Misururu mirefu na misongamano ya vijana kujiandikisha kujiunga na Chama cha Mapinduzi ni mikubwa mno. Hongereni sana vijana Tanzania

Wanaugua Suruwa hao sio bure.
Kujiunga na Vigagura yataka usukule.
nimefurahi wamejiepusha kujiunga na vyama vya siasa vyenye kujihusisha na magenge ya kihalifu kama kile ambacho waandamizi wake wametiwa nguvuni na bado wanasota lupango πŸ’
 
Ikumbukwe pia kwamba, kuna kujiunga kwa kushawishiwa kwa kupewa kitu au kuahidiwa ila katika swala la uchaguzi linabaki ni uamuzi wa mhusika.
 
Sawa mkuu maana kijana wangu jana alikuja na kofia ya chama na yupo form two....
I hope ni above 18 huyo, ama yuko chini ya hapo wakampooza na kofia baada ya kutaka kulazimisha kuandikishwa?🀣

maana wanaoneana wivu sana watoto wa siku hizi hakuna anaetaka kuonekana mdogo kwa mwingine πŸ’
 
Ikumbukwe pia kwamba, kuna kujiunga kwa kushawishiwa kwa kupewa kitu au kuahidiwa ila katika swala la uchaguzi linabaki ni uamuzi wa mhusika.
hiyo inafanyika zaidi mtaani kwa wahitimu wa vyuo ambao wamekutana na maisha tofauti mtaani, wafanyabiashara, wakulima, wafugaji, wasafirishaji, makundi maalumu n.k. hawa tunatumia ushawishi wa kisera, vipaumbele na mahitaji yao ya msingi kulingana na kundi walilopo...

ushawishi wa zaidi ya hapo ni binafsi πŸ’
 
Ukweli ni kwamba vijana wanajiunga mbogamboga kwa manufaa yani ujue kunafursa imeonekana huko.Tofauti na hapo tunadanganyana
 
Yes,
Baraka na Neema za Mungu zilipa for sure, hakiwezekani bila hizo gentleman πŸ’
Lazima wakulipe,wenzenu wakina steve nyerere na machawa wengine wako kwenye payroll ohoo,changamka usizubaezubae
Wakulipe,mnafanya kazi kubwa mjuwe

Ova
 
Wekeni katiba mpya am tume huru ya uchsguzi muone hali halisi.
Sasa hivi ni kila mtu anapeleka njaa zake
hilo ni jambo la kitaifa kwa wananchi wote,sio suala la CCM πŸ’

CCM ina vipaumbele vyake, mipango yake na ratiba zake kama hii inayoendelea hivi sasa, hata hivyo

CCM inaweza kulifanyia kazi jambo hilo baada ya uchaguzi mkuu kulingana na mipango na ratiba zake πŸ’
 
Hapo zishatembea elf 20/20 yani kwa mtoto wa shule maskini hio hela anaona ndefu mno anaizika future yake
kujiunga CCM ni uzalendo wa kiwango cha juu sana, kwa maslahi mapana na manufaa yako mwenywe na Taifa kwa ujumla...

kwahiyo gentleman,
ungependelea zaid kijana ajiunge na vyama vyenye mirengo ya magenge ya kiahalifu ili akasote lupango kama wale jamaa waliotiwa nguvuni huko mbeya?πŸ’
 
Ukweli ni kwamba vijana wanajiunga mbogamboga kwa manufaa yani ujue kunafursa imeonekana huko.Tofauti na hapo tunadanganyana
ndiyo,
kujiunga CCM ni fursa ya kipekee mno....
ni uzalendo na ufahari wa kiwango cha juu sana kwa vijana hawa na wana CCM wote hujiskia wakiwa ndani ya CCM,

kwani wewe ulitamani hawa vijana nao wapate fursa ya kutiwa nguvuni sambamba na viongozi wa vyama vyenye mirengo ya magenge ya wahalifu?πŸ’
 
Wamefuata rushwa.
upotoshaji sio deal..

mashuleni tunazo clubs za kupambana na rushwa na kwahivyo haiwezekani makamanda wanafuzi wa rushwa kujihusisha na rushwa hata kidogo....

kwa hiyari, utashi na mapenzi yao,
vijana hawa wameamua kujiunga CCM πŸ’
 
Wakati vyeo vya juu wanapeana wao na familia zao,hao wengine
Labda wanapewa kazi ya kulamba viatu

Ova
huo ni upotoshaji,

hakuna kupeana vyeo kwenye chama wala serikalini,

dhama za umma hutolewa kwa niaba ya waTanzani kwa watu wenye vigezo na sifa stahiki na bila kujali vyama vyao vya siasa, dini,rangi wala kabila zao ilimradi tu awe mTanzania mwenye sifa πŸ’
 
Pole sana

Ova
 
Lazima wakulipe,wenzenu wakina steve nyerere na machawa wengine wako kwenye payroll ohoo,changamka usizubaezubae
Wakulipe,mnafanya kazi kubwa mjuwe

Ova
nadhani sihitaji malipo ya aina yoyote kwenye kusema ukweli,

ile kidogo wananchi wananipatia nikifanya kazi yao inanitosha mimi na familia yangu kujitosheleza...

hata hivyo kazi za mikono yangu shambani, na hii ingine ya ng'ombe na kufundisha huko kwa vyuo inanilipa vizuri zaid πŸ’

zaidi sana,
ni Neema na Baraka za Mungu katika kazi na majukumu yangu zinanipa nguvu zaidi, furaha na moyo wa kutokukata tamaa kabisaa licha ya ugumu na uzito wa baadhi ya mambo...
You understand what I am saying?πŸ’
 
Kuna uhalifu mbaya kuliko kuwaibia waTanzania raslimali zao? Halafu ni wapi umeona wamepanga foleni wanajiunga na CCM leta picha. Watu wa leo siyo wa mwaka 47
 
Kuna uhalifu mbaya kuliko kuwaibia waTanzania raslimali zao? Halafu ni wapi umeona wamepanga foleni wanajiunga na CCM leta picha. Watu wa leo siyo wa mwaka 47
picha ni kwa walio na imani haba kama Thomaso, je nawe ni ndugu wa Thomaso mpaka uone picha ndipo uamini?πŸ’

by the way,
picha ni kwajili ya kutafuta kiki au umaarufu, mimi nadeal na ukweli tu gentleman,
usijifungie ndani toka nje mtaani ujionee hali halisi πŸ’

uvunjifu wa amani na utulivu wa wananchi waTanzania ni uhalifu wa kiwango cha juu sana kuliko hayo yakusadikika unayoamini πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…