Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Waziri wa mambo ya nje wa Misri amesema vikwazo vya Israel ikiwwemo upekuzi ndicho kinachopelekea kutokuingia misaada Gaza kama inavyotakiwa. kupitia kituo cha Rafah
Katika malalamiko yake amesema malori lazima yapekuliwe katika kituo kinachoitwa Israel Nitzana ambacho kiko ndani ya Misri.Baada ya hapo malori hayo huchukua safari ya kilomita 100 ndipo yafike kituo cha Rafah ambako tena kuna askari wa Israel upande wa pili.
Imeelezwa kituo hicho cha Rafah wala hakikupakana na Israel bali kimepakana na Gaza.
Kabla ya vita kituo hicho cha Rafah hupita malori 500 kwa siku ya mahitaji mbali mbali ya Gaza,Kwa sasa ni malori baina ya 10 na 20 tu yanayopita kwa siku.