eneo la jangwa karibu na mji wa Luxor. Lakini wakaanza kugundua jambo lingine, ukuta wa nyumba ambazo zilionekana kila upande.
Kulikuwa na vyumba vilivyokuwa na vitu ambavyo Wamisri wa kale walikuwa wakitumia kila siku katika maisha yao.
Pete na vyungu vilivyochorwa kwa rangi na kugongewa muhuri wa farao aliyekuwa na nguvu kubwa nchini humo .
Kulikuwa na duka la kuuza mikate katika eneo la jirani ambapo ushahidi wa maandalizi ya chakula cha watu wengi yalionekana.
Sehemu nyingine kulikuwa na ishara ya shughuli za kiwanda.
Inaonekana kuwa wakazi wa eneo hilo walikuwa wanajishughulisha kutengeneza mapambo ya maeneo ya kuzikia na hekaluni.
Uzinduzi huo ulikuwa na taarifa nyingi hata kuhusu majibu ya kwanini eneo hilo lilitelekezwa na watu wake.
Ugunduzi huu ni jambo muhimu sana katika historia ya Misri na wataalamu wake wa akiolojia.
Mji huu uliohifadhiwa vizuri umeelezewa kuwa kumbukumbu ya historia ya Misri.
View attachment 1748294
Propaganda ya kutibu ukame wa watalii uliosababishws na covid19
Mkuu,umeshashua uzi?powa mkuu nitaandika kesho niweke na videos