Mitaala ya somo la Historia iliyositishwa ilijaa propaganda za kumsifu Magufuli kuwa ni kinara wa mabadiliko nchini

Mitaala ya somo la Historia iliyositishwa ilijaa propaganda za kumsifu Magufuli kuwa ni kinara wa mabadiliko nchini

Status
Not open for further replies.
Katiba mpya hazizuzii kina Magufuli.

Kina Magufuli huwa hawafuati KATIBA.
Katiba ya Sasa inampa mamlaka rais kuingiza kichwa kwenye mifumo takriban yote huku wakituhadaa kuwa hatoingia mzima. Sasa wewe unaelewa Tembo akiingiza kichwa atashindwaje kuingia mzima akitaka?

Tunataka katiba ambayo kuna baadhi ya vitu hata kuvisogelea tunampiga stop achilia mbali hiyo nafasi ya kuingiza kichwa!

Vitu kama mahakama na bunge raisi anapaswa akae mbali navyo, asiwe na mkono wake mle tofauti na sasa ambapo yeye ni sehemu ya kwanza ya bunge na ukina kwenye mahakama yeye ndo bosi wa DPP na ndiye anayemteua, na anateua Majaji wote hadi mkuu wao yaani Jaji mkuu
 
Huu ni upotoshaji wa makusudi kabisa
Somo la historia lipo miaka nenda Ila halikuwa la lazima, kilichotaka kufanyika ni kuliweka hili somo kuwa la lazima Kama lilivyo somo la uraia civics/ general study
Wewe na nyiendio mnaopotosha sema ukweli wa unalofahamu ili usilofahamu ufahamishwe.Vinginevyo ni wale wale.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Katiba zinajengwa na kulindwa na watu.

Usitegemee katiba ndio itaandamana badala yako pale haki zako zitakapokiukwa.

Kama watu hawajawa tayari kwa hilo hakuna namna ya kulifanya.

Siku watu wakihitaji katiba mpya, itapatikana ndani ya muda mfupi tu. Sasa hivi wananchi wa kawaida bado wanaona katiba mpya hakuna namna itawasaidia kuwaletea tonge mezani.
Katiba Bora inabalance mambo..Mfano Matendo ya magufuli yangeweza kupingwa na Mkurugenzi wa usalama wa taifa kama kungekuwa na katiba yenye checks and balance. Yaani matendi ya magufuli yalikuwa yakihatarisha usalama wa taifa letu hivyo asingepewa upenyo.
 
Hakijavuja hata kitabu kimoja kiwe sample huku mtaani au smartphone ya chanzo haina scanner
Bila hata kuona kitabu, namna amri ya kuanzishwa hili somo ilivyotolewa inaonyesha utaalam haukuzingatiwa. Mitaala ya masomo haianzishwi na kutayarishwa kwa gahafla namna hiyo. Inatakiwa kwanza ifanyike research na wataalam wa kuandaa mitaala wapewe muda ili kuandaa. Tulikuwa na rais kichaa.
 
Uizia Wizara ya Ujenzi alikokuwa, he was a forgerer all along.
Ndio maana wale walioshutumu jinsi ilivyopatikana PhD yake (tena somo gumu la Kemia) aliyosoma miaka miwili walipotezwa.
Kimsingi huyu jamaa hakuenda moja kwa moja Chuo Kikuu, alienda ualimu .
Maana yake unaelewa kama ni msomi.
Phd ya mashaka. Ndio maana baada ya kupata Urais Maprof wote wa udsm walipata vyeo. Ni kama alikuwa analipa fadhila
 
Si mara ya kwanza zimamoto imeleta hasara kubwa kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania.

Taratibu zina faida zake
Na hao TET walishindwa kusimamia taaluma na sheria zao kuzuia mwendazake asiwapangie ??, ona sasa, shilingi ngapi zimepotea hapo ??
 
Chanzo chetu kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) kimeiambia SAUTI KUBWA: “Sehemu kubwa ya vitabu vilivyochapishwa imebeba historia potofu; inasifia mmoja wa marais wa Tanzania kuwa ndiye kinara wa mabadiliko ya maendeleo yanayoonekana sasa, hatua ambayo haina usahihi.” TEA ndiyo waandaaji wa mitaala ya elimu nchini Tanzania.
Hicho chanzo ni TET siyo TEA, isitoshe ni kwamba waandishi ndiyo walijipendekeza kuandika hizo sifa, wakati mwingine hata ibilisi anasingiziwa tu, Mwendazake hakuwapelekea TET cha kuandika wala kuwalazimisha wamuandike ila kuna kasumba imejengeka kwa wengi wa viongozi kutojitegemea kiakili isipokuwa mentality ya kujipendekeza
 
Akiwa mjini Morogoro Februari 12, 2021, Rais Magufuli alikumbusha tena umuhimu wa somo hilo na kutishia kumfukuza kazi Prof. Ndalichako kwa kuendelea kuchelewa kulianzisha.

