Uchaguzi 2020 Misungwi: Alexander Mnyeti hajapita bila kupingwa, Mgombea wa CHADEMA ameteuliwa kupambana naye

Uchaguzi 2020 Misungwi: Alexander Mnyeti hajapita bila kupingwa, Mgombea wa CHADEMA ameteuliwa kupambana naye

Hao wanaotaka kupita bila kupingwa wanamambo yao binafsi ya kumharibia Magufuli Sasa unapita bila kupingwa, unakaa anasubiri kuapishwa na hujafanya kampeni kwa wananchi kwaajili ya chama chako ili wakupigie kura na ngazi zingine zipigiwe Kura kwa hamasa wewe unakwenda kulala kwamba kazi imeisha kwenye Jimbo lako Sasa huoni nikuabisha chama kwa mbinu za kijinga? Hebu waache kuharibu sifa ya chama kwa kupita bila kupingwa.
 
Uhuni ndo lugha sahihi ya kinachoendelea, Mpaka waziri mkuu alikuwa ni mtu namheshimu sana lakini naye ameshiriki vitendo vya kiharamia ili naye apite "bila kupingwa"
Yani ilikua anaonekana ni MTU mwenye hekima na busara sijui kwa nini aliamua kuingia ktk huu mtego
 
Nnachojiuliza tu, ni hao watekaji waliofeli na pesa ya watu wamekula! Hawajachezea makofi kweli?!
 
Kama haya mabarabara, madaraja na majumba yangekuwa na maana kubwa hivyo, kwa nini wateke wagombea wa vyama vingine eti wapite bila kupingwa? Wanajua kuwa madaraja hayagusi mioyo ya watu.
Acheni drama za kitoto. hakuna mgombea yoyote anaetekwa.
 
Kama haya mabarabara, madaraja na majumba yangekuwa na maana kubwa hivyo, kwa nini wateke wagombea wa vyama vingine eti wapite bila kupingwa? Wanajua kuwa madaraja hayagusi mioyo ya watu.
Umesema ukweli ndugu yangu. Wazazi wangu kule ndani ndani kijijini huwezi kumshawishi akupigie kura kwa kumtajia kununua ndege 11, na kujenga madaraja ya juu
 
chadema ni watoto, mnafahamu jinsi watoto walivyo, ...
 
Ni kweli kwamba Mgombea wa CHADEMA, Mwl Shija alivamiwa na watu waliotumwa kumpora fomu ili akose uteuzi kwa malengo ya kumpitisha Mnyeti bila kupingwa lakini alichoporwa ni fomu feki.

Amewasilisha fomu halisi kwa Mkurugenzi na ameteuliwa, anazo nyaraka zote za tume za kumtambulisha kama mteule kwa hiyo hizo porojo kwamba Mnyeti kapita bila kupingwa zipuuzwe, atalazimika kuutafuta ubunge jukwaani.


