Misri yawasilisha malalamiko rasmi FIFA kupinga uamuzi wa waamuzi dhidi ya Argentina

Misri yawasilisha malalamiko rasmi FIFA kupinga uamuzi wa waamuzi dhidi ya Argentina

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Shirikisho la Soka la Misri limewasilisha rasmi malalamiko likitaka kufanyika kwa uchunguzi kuhusu maamuzi ya waamuzi katika mchezo wao wa Kombe la Dunia dhidi ya Argentina uliomalizika kwa kipigo kwa Misri.

Rais wa Shirikisho hilo, Hany Abo Rida, ameamua kupinga uamuzi wa mwamuzi wa Ufaransa François Letexier pamoja na wasaidizi wake, akitaka timu hiyo ya waamuzi wa Ufaransa iondolewe kwenye mechi zitakazofuata za mashindano hayo kutokana na makosa makubwa waliyodai kufanyika.

Soma: Mourinho: Mechi ya Misri na Argentina ilikuwa filamu

Kwa mujibu wa ripoti ya Win Win All Sports, Shirikisho la Misri linaamini kuwa makosa hayo ya uamuzi yalikuwa na mchango mkubwa katika matokeo ya mchezo huo.
 
Subiri nyumbu wa goti wa kuvundika waje kuujaza huu uzi kwa komenti ndefu ndefu.
 
Ukijitambulisha kutokea Afrika ili ufaulu duniani lazima uonyeshe kiwango mara mbili ya kawaida.

Sasa ukiwa wa kawaida au ukawazidi kidogo tena bila consistency kitakupata cha Misri.
Ukilalamika wazungu wanafurahi wanaona dawa haijaingia.

Walitakiwa waongeze magori yafike manne iishe nne tatu. Dunia haiko fair hasa ukiwa kwenye eneo la kupoteza kama Afrika. Utagombana na watu bure.
 
Malalamiko yao yatakuwa dumped tu kama Algeria.

FB_IMG_1783451376352.jpg
 
Why argentina ndyo walalamikiwe tu.kuna nn kwa argentina?
 
World Cup ya mwaka huu imepoteza mvuto sana. World Cup iliyofanyika Urusi mwaka 2018 ilifanikiwa sana kuliko hii ambayo rais wa nchi anajiingiza kuwa refarii, au serikali inazuia mashabiki na baadhi wa waamuzi wasihudhurie. Kibaya zaidi FIFA nayo imekubali yote hayo
 
Unaongoza 2 kwa 0 bado dakika 11 mpira uishe unataka kulalamika nini?
 
Huyu rais wa FIFA Gianni Infantino hata haeleweki. Ni kama vile anapelekwa pelekwa tu hovyo na watu wenye nguvu duniani. Bora hata Sepp Blater alikuwa ana misimamo yake binafsi.
 
Wanajifurahisha tu ila mioyoni ukweli wanaujua, refa alikiwa fair. Unashindwa kushikilia bomba goli mbili? Ila si shangai ndio tatizo ya timu za Africa,England wapo pungufu kuanzia dk 54,wanaongoza 3-1 na Mexico, wakashikilia bomba mpaka dk 90 wakashinda ,tena timu walio cheza nayo ilikuwa inacheza mpira wa kasi. Unaongoza mbili bado dk kumi na mbili zinachomolewa zote mbili na kuongezwa la tatu.

Uzuri review zipo Lisandro kakanyagwa ukirudi kwa Salah, Julian aliamza kuucheza mpira unakatoka kwenye miliki ya Salah hamna faulo,wanajisumbua tu ila wakafanye homework jinsi ya kumaliza mechi dk za mwisho.
 
Back
Top Bottom