kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Kingereza chenyewe cha kukariri.. ovyoooo wala haikuonyesha umahiri wowote kwa warembo hao. mwingine kajidai Kifaransa wala hajaulizwa! Warembo wote hawajaonyesha umahiri wowote kwa kutaka kuonyesha wanajua lugha ya Kingereza wakati wangeweza kuonyesha ujuzi wa mambo na umahiri wao katika lugha ya taifa na waliyoizoea. ngoja huko miss world tuone wakipeleka madudu.Kati ya washiriki 30 wa Redds Miss Tanzania..Sitty Mtemvu ndiye aliyenyakuwa taji hilo akitokea wilaya ya Temeke.
Ushindi huo unampatia zawadi ya sh 18 Milioni.
Wakiwa Jukwaani wakati wa shindano hilo la Redds Miss Tanzania 2014 hakuna hata mshiriki mmoja kati ya watano waliofanikiwa kuingia kwenye tano bora aliyejibu swali kwa lugha ya Kiswahili..wote walitumia lugha ya Kingereza na mshiriki mmoja kutumia lugha mbili ya Kingereza na Kifaransa
Wanaharakati mbalimbali nchin wanafanya juhudi za kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya bara la Afrika cha ajabu sisi wenyewe Watz tumekuwa tukikionea aibu Kiswahili kukizunguza ktk majukwaa mbalimbali kama Miss Tz.
My take.
Jamani Tanganyika tuikatae,hata Kiswahili pia tukikatae?