Mitambo ya Rais Samia Yarejesha Bwawa lililopotea Handeni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MITAMBO YA RAIS SAMIA YAREJESHA BWAWA LILILOPOTEA HANDENI

Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bwawa la Maji Kwenkambala lililopo Kata ya Kwediyamba, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambao awali ulikumbana na changamoto kadhaa ikiwamo rushwa na kusimamishwa kwa wasimamizi wa mradi.

Akizungumza na wananchi katika eneo la mradi huo, Ijumaa Novemba 15, 2024 Waziri Aweso ameeleza kuwa safari ya kuanzisha ujenzi wa bwawa hilo haikuwa rahisi lakini sasa ameridhishwa kuona mitambo iliyonunuliwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa bwawa inatumiwa vyema kutokana na usimamizi mzuri wa mradi huo.

Kutokana na hatua hiyo ameahidi kuleta Shilingi Milioni 300 kwa ajili ya kuongeza kasi ya utekelezaji wake.

"Nilikuja hapa, hali ilikuwa ngumu sana, unamuuliza. Mkandarasi bwawa lipo wapi, halioni", ameeleza Aweso.

Aidha, amesema kuwa atahakikisha watu wa eneo hilo wanapata maji safi na salama, akieleza kuwa juhudi kubwa zimefanyika kuhakikisha maji yanapatikana wilayani Handeni chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
 

Attachments

  • GcfS9mRWkAAe7vW.jpg
    116.5 KB · Views: 3
  • GcfS9mPXcAAMuyj.jpg
    128.4 KB · Views: 6
  • GcfS9mKWAAAED7g.jpg
    131.9 KB · Views: 3
  • GcfS9mOW0AERBo3.jpg
    134.2 KB · Views: 4
  • GcfS-mRWMAE7XeE.jpg
    132.6 KB · Views: 3
  • GcfS-mQWEAAAXvr.jpg
    116.6 KB · Views: 4
  • GcfS-mPWQAA4pqx.jpg
    165.9 KB · Views: 4
  • GcfS-mPWsAAbs7o.jpg
    149.4 KB · Views: 4
Ila tanzania viongozi mjitathimini yaani handeni liwilaya likubwa ila hakuna maji salama wananchi wanatumia maji ya bwawani alafu tupo bize kumtafuta mchawi wa magonjwa ya kuambukiza ya matumbo.
Shameful kabisa.
 
Mitambo ya Rais Samia? Huu ujinga huwa hamjisikii vibaya kuuandika?
 
kunawatu wanaumia walitaka hahari isomeke mitambo ya mbowe
 
Sasa mkandarasi anaulizwa bwawa liko wapi halioni
Kweli ndio maswali ya kuuliza haya
Ipi siku na Indian ocean litapotea
Houdini bwana 😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…