Miss Tanzania 2014 live Star TV

Miss Tanzania 2014 live Star TV

Kati ya washiriki 30 wa Redds Miss Tanzania..Sitty Mtemvu ndiye aliyenyakuwa taji hilo akitokea wilaya ya Temeke.

Ushindi huo unampatia zawadi ya sh 18 Milioni.

Wakiwa Jukwaani wakati wa shindano hilo la Redds Miss Tanzania 2014 hakuna hata mshiriki mmoja kati ya watano waliofanikiwa kuingia kwenye tano bora aliyejibu swali kwa lugha ya Kiswahili..wote walitumia lugha ya Kingereza na mshiriki mmoja kutumia lugha mbili ya Kingereza na Kifaransa

Wanaharakati mbalimbali nchin wanafanya juhudi za kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya bara la Afrika cha ajabu sisi wenyewe Watz tumekuwa tukikionea aibu Kiswahili kukizunguza ktk majukwaa mbalimbali kama Miss Tz.

My take.

Jamani Tanganyika tuikatae,hata Kiswahili pia tukikatae?
Kingereza chenyewe cha kukariri.. ovyoooo wala haikuonyesha umahiri wowote kwa warembo hao. mwingine kajidai Kifaransa wala hajaulizwa! Warembo wote hawajaonyesha umahiri wowote kwa kutaka kuonyesha wanajua lugha ya Kingereza wakati wangeweza kuonyesha ujuzi wa mambo na umahiri wao katika lugha ya taifa na waliyoizoea. ngoja huko miss world tuone wakipeleka madudu.
 
Ushindi wa sitti mtemvu nimeufurahia sana. ..wale mapedeshee wanaotishia vitoto vya watu kwa mandinga kuwahonga hapa kwa sitti wabadili mbinu kwani mtoto hata hajashiriki haya mashindano anacruise ndinga za maana. ..nilibahatika kuwaona hawa mamiss before leo huyu sitti alikuwa ana confidence sana na kwa talent ya kudance nyoko. ..anakatika balaa
 
Hivi kwani lazima watumie Lugha za kigeni?

Ushamba unawasumbua kwani wao wanafikiri ukiongea Ung'eng'e ni Ujanja hata kwa kukariri bado wanajiona ni wana-England wazaliwa Ulaya, huu ujinga wa kudhani English ni bora kuliko Kiswahili unafaa ukemewe kwa nguvu Zote na Waziri wa Utamaduni sanjari na Waziri wa Elimu.
 
Lundenga hana udhamini wa kutosha jamani anadaiwa sana patel aliweka zuio la kufanyika kwa kudaiwa 20mils so inawezekana walikaa mezani kusuluhisha uenda makubaliano ni kulipa deni soon baada ya kufanyika so ili akidi itimie inawezekana kachukua fungu kutoka kwa mtemvu ili akisemwa semwa sana baba yake wanamuongezea kiki.

Huenda Kalipiwa Deni kwa Masharti Kuwa lazima Binti awe Miss Tz kwa mbinu yeyote ile, huu kwa kweli ni Uchakachuaji wa hatari ni Kama wa Sita kule kwenye Bunge la katiba . Nchi hii kuna masiara kila kukicha !
 
Mimi mashindano yoyote siwez kabisa ntapata presha bure ya kukosa zawadi
ha ha ha ha ha ha ha ha, hiini kali sasa. unahitaji cancelling tu, na ukishiriki hata mara moja unazoea, kila kitu kinaanza kidogo na uoga lazima uwe nao
 
Hakyanani kabisa wamechakachua, inawezekana kuna mzee pale alipewa ahadi siyo bure

Waandaaji walikuwa na Vimeo vyao huenda wajanja wamejipenyeza kwenye kuvisawazisha kisha Malipo ni kumpa Umiss Tz Kama shukurani.
 
Hii ndiyo Tanzania hakuna lisilowezekana, watu wakiamua kukuletea Yao hata ufanyeje wataleta tu, jawabu mtalipata miss Dunia kwani pale Uchakachuaji haupenyi kirahisi Kama Bongo.
 
Mfyuuuuuuu yani leo wameniuz inabid nisonye tuuu
 
Hii nchi in a matahira wengi,sasa unaambiwa uchague lugha mbili we unaongeza ya tatu......Hizo dharau sasa!!!
 
Kweli wamefulia, yani leo Miss Tanzania halafu watu wengine wala hatuna habari...wakati kipindi kile ilikuwa hatumwi mtu dukani...

Bora hata nilivyolala tu...
 
Hii nchi in a matahira wengi,sasa unaambiwa uchague lugha mbili we unaongeza ya tatu......Hizo dharau sasa!!!

Ha ha ndo mana Tanzania majority ya watanzania wana iq ndogo hapo kama ni mtihani si kashafeli ndo nashangaa eti mshindi kingereza na kifaransa kwani yale yalikua mashindano ya lugha
 
Nikiripoti kutoka insta
 

Attachments

  • 1413071736831.jpg
    1413071736831.jpg
    65.6 KB · Views: 1,465
Hapa Tz kuna watu huwa wanafikiri Kuwa Mtu akizungumza Kingereza ni Msomi, hawajui Kuwa Taaluma na Lugha ni vitu viwili tofauti , kwani Taaluma hupatikana kwa Lugha za Kichina, kifaransa, kijerumani, kispain nk, na wengine wana PHD kwa lugha zao na hawajui Kingereza na maisha yanaendelea , huu ukumbuke wa kufikiri kwa Lugha za kigeni Utakwisha lini? Kwa staili hii kiswahili hakitakaa kikue kwani Hakuna kiongozi mwenye ujasiri wa kusisitiza watu kuipenda Lugha ya Taifa.

Tanzania haina tabia ya kufanya vizuri, bora liende, bora tulishiriki.
 
Back
Top Bottom