Kwa Tanzania kama mtaa wenu u a open space, inabidi huo mtaa muwe watu wa umoja, maana mkitetereka kidogo tu unashangaa mijitu ishajimilikisha.
Nimeona baadhi ya mitaa ambayo wananchi wake wako serious, wanaziwekea thamani hizi open space kwa kuzipanda garden zenye miti mizuri ya kupumzikia, viwanja vya michezo (vya kueleweka).
Ushauri. Kama mtaani kwenu hizi open space kama bado zipo, unaweza washawishi wakazi kuitisha mkutano na kuvipangia muziendeleze vipi hizi open space? Mfano; kama mfuko wenu upo vizuri mnaweka mchoraji anaplan halafu mnaifanyia utekelezaji.
Hapa ngoja niweke mfano wa jiji la New York, Central park. Watu waliostaharabika wenye akili kubwa ya kutunza mazingira na mipango miji ya kueleweka.
View attachment 3002335
View attachment 3002336