Juni 26, 2021, Prof. Ndalichako alitangaza kusitishwa kwa mchakato wa kuanza kufundishwa Historia ya Tanzania, akiueleza umma kwamba kuna “mambo yanaboreshwa kwanza.”
Kama ni Prof. kwelii alitakiwa kuonyesha msimamo tangu awali kulinda taaluma yake na kujitegemea kwa akili yake
 
Katiba ya Sasa inampa mamlaka rais kuingiza kichwa kwenye mifumo takriban yote huku wakituhadaa kuwa hatoingia mzima. Sasa wewe unaelewa Tembo akiingiza kichwa atashindwaje kuingia mzima akitaka?

Tunataka katiba ambayo kuna baadhi ya vitu hata kuvisogelea tunampiga stop achilia mbali hiyo nafasi ya kuingiza kichwa!

Vitu kama mahakama na bunge raisi anapaswa akae mbali navyo, asiwe na mkono wake mle tofauti na sasa ambapo yeye ni sehemu ya kwanza ya bunge na ukina kwenye mahakama yeye ndo bosi wa DPP na ndiye anayemteua, na anateua Majaji wote hadi mkuu wao yaani Jaji mkuu
Na Je, akizuiwa kuingia na akalazimisha kuingia mzima mtafanyaje ?

Africa tunajijua tulivyo mabingwa wa kukiuka kanuni na taratibu ndogo tulizojiwekea.

Katiba ngapi za Africa zina ukomo wa madarak, zinaheshimika ?

Kuna kubwa kuliko hilo ?
 
VITABU vipya vya “Historia ya Tanzania” vilivyokuwa vimechapwa kwa agizo la Rais John Magufuli havitatumika tena. Badala yake, vitaandaliwa vingine – endapo kutakuwa na umuhimu huo, SAUTI KUBWA imeelezwa.

Somo hilo lilipangwa lifundishwe kwa wanafunzi wa shule za awali hadi sekondari za juu kuanzia Julai Mosi mwaka huu. Kwa taarifa zilizopo, sasa itabidi somo hilo lisubiri au halitakuwepo kabisa kutokana na udhaifu uliogundulika.

Taarifa ambazo zimeifikia SAUTI KUBWA zinaeleza kwamba kusitishwa kwa somo hilo kunatokana na kile kinachoelezwa kuwa ni mkanganyiko wa “usahihi wa historia” iliyokuwa imelengwa na imechapishwa kwenye vitabu hivyo vya kiada.

Sehemu kubwa ya historia hiyo ilikuwa imeandikwa kama propaganda za kusifu watawala na kubeba taarifa nyingine zisizokuwa sahihi, hasa katika kuelezea mwenendo wa kuimarika kwa uchumi na maendeleo ya siasa nchini Tanzania.

Chanzo chetu kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) kimeiambia SAUTI KUBWA: “Sehemu kubwa ya vitabu vilivyochapishwa imebeba historia potofu; inasifia mmoja wa marais wa Tanzania kuwa ndiye kinara wa mabadiliko ya maendeleo yanayoonekana sasa, hatua ambayo haina usahihi.” TEA ndiyo waandaaji wa mitaala ya elimu nchini Tanzania.

Alisema vitabu hivyo vilisheheni sifa kwa Rais Magufuli, huku viongozi wengine waliomtangulia wakitajwa kwa mbali kama sehemu ndogo au “wakibebeshwa lawama” kwa baadhi ya madhila yaliyoonekaa kushamiri Tanzania.

Miezi michache kabla ya kifo chake, Rais Magufuli ndiye alitamka hadharani, na kaagiza waziri wa elimu, kwamba kuna ulazima wa kubadili mitaala na kuandika upya vitabu vya somo la Historia na kwamba lianze kufundishwa haraka tangu madarasa ya awali. Magufuli aliaga dunia Machi 17, 2021.

Ofisa mwandamizi wa TEA ambaye hakupenda kutajwa jina lake alisema kuwa uamuzi wa kusitisha vitabu hivyo umefikiwa baada ya serikali kubaini kwamba somo hilo litakuwa limejaa hadaa za kisiasa, jambo ambalo ni upotoshaji wa historia halisi ya Tanzania.

Rais Magufuli alitaka somo hilo liwe maalumu, akidai kwamba Watanzania wengi hawajui historia ya nchi yao. Hata hivyo, historia ya Tanzania, miaka nenda rudi, imekuwa ikifundishwa shuleni katika somo la historia na kama sehemu ya somo la Uraia.

