I was there. Mtu akijibu swali bila kubabaika ni kosa?
Lakini, pia tujiulize, wale wengine walistahili nafasi ya kwanza?
Maana Miss Tanzania ni mshiriki wa Miss World moja kwa moja. Je, alieshinda taji ataweza kwenda kushindana huko kwenye Miss World?
Kwakifupi, wote hawakulielewa swali husika, ndio maana huyu alieshinda, ameshinda kwa "confidence" yake lakini siamini kama alishinda kwa uzuri. Najua kuna wadada wazuri sana ambao hawakushiriki kwenye mashindano ya mikoani kwasababu mashindano haya yalichafuliwa na viongozi wa zamani wa Miss Tanzania Organization. Huyu Basila Mwanukuzi ni Kiongozi mpya na ndio mara ya kwanza anasimamia Miss Tanzania Beauty Contest. Naamini NEXT YEAR watajitokeza wadada WAREMBO zaidi na Wenye uwezo zaidi kushiririki. Kwa Mtazamo wangu tu, jana Hamisa Mobetto kama angekuwa anashiriki basi angewashinda wote mapema. She Looked splendid and gorgeous. Thats just my opinion.