SoC02 Mitandao ya kijamii ni jamvi linalotuunganisha, maudhui ya kikao juu ya jamvi yasitusambaratishe

SoC02 Mitandao ya kijamii ni jamvi linalotuunganisha, maudhui ya kikao juu ya jamvi yasitusambaratishe

Stories of Change - 2022 Competition

chime pinchi

Member
Joined
Aug 13, 2022
Posts
9
Reaction score
38
Ndugu msomaji wa makala hii, kwanza napenda kukukaribisha katika kuchanganua mawazo yetu kwa namna Moja ama nyingine Ili tu kujenga weredi na utashi wa maarifa yetu kupitia jamvi hili ambapo tunaketi na kujadili masuala ya msingi, yanayoweza kusaidia kuanzia mtu binafsi familia na hata maendeleo chanya ya taifa letu.

Kama ifaamikavyo neno jamvi halina tofauti sana na neno mkeka, ambao ufanana na kitu kinachoshonwa kutokana na Kili na huweza kutumika kukalia ama kutandikia kitanda. kama ilivyo kawaida katika tamaduni zetu za kitanzania jamvi limekuwa ni kitu au kifaa muhimu sana cha kukutania na kufanyia vikao ama kujumuika baada ya kazi ama wakati wa kula chakula, ama wakati wa faragha. Jaribu kupata picha Kwa familia za kawaida kabisa ambapo nyumba zilikuwa ni sehemu tu ya kujihifazi wakati wa usiku lakini mahali pa kukutania wageni palikua ni katika uwanja ama uwa wa nyumba. Vikao, mazungumzo ama faraga nyingi zilifanyika juu ya jamvi.

Hivyo basi taswira ya thamani ama hadhi ya mtu ilionekana kupitia jamvi ambalo mwenyeji aliwaandalia wageni kuketi. Naam namaanisha usafi wa Jamvi, ama uzuri wa jamvi ulitengeneza taswira ya ukarimu, hekima na busara ya mwenyeji, hivyo wageni walikaribishwa kuketi na kujadili mambo mbalimbali na hata wakati wa kutoa posa jamvi lilitumika.

Ndugu msomaji nimejaribu kufafanua kiundani maana halisi ya jamvi ili tu kupata taswira halisi ya umuhimu wa neno jamvi ambapo nimelifanannisha na mitandao ya kijamii ambayo imeonekana ikikua kwa kiasi kikubwa na kiuhalisia ni mahali ambapo watu mbalimbali tumekuwa tukikutana katika mitandao hiii hata pasipo kufahamiana.

Mitandao ya kijamii ni jamvi ambalo halina mmiliki isipokuwa ni sisi wenyewe kama jamii tuliofanikisha kutengeneza mitandao hii. Kukua kwa sayansi na technologia hususan katika mambo ya tehama kumechangia kwa kiasi kikubwa sana kutuunganisha na kutuweka pamoja kuweza kupata taarifa, burudani na kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo jamii yetu, afya zetu biashara, siasa n.k.

Kama jamii ya watanzania Sasa ni wakati muafaka wa kujua umuhimu wa kulitunza jamvi hili, kulitumia na kulilinda kwa ajili ya kutunza amani ya nchi yetu, kutunza mila,desturi na utamaduni wetu na kuinua uchumi wa Taifa na hata uchumi wa mtu mmoja mmoja. La hasha mitandao hii ina umuhimu mkubwa sana naweza kusema kuwa mitandao hii ni jamvi la thamani Sana Kwa Sasa na limetengenezwa katika thamani ambayo tukiiharibu itatugharimu Sana kuweza kupata zama kama hizi ambayo Dunia imepiga hatua sana na kurahisisha maisha ya mwanadamu kwa kiasi kikubwa sana, mfano Kwa Sasa unaweza kununu ama kupata hudumua kupitia tu mitandao, ambapo ilitupasa kutumia muda mrefu sana kuweza kusafiri na kuacha shughuli nyingine za kimaendeleo.

Naamini umepata picha halisi Nini maana ya jamvi na ni namna gani mitandao ya kijamii inaweza kufanana na jamvi.
Kwa miaka ya hivi karibuni Toka kuibuka kwa mitandao ya kijamii, mawasiliano ya simu janja hata komputa kumekuwa na mabadiliko sana makubwa kwa mwanadamu na utendaji hata namna ya kuweza kuwasiliana. kumekuwa na wimbi kubwa sana la kuibuka kwa lugha ama misemo mipya, namna ya uendeshwaji wa serikari yetu, familia zetu hata namna ya ufanyaji wa kazi na biashara.

Lakini kitu ambacho kikubwa sana tunapaswa kuangalia faida ya mitandao hii pamoja na Nini ni hasara ya mitandao hii.

Mitandao hama jamvi hili lenyewe lipo tu pale kuwasubiri wahusika kuketi na kujadili ama kufanya shughuri zao, Lakini kitu kikubwa zaidi kinachoathiri thamani ama lulu ya jamvi hili ni maudhui juu ya maada ama vitu tunavyotuma katika mitandao hii.

kiukweli tusipoweza kudhibiti suala hili linaweza kutufikisha mahali pabaya sana.
tumeona hata namna viongozi na makampuni yakiteua watu maarufu kutoka mitandao hii ya kijamii pasipo kuangalia weredi ama wasifu wa watu hao katika maisha halisi, hivyo kupelekea kuleta Hali ya sintofahamu katika maisha ya watu.

Pia mitandao hii imeongeza watu kufanya vitu vya kipuuzi kabisa ilimradi kufurahisha hadhira ya watu waliomo katika jamvi letu, watu wenye wafuasi wengi katika mitandao hii wamekuwa wakituma picha za utupu na za aibu kabisa lakini Cha kushangaza watu na hata viongozi ama taasisi zetu hazikukemea wala kuchukulia hatua masuala hayo.

Kurasa ama watu wa mitandao hii ya kijamii ambazo ziliweza kutoa elimu na weredi katika maudhui yake hazipewi kipaumbele kabisa kwa kuthaminiwa, hivyo inajenga picha ya kutisha kabisa ni namna gani maudhui yanayofanyika katika jamvi hili yanachangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu.

kumeibuka na wimbi kubwa sana la utapeli, ulaghai biashara za ngono na uharifu katika mitandao hii. kilio changu zaidi ni kizazi tunachokitengeneza katika mitandao hii, kitatisha maana tutaacha Dunia yeye kiasi kikubwa cha maovu na mmomonyoko wa maadili.

Swali la kujiuliza je mababu zetu ambao wametunza Imani, vitabu na masahafu ya dini na kutufanya tusome na kuishi katika misingi ya Imani maadili na kupendana wangetuachia maudhui kama ya Leo katika zama zao, je sisi tungekuwa ni jamii ya namna gani?

Bila kuchelewa napenda kutoa Rai kwa serikali yetu, jamii husika ama taasisi kuweza kuliangalia kabisa suala hili na kama Kuna Sheria basi sheria hiyo ipewe mkazo wa kiasi kikubwa sana ili kuweza kutunza na kulilinda jamvi letu ikibidi hata vitukuu vyetu viweze kurithi mambo mema yatayompendeza mwenyezi Mungu.

Wito "Mitandao ya kijamii ni jamvi linalotuunganisha, maudhui ya kikao juu ya jamvi yasitusambaratishe!".
 
Upvote 0
Back
Top Bottom