Licha ya Mitandao ya Kijamii kurahisisha mawasiliano na kupatikana kwa taarifa katika jamii, imesaidia pia kukuza demokrasia kwa kuwawezesha wananchi kutoa maoni, kuhoji viongozi, na kushiriki mijadala ya kidemokrasia.
Kupitia majukwaa ya mitandao hayo kama WhatsApp, X (zamani Twitter), Telegram, Tik Tok, sauti za Wananchi wengi zaidi zinasikika bila vikwazo vikubwa.
Hata hivyo, Mitandao ya Kijamii imelalamikiwa kuchochea chuki katika jamii kutokana na baadhi ya watumiaji kutoa lugha za matusi, lugha za chuki na uchochezi. Hali hii imezua mjadala mpana kuhusu nafasi na mchango wake halisi katika kuimarisha au kudhoofisha demokrasia nchini.
Kutokana na nguvu ya mitandao, ndio maana baadhi ya nchi zimekuwa zikiizima nyakati za uchaguzi. Kwa mfano katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 intaneti ilizimwa baada ya maandamano kuanza nchini Tanzania.
Hata katika uchaguzi mkuu wa Uganda Januari 15, 2026, intaneti ilizimwa siku mbili kabla na kurudishwa simu mbili baada ya uchaguzi.
USHIRIKIANO KATI YA WANANCHI, WANAHABARI NA MITANDAO YA KIJAMII
Baadhi ya wananchi wanatumia Mitandao ya Kijamii kushiriki mijadala ya kisiasa, kutoa maoni kuhusu sera za serikali, na kuibua changamoto zinazowakabili katika jamii zao.
Kupitia machapisho, maoni na mijadala ya moja kwa moja (live), wananchi wanapata fursa ya kushiriki katika siasa bila kujali eneo walilopo. Hii imeongeza kiwango cha ushiriki wa wananchi, hususan vijana, ambao kwa muda mrefu walionekana kutokuwa na hamasa ya kushiriki katika masuala ya kisiasa.
Ushirikiano kati ya watumiaji wa mitandao ya kijamii na wanahabari unaweza kuimarisha zaidi demokrasia. Wananchi wanapotoa taarifa na wanahabari wakazihakiki na kuzipa muktadha sahihi, jamii hunufaika kwa kupata taarifa zilizo sahihi na zenye kuaminika.
Ushirikiano huu hujenga daraja kati ya sauti za wananchi na vyombo rasmi vya habari.
Matukio ya Oktoba 29, 2025 yameacha funzo muhimu kwa Watanzania kwamba, mitandao ya kijamii ni chombo chenye nguvu kubwa, ambacho kinaweza kujenga au kubomoa demokrasia.
WANAHABARI NA MITANDAO YA KIJAMII
Wanahabari nao wameathiriwa kwa kiasi kikubwa na ukuaji wa Mitandao ya Kijamii, kwani mazingira ya ukusanyaji na usambazaji wa habari yamebadilika kwa kasi kubwa. Leo, mitandao ya kijamii imekuwa chanzo muhimu cha taarifa, mawazo na mitazamo ya wananchi, na hivyo kupanua wigo wa habari unaowafikia wanahabari kwa wakati mmoja.
Kupitia Mitandao ya Kijamii, wanahabari wana uwezo wa kufuatilia kwa karibu mijadala ya kisiasa inayoendelea miongoni mwa wananchi.
Maoni, mijadala ya moja kwa moja (live), na machapisho ya Wananchi huwapa wanahabari dalili za masuala yanayowagusa watu kwa undani. Hii huwasaidia kubaini ajenda muhimu za jamii, mada zenye mvuto wa kitaifa, na changamoto zinazohitaji kuangaziwa na vyombo vya habari.
Aidha, mitandao ya kijamii imekuwa chanzo kipya cha vyanzo vya habari. Wananchi wa kawaida hutuma picha, video na ushuhuda wa matukio yanayoendelea, hali inayowawezesha wanahabari kupata taarifa kwa haraka zaidi kuliko hapo awali.
UCHAMBUZI WA MASUALA YA KISIASA
Kwa mujibu wa baadhi ya Wachambuzi wa siasa, mitandao ya kijamii imeongeza wigo wa mijadala ya kisiasa, lakini pia imeongeza mkanganyiko pale taarifa zinaposambazwa bila uchambuzi wa kina.
Pia amesisitiza nguvu ya Mitandao ya kijamii Ukitumia vibaya basi inaweza kubomoa jamii kwa sasa Dunia imekua na uhasama kutokana na mitandao ya kijamii basi isipo dhibitiwa inaweza kutule madhara makubwa
Hata hivyo, mchambuzi anaeleza kuwa mitandao ya kijamii si tatizo lenyewe, bali namna inavyotumika. Ikitumika vizuri, mitandao ya kijamii ni fursa kubwa ya kiuchumi na kijaimii.
“Ni chanzo cha ajira kwa vijana kupitia uundaji wa maudhui, biashara mtandaoni, uandishi wa kidijitali na ujasiriamali wa mtandaoni. Aidha, ni jukwaa muhimu la kupata maarifa, elimu na taarifa mbalimbali zinazowawezesha wananchi kujifunza, kujijengea uwezo na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii,” anasema.
NAFASI YA WAHAMASISHAJI KATIKA SIASA
Wahamasishaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa na nafasi kubwa katika kuchochea mijadala ya kisiasa.
Baadhi yao hutumia ushawishi wao kuelimisha umma kuhusu haki za kiraia, masuala ya uchaguzi, na uwajibikaji wa viongozi.
Hata hivyo, wapo pia wanaotumia ushawishi huo kusambaza taarifa zisizo sahihi au kuchochea misimamo mikali, jambo linalohitaji umakini mkubwa kutoka kwa watumiaji wa mitandao hiyo.
Kwa mfano, Maria Sarungi Tsehai ni mwanaharakati na mkurugenzi wa kampeni ya Change Tanzania, ambaye ametumia mitandao ya kijamii kama jukwaa la kuhamasisha ushiriki wa vijana katika siasa na kuzungumzia masuala ya kijamii na haki za binadamu. Kampeni yake ilizinduliwa kupitia hashtag (#ChangeTanzania) iliyosambaa mtandaoni na kuibua mijadala ya mabadiliko chanya.
Mange Kimambi pia ni mwanaharakati anayeishi nchini Marekani aliyejulikana kwa ushawishi wake mkubwa mtandaoni, hasa kwa kuhamasisha mijadala ya kisiasa kama vile maandamano ya October 29, 2025.
Hata hivyo, akaunti yake ya Instagram na namba ya WhatsApp zilifutwa na Meta, jambo aliloliona kama kuzuia sauti yake katika mazungumzo ya siasa mtandaoni.
HITIMISHO
Kwa ujumla, mitandao ya kijamii imekuwa nguzo muhimu katika kuonesha njia ya demokrasia katika siasa ya Tanzania. Imeongeza ushiriki wa wananchi, uwazi na uwajibikaji wa viongozi.
Hata hivyo, ili mitandao hii iwe chombo chenye manufaa zaidi kwa demokrasia, ni muhimu kwa wananchi, viongozi na wadau wengine kuitumia kwa uadilifu, busara na kuwajibika.
Demokrasia ya kweli haiishii kwenye uhuru wa kusema, bali pia inahitaji uwajibikaji katika matumizi ya uhuru huo.