Kauli ya Rais Magufuli ilitolewa Desemba 9 mwaka jana wakati akiapisha mawaziri wapya Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma, akamwagiza Prof. Joyce Ndalichako kuhakikisha somo la Historia ya Tanzania linaanza kufundishwa upya na haraka – na kwamba liwe ni somo la lazima kwa kila mwanafunzi.

Februari 12, 2021 Prof. Ndalichako alisema wizara hiyo ilikuwa imeanza utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli mara moja kwa kuandaa muhtasari ambao ungewezesha somo hilo kuanza kufundishwa kutoka madarasa ya chini hadi kidato cha sita.

Alisema kwamba somo hilo lingesaidia “kujenga moyo wa uzalendo” kwa kuwafanya Watanzania kuifahamu nchi yao, kuithamini na kuipenda na kujenga moyo wa kulinda rasilimali; akasema maandalizi – ikiwa ni pamoja na kuandika vitabu hivyo – yalikuwa yanaendelea vema.

SAUTI KUBWA inazo taarifa kuwa kazi ya kuandaa na hatimaye kuchapishwa vitabu vya somo hilo ilikamilika mwezi Aprili, 2021 na zilikuwa zikisubiriwa fedha za kuanza kuvisambaza shuleni.

Wadau wengi wa elimu walilaumu serikali kwa kuanzisha somo hilo kana kwamba ni jipya huku wanafunzi wamekuwa wakilisoma miaka yote kuanzia madarasa ya chini.

Akitoa maoni yake, mhadhiri mstaafu wa vyuo vikuu, Dk. Lenny Kasoga, amesema kuwepo kwa “somo la Historia linalojitegemea” ni mzigo mwingine kwa serikali na matumizi mabaya ya raslimali fedha.

“Wanafunzi wamekuwa wakisoma historia ya nchi yetu. Sasa kuwaongezea somo jingine ni kuwapa shida watoto wetu. Kwanza tayari wana masomo mengi sana,” aliongeza msomi huyo wa siasa ya uchumi.

Akiwa mjini Morogoro Februari 12, 2021, Rais Magufuli alikumbusha tena umuhimu wa somo hilo na kutishia kumfukuza kazi Prof. Ndalichako kwa kuendelea kuchelewa kulianzisha.

Juni 26, 2021, Prof. Ndalichako alitangaza kusitishwa kwa mchakato wa kuanza kufundishwa Historia ya Tanzania, akiueleza umma kwamba kuna “mambo yanaboreshwa kwanza.”

Wachambuzi wa siasa na wanazuoni walitoa maoni na kutoona mantiki ya kuanzishwa kwa somo jipya, na sasa wanabashiri kwamba huenda somo hilo halitakuwepo tena kwa kuwa si kipaumbele cha Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alirithi madaraka kutoka kwa Magufuli.

Mwalimu Phoebe Makelemo, ambaye sasa ni mshauri wa masuala ya elimu katika balozi kadhaa nchini ni mmoja wa wataalamu wa elimu ambaye alipinga kuanzishwa kwa somo hilo, alihoji umuhimu wa somo hilo sasa na uharaka wake huku akitahadharisha kupotoshwa au kuandaliwa kwa mtaala ambao hauna vigezo ili tu kukidhi matakwa ya rais.

Mwalimu huyo alisema katika kuandaa mitaala yapo mambo ya msingi kuzingatia, na kwamba ana shaka endapo yalifuatwa.

Mambo hayo ni pamoja na kufanya maandalizi ya ufundishaji ni kuchambua muhtasari wa somo na vitabu vya kiada kwa somo husika ili kubaini mada kuu na mada ndogo zilizopo na kuzipangilia kimantiki kufuatana na mazingira ya ufundishaji unaoukusudia, uandaaji wa azimio la kazi, uandaaji wa somo na zana pamoja na mbinu za kufundishia.

“Shaka ni kwamba mambo haya hayakuzingatiwa kwa kuwa kulikuwa tu na msukumo wa rais, na kwamba muda haukuweza kutosha kuwa na mitaala yenye maana pana na kubeba dhana iliyokusudiwa,” alisema na kuongeza: “Hawa walichofanya ni kazi ya zima moto.”

Source: Sauti Kubwa
Jamani inatosha. Hiyo legacy ya JPM mnayojaribu kuiua mpaka kwa propaganda haiwezekani. Nasema tena haiwezekani. Kila mtu ana macho na ameona kilichotendeka katika awamu zote. Mnatumia nguvu kubwa sana.

Huyu mtu ameshakufa mwacheni apumzike kwa amani. Kumtoa kwenye mioyo ya watanzania narudia tena haiwezekani.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Naanza kuelewa ni kwanini Mungu aliamua kufanya yake; fikiria hi elimu ingewafikia watoto/wajukuu zetu, imagine yaani!
Unataka kumuelewa Mungu utaweza? Mungu huyo huyo kamchukua Magufuli ila kamuacha Ibilisi hadi leo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom