LGE2024 Missenyi, Kagera: Kada CHADEMA, Joseph Elemedius auawa akingojea Uteuzi kugombea Serikali za Mitaa

LGE2024 Missenyi, Kagera: Kada CHADEMA, Joseph Elemedius auawa akingojea Uteuzi kugombea Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Hivi uenyekiti wa mtaa au Kijiji unalipa saaana. Ukitaka kuamini watu wanaudumavu wa akili nchi hii fuatilia uchaguzi wa serikali za mitaa.
 
Alianza vizuri sama sasa anamwaga damu kwenda mbele yeye abakie madarakani khaaaaa damu za watu hazitaenda bure
 
Tanzia.

Joseph Elemedius (57) ambaye alikuwa amechukua fomu ya kugombea Uenyekiti wa Kijiji cha Kalagala Wilaya ya Missenyi ameuawa usiku wa kuamkia leo. Joseph ameuawa wakati akisubiri uteuzi.

Kwetu sisi hili ni shambulio kubwa na tunategemea kuona watu waliofanya unyama huu wako mikononi mwa polisi.

Zacharia Obad
Katibu wa CHADEMA Kanda ya Victoria.


===============

JESHI LA POLISI LAELEZA
JamiiForums imezungumza na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa SACP Blasius Chatanda amesema “Nipo eneo la tukio, tunafanya utuatiliaji wa kina, sasa hivi ni mapea kutoa taarifa kamili, ni wajibu wa umma kujua kilichotokea.”

Pia soma ~ Polisi: Kada wa CHADEMA aliyefariki alipata ajali ya Bodaboda akiwa amelewa
Sasa tushike lipi???
Chadema wanadai kada wao ameuawa nalo jeshi la police linasema amepata ajali.
 
Back
Top Bottom