Ndugu zangu,
Wanafunzi wa sekondari na wa elimu ya juu ngazi mbalimbali nchini karibuni sana chama Tawala...
Kwanza hongerini sana kwa kuhamasika kiasi hicho na kuamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM. mmefanya uamuzi wa hekima na busara sana kwa faida na mustakabali wa maisha yenu wenyewe.
Nawapongeza kwa kutambua kwamba mna wajibu katika kulitumikia taifa kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Huo ni uamuzi wa kizalendo na kijasiri sana. Mwenyekiti wa CCM taifa Samia Suluhu Hassan amefurahi sana, na kwasababu ya majukumu mazito mengi ya kitaifa na kimataifa, huenda akapata muda wa kuzungumza nanyi baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
hakikisheni wote mnajiandikisha na kua wanachama wa CCM, sambamba na kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa na vijijini, lakini pia kwa wale wote ambao hawakujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura miaka ya nyuma, kwasababu za kuimri ule, huu ndio wakati wenu muafaka, jiandikisheni sasa.
CCM ndiyo pekee chama kinachoaminika kwa umma, kitaifa na kimataifa, kinapendwa na wa Tanzania wote, kina aminika, ndicho chenye Serikali na kina ongoza dollar, ndicho chenye sera nzuri za kueleweka na kutekelezeka, chenye uelekeo wa wazi na chenye uhakika wa kushinda uchaguzi kwa kishindo bila mbambamba yoyote.
Daima epukeni kurubuniwa na kujiunga na vyama vya vya kisiasa vyenye sura na mienendo ya magenge ya kihalifu, mtapata tabu sana..🐒
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Mungu Ibariki Tanzania.