Miss Tanzania 2014 live Star TV

Kingereza chenyewe cha kukariri.. ovyoooo wala haikuonyesha umahiri wowote kwa warembo hao. mwingine kajidai Kifaransa wala hajaulizwa! Warembo wote hawajaonyesha umahiri wowote kwa kutaka kuonyesha wanajua lugha ya Kingereza wakati wangeweza kuonyesha ujuzi wa mambo na umahiri wao katika lugha ya taifa na waliyoizoea. ngoja huko miss world tuone wakipeleka madudu.
 
Ushindi wa sitti mtemvu nimeufurahia sana. ..wale mapedeshee wanaotishia vitoto vya watu kwa mandinga kuwahonga hapa kwa sitti wabadili mbinu kwani mtoto hata hajashiriki haya mashindano anacruise ndinga za maana. ..nilibahatika kuwaona hawa mamiss before leo huyu sitti alikuwa ana confidence sana na kwa talent ya kudance nyoko. ..anakatika balaa
 
Hivi kwani lazima watumie Lugha za kigeni?

Ushamba unawasumbua kwani wao wanafikiri ukiongea Ung'eng'e ni Ujanja hata kwa kukariri bado wanajiona ni wana-England wazaliwa Ulaya, huu ujinga wa kudhani English ni bora kuliko Kiswahili unafaa ukemewe kwa nguvu Zote na Waziri wa Utamaduni sanjari na Waziri wa Elimu.
 

Huenda Kalipiwa Deni kwa Masharti Kuwa lazima Binti awe Miss Tz kwa mbinu yeyote ile, huu kwa kweli ni Uchakachuaji wa hatari ni Kama wa Sita kule kwenye Bunge la katiba . Nchi hii kuna masiara kila kukicha !
 
Mimi mashindano yoyote siwez kabisa ntapata presha bure ya kukosa zawadi
ha ha ha ha ha ha ha ha, hiini kali sasa. unahitaji cancelling tu, na ukishiriki hata mara moja unazoea, kila kitu kinaanza kidogo na uoga lazima uwe nao
 
Hakyanani kabisa wamechakachua, inawezekana kuna mzee pale alipewa ahadi siyo bure

Waandaaji walikuwa na Vimeo vyao huenda wajanja wamejipenyeza kwenye kuvisawazisha kisha Malipo ni kumpa Umiss Tz Kama shukurani.
 
Hii ndiyo Tanzania hakuna lisilowezekana, watu wakiamua kukuletea Yao hata ufanyeje wataleta tu, jawabu mtalipata miss Dunia kwani pale Uchakachuaji haupenyi kirahisi Kama Bongo.
 
Mfyuuuuuuu yani leo wameniuz inabid nisonye tuuu
 
Hii nchi in a matahira wengi,sasa unaambiwa uchague lugha mbili we unaongeza ya tatu......Hizo dharau sasa!!!
 
Kweli wamefulia, yani leo Miss Tanzania halafu watu wengine wala hatuna habari...wakati kipindi kile ilikuwa hatumwi mtu dukani...

Bora hata nilivyolala tu...
 
Hii nchi in a matahira wengi,sasa unaambiwa uchague lugha mbili we unaongeza ya tatu......Hizo dharau sasa!!!

Ha ha ndo mana Tanzania majority ya watanzania wana iq ndogo hapo kama ni mtihani si kashafeli ndo nashangaa eti mshindi kingereza na kifaransa kwani yale yalikua mashindano ya lugha
 
Nikiripoti kutoka insta
 

Attachments

  • 1413071736831.jpg
    65.6 KB · Views: 1,465

Tanzania haina tabia ya kufanya vizuri, bora liende, bora tulishiriki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…