*Miss Tanzania 2008*

2nd runner-pendo(#13),
1st runner-sylvia mashuda(#14)
winner is...#22....
 
...eh! haaya, yote kheri, ...mashaallah
 
Jamani,

Vipi mnamuonaje huyu? ataleta taji kweli au itakua ni kama kawaida tu kwa Tanzania kila inaposhiriki kwenye mashindano ya kimataifa (Mpira, miss world, Olympics etc) kushiriki na kushindwa?
 
Jamani pamoja na Nasreem kushinda taji tukubali kuna wazuri waliomzidi sana. kwa mtazamo wangu hii ndio list yangu by Outlook 1. Rona Swai 2.Tusikile Mwaki 3. Pendo 4. Nasreem 5.Flora 6. Florence 7.Lilian 8. Miriam 9. Nadya 10 Devota 11 Slyvia. Wasiokuwa na Mvuto sana Angela annet Elizabeth Johari tadya Doris Cessilia. waliosalia wapo wapo tu.
 
Nimefurahi kuwa top mshindi na yule wa tatu wametoka katika list yangu. Yule mshindi wa pili pia alikuwa karibu sana na macho yangu kwenye list ingawa sikumpa nafasi kubwa sana nikilinganisha na wale niliokuwa nimewatanaguliza. Hali ndivyo ilivyo, macho yangu huona kwa kutumia ultra violet light, hivyo naweza kutofautiana na wengi.

Kilichonisikitasha kwa sasa ni taarifa nilizosoma baadaye kutoka vyanzo mbali mbali kuhusu tabia za huyu Miss Tanzania wetu wa mwaka huu. Sina uhakika na taarifa hizo lakini kama taarifa hizo ni za kweli, basi zinanifanya nifikirie mara kumi umuhimu wa kuendela na mashinado ya namna hii bila kuwa na standard thabiti. Najua kuwa washindi wa mashindanio haya huwa wanapata exposure ya kimataifa ambayo pia huwawezeasha kupata mikataba ya kimataifa na hivyo kujiendeleza kiuchumi wao binafsi na familia zao na taifa zima kwa jumla. Jambo linalotia wasiwasi ni kuwa washindi wa mashindano haya wanagubikwa na rekodi mbaya (kulingana na taarifa za pembeni kama ni za kweli) wanaweza kuweka mfano mbaya kwa watoto wa kike wanaotafuta namna ya kukwamuka na ufukara wakizania kuwa njia moja ya mafaninkio ni kuendeleza tabia mbaya za namna hiyo.
 


Haya mashindano yote kwa ujumla wake ni non starter kwa watoto wa kike wa kizazi kijavyo. Ukiachana na mambo mengine, yanatoa picha kwamba maisha sio magumu vile, ni swala kuwa mrembo na kujiremba, unajipitisha mbele dakika kadhaa, unaibuka na gari, ebo-very artifical sort of life! Sasa hii ndio inafanya watoto wa kike waache kuchangmkia Physiscs!
 

Mkuu!
Picha ndo hazikuwatoa vizuri au hawako photogenic maana kwa kuwaona "live" they all look beautiful.... tuwape sifa zao jamani.Niliwashuhudia walivyowarembo ndio maana nawafagilia tena sana!
 
Kuna vigezo vingi vinavyotumika kumchagua mtu, uzuri na mvuto huwa vinachangia tu. After all Mzuri kwako mara nyingi anakuwa si mzuri kwa mwingine. Hata hivyo tunawapongeza maana hatukutegemea kumpata mtu kutoka kanda ya ziwa.
 

..hizo tabia ndio zinawapa ushindi, si ndo maana wote huwa ka watoto wa mama/baba mmoja!
 
Kuna vigezo vingi vinavyotumika kumchagua mtu, uzuri na mvuto huwa vinachangia tu. After all Mzuri kwako mara nyingi anakuwa si mzuri kwa mwingine. Hata hivyo tunawapongeza maana hatukutegemea kumpata mtu kutoka kanda ya ziwa.

..na uzuri mwingine hauonekani kwa macho, au sio?
 
Jamani,

Vipi mnamuonaje huyu? ataleta taji kweli au itakua ni kama kawaida tu kwa Tanzania kila inaposhiriki kwenye mashindano ya kimataifa (Mpira, miss world, Olympics etc) kushiriki na kushindwa?

...Ila aminia tukipeleka wacheza ngoma ktk mashindano ya dunia tutachukua medali zote mhimu.....lol
 
Nadhani matangazo teyari kwa sasa tungoje mchakato mzima wa utendaji. Magazeti ya Udaku sasa ndio yanakuja na suala zima la kuuza. Katika Race ya Mamiss kuandikwa vibaya na magazeti ya Udaku mimi nangoja tu kujua ni nani atakuwa wa kwanza kuwa katika SPotlight!

Hongera kwa Washindi.
 
je mvuto ni kipaji? kwa kiingereza kipaji tunachozungumzia hapa kinaitwaje?
 
Mshindi ndo huyo kapatikana bado sijasikia malalamiko ya watu kama kawaida yetu. naona wengi wamemkubali.
Nawashauri mamiss kama lugha ya Kiingereza haipandi vizuri bi bora kuongea kiswahili tu.

Jana nilikuwa naangalia taarifa ya habari kupitia luninga zetu, karibu vituo vyote vimetuonyesha jinsi mshindi alivyopatikana isipokuwa ITV tu ndo hawakuonyesha sielewi ni kwa nini wamefanya hivyo. au ni kwa sababu tender ya kurusha matangazo ya moja kwa moja walipewa TBC1? ITV wakumbuke haya mashindano ni Miss Tanzania na wala sio Miss TBC1
 
je mvuto ni kipaji? kwa kiingereza kipaji tunachozungumzia hapa kinaitwaje?

...haika, Kwa uelewa wangu mdogo, mvuto ni attractive, attractiveness, katika fani hii wao wanaita 'photogenic', Kipaji ni talent, talented.

au?...
 
dah uwongo mbaya baadhi ya akina dada hapa hawana mvuto sio siri wala nini kupata kura itakua ngumu sana kwao....kura yangu naona Florence anaweza nishawishi nikajiunga na Zain!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…