View attachment 1548289
Hata mauzauza yanapatikana hapa Tanzania pekee Duniani.Tafsiri ya kupiga bila kupingwa ni IPI?Ninavyoelewa miye ni kwamba kunakuwa hakuna aliyejitokeza kuchukua fomu.Hawa wagombea waliopitishwa bila kupingwa kwa msamiati wa kiccm wote wanatabia au hali zinazofanana,Mara zote huwa ni CCM,wenye madaraka serikali ni au fedha nyingi za kuhinga wagombea wengine toka upinzani ama wasimamizi/wajumbe.Tujiulize,ukiwa na akili zako timamu utaamini kuwa bado wanafaa kuwa viingozi?
Wakati mwingine hujitokeza hali isiyokuwa ya kawaida kama vile kutekwa,kuporwa fomu,kujeruhiwa au kukamatwa na vyombo vya dola muda mfupi au wakati wa kuchukua,kurudisha fomu au kabla ya uteuzi.Je,tuendelee kuiamina hii coincidence? Yaweza kuwa kweli wapinzani hawa ni wahalifu wa kukamatwa kipindi cha uchaguzi tu?Hili nalo ni kawaida?
Kwa mini kusiwe na namna ya kurekebisha hali hii?Uzoefu unaonyesha matukio kama hata hujitokeza nyakati za uchaguzi,vyombo vyetu vya usalama hawajifunzi kutokana na matukio kama haya yaliyowahi kutokea ili kuyazuia kabla.Wapinzani wanashindwa kurejesha fomu kwa sababu wasimamizi hawapo ofisini au zimefungwa tena Siku za mwisha za uchukuaji/urejeshaji wa fomu.Hii nayo pamoja na kukemewa bado linafanyika sehemu nyingi na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa au kigugumizi kinatawala kuhusu hali za wanaoathirika na uzembe kama huo.Wanafungua ofisi au kuonekana baada ya saa zilizowekwa kuwa zoezi limeisha kuja kuwatangaza wagombea kupita bila kupingwa.Wahusika bado wapo katika hizi nafasi zao as if hakuna kibaya hapo.
Nashauri utaratibu wa rufaa,kusikiliza malalamiko uwepo ili waathirika wapate hali zao za kugombea.Uwajibishaji wa wasimamizi ufanyike Mara moja ili kuepusha mazoea na pia wagombea wa nafasi yoyote hata kama ni moja,apigiwe kura za ndiyo au hapana na asilimia zizingatiwe aka zoezi LA kutafuta wagombea wengine lifanyike.Hii itaondoa watu kutumia rushwa kubaki peke yao maana wanafahamu kuwa wanakuwa wamepita kuwa viongozi au iwekwe sheria ya kila nafasi I we na washindani wasiopungua wawili kwa kila uchaguzi.
CCM, nchi hii ni yetu sote.
 
Ni kweli kwamba Mgombea wa CHADEMA, Mwl Shija alivamiwa na watu waliotumwa kumpora fomu ili akose uteuzi kwa malengo ya kumpitisha Mnyeti bila kupingwa lakini alichoporwa ni fomu feki.

Amewasilisha fomu halisi kwa Mkurugenzi na ameteuliwa, anazo nyaraka zote za tume za kumtambulisha kama mteule kwa hiyo hizo porojo kwamba Mnyeti kapita bila kupingwa zipuuzwe, atalazimika kuutafuta ubunge jukwaani.


View attachment 1548289
Walitumwa na Mnyeti, tena hao ni warundi inavyosemekana,
 
Huyo mgombea alicheza kama KGB kutegesha fomu fake,,mi nashangaa hao wanaoporwa wanakuwa hawajui huu ndo msimu wa kukaa chonjo masaa yote,,,
True meaning of Wary Transgressor.
Definition of wary
: , cunning, and watchfulness especially in detecting and escaping danger
Kwny aina ya demokrasia hii ya kunyang'anyana form inaangukia kundi gani?
 
Umesema ukweli ndugu yangu. Wazazi wangu kule ndani ndani kijijini huwezi kumshawishi akupigie kura kwa kumtajia kununua ndege 11, na kujenga madaraja ya juu
Kuna wahuni hapa JF waliweka hii picha mkuu.
JamiiForums-561822830_720x720.jpg
 
Uhuni huu utaisha kwa Watanzania kuukataa tu. Ajabu kuna kundi kubwa wanaushangilia kwa vigelegele. Maadili yetu kama Taifa yamekwenda wapi?
kwa jinsi watanzania wengi walivyo wajinga huwa naona bora ccm iendelee kuwafisadi tu, maana mijitu haijitambui.

Unakura sehemu kuna wizi wa kura ili lijitu linashangilia tu, na wajinga wengine wamejaaaa, kutwa kucha wao ni kusifia ccm tu hata kwa matendo ya ccm yaliyo dhahiri shahili
 
Back
Top Bottom