SoC04 Mitandao ya Kijamii Tanzania imulikwe, itumike kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii, irasimishwe

SoC04 Mitandao ya Kijamii Tanzania imulikwe, itumike kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii, irasimishwe

Tanzania Tuitakayo competition threads

Xpertz

Member
Joined
May 3, 2024
Posts
13
Reaction score
10
UTANGULIZI
Tanzania mitandao ya kijamii bado inatumika kama sehemu ya watu kutoa mawazo(stress), kupata habari nyepesi na udaku. Bado mitandao haijawa mahali salama sana kwa kizazi cha sasa na cha baadae kama hatutatengeneza mazingira salama kwa ajili ya wakati ujao. Bado haiaminiki, ina kundi kubwa la mamluki wanaotumia jukwaa hilo kutekeleza uhalifu wao wa kimtandao.

Bado mitandao ya kijamii nchini Tanzania inaongoza kwa habari nyingi za uongo, upotoshaji na uzushi ni vyombo vichache au watu wachache mfano JamiiForums.com wanaoaminika kwa kutoa habari za uhakika na kuaminika kwenye jamii ila asilimia kubwa ya watumiaji wa mitandao hiyo hawaitumii kutoa habari au maudhui yenye tija kwenye jamii.

Mitandao ya kijamii bado imeendelea kutumika kama majukwaa ya watu kuchafuana, kutukanana, kueneza habari za uongo na hata kupotosha habari mbalimbali kwa makusudi kabisa kwakua wanajua serikali itafatilia yupi iache yupi, Kiufupi kwenye mitandao ya kijamii nchini Tanzania kinachoendelea ni vurugu tupu.

Serikali imetangaza kwamba sasa imeanza kupata kodi kutoka kwenye makampuni ya mitandao hiyo ya kijamii je hilo tu linatosha? Jibu ni HAPANA

Mitandao ya kijamii ikitumika vizuri inaweza kusaidia kujenga jamii bora iliyostaarabika, kuzuia uhalifu, uzushi na uvunjifu wa maadili kwenye jamii.

Je nini kifanyike kuyafikia hayo?
1. Nashauri account zote za mitandao ya kijamii nchini zisajiliwe ziwe rasmi kupitia makampuni husika, ziwe rasmi zisiwe virusi(scam/spam) ili kujenga jamii yenye uwajibikaji. Hii itasaidia kuzuia wahalifu wanaofungua account bandia(feki) na kufanya matukio mengi ya kihalifu ikiwemo utapeli. Wengine wamekua wakitumia majina ya viongozi nk. Iwapo akaunti/kurasa binafsi za watumiaji zitahakikiwa na mitandao husika kwa usajili rasmi itasaidia watumiaji kuwa na dhamana ya akaunti zao na maudhui yao kuepuka kufanya uhalifu na kuchukuliwa hatua ikiwemo kufungiwa. Akaunti au kurasa binafsi zikiendelea kuwa sio rasmi /sio zilizothibitishwa tutaendelea kuwa na jamii inayolishwa kila aina ya upotoshaji, maudhui mabaya na uhalifu uliokithiri. Mitandao ya kijamii nchini itaendelea kuwa eneo hatarishi kwa vizazi vyetu na kupoteza fursa ya kuwa jukwaa rahisi na nafuu kuikomboa jamii kifikra na kimaudhui kupitia kuwakutanisha pamoja kwa gharama nafuu.

2. Taasisi zote za kiserikali ziwe na kurasa(account) rasmi za mitandao ya kijamii zinazofanya kazi ili kurahisisha ufikaji wa taarifa kwa jamii kwa haraka na kwa wakati. Kwa sasa bado taasisi nyingi za Serikali kwenye mitandao ya kijamii hazipo hivyo kuwapa mwanya wapotoshaji wengi kujitwalia utukufu kwenye jukwaa hilo kwa haraka inapotokea upotoshaji wa taarifa kuhusu taasisi husika na kuzua taharuki. Taasisi nyingine zina kurasa za mitandao ya kijamii ila hazitumiki. Nyingine hazina kabisa kurasa hizo. Hii inaonesha ni kwa kiasi gani Serikali yenyewe ipo nyuma kwenye kutumia fursa ya mitandao hiyo ya kijamii kuhudumia wananchi kwa unafuu. Mfano matangazo kwa umma nk mitandao hiyo ingefaa sana kutumika kufikisha taarifa kwa haraka hususani nyakati za dharura. Nipongeze baadhi ya taasisi ambazo zinajitahidi kutumia mitandao hiyo kwa ufanisi mkubwa mfano Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Tanzania, Mamlaka ya hifadhi za taifa TANAPA, mamlaka ya mapato Tanzania TRA, Shirika la umeme Tanzania TANESCO, shirika la reli Tanzania TRC nk

3. TCRA isiishie kukamata tu wahalifu wa kimtandao bali itoe mafunzo mengi kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwenye jamii. Mamlaka hiyo ya kudhibiti mawasiliano nchini bado haitoi elimu ya kutosha kwa mapana yake kwenye jamii kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii hasa ikizingatiwa mitandao hiyo imeingia kwenye matumizi kwenye jamii bila jamii kuandaliwa. Elimu sahihi itasaidia kupunguza matukio mengi ya kihalifu yatokanayo na matumizi yasiyo sahihi ya mitandao hiyo ya kijamii. Kwa kiasi kikubwa kwa sasa jamii inawatambua TCRA kama askari wakamataji badala ya wasimamizi, yaani kwa maana nzima ya elimu na udhibiti.

4. Gharama za data zishushwe kuwezesha asilimia kubwa ya wananchi kwenye jamii kutumia mitandao hiyo ya kijamii kupata habari. Hii itasaidia jamii kuwa na uelewa wa mambo mengi kwa kasi kuendana na ulimwengu wa utandawazi. Majukwaa hayo yamekua muhimu watu kuhabarika na kuelimika pamoja na kutoa maoni yao pia kujiajiri kidigitali ila bado gharama sio rafiki kwa Tanzania, ni kubwa. Gharama za data zikiwa chini zitasaidia wananchi wengi kutumia mitandao. Kadri miaka inavyosogea nchini Tanzania gharama za data zinazidi kupanda badala ya kushuka hii inaua motisha ya ukuaji wa matumizi ya jukwaa la mitandao ya kijamii na kuua uhuru na haki ya watu wengi zaidi katika jamii kupata habari, kuelimika na kutoa maoni yao. Sambamba na hilo akaunti au kurasa binafsi zisitozwe gharama za leseni isipokua kwa vyombo rasmi vya habari vinavyofanya biashara pia.

5. Nyakati za matukio muhimu ya kitaifa mitandao ya kijamii isizimwe. Hili limekua likijitokeza kwenye Mataifa mengi ya Afrika hususani nyakati za uchaguzi mkuu ili kuzuia ueneaji wa taarifa za matokeo. Nashauri Tanzania baada ya mitandao kurasimishwa uhuru wa habari ubaki kuwa kipaumbele ila jamii itahadharishwe kwamba mtu akiandika upotoshaji atawajibika nao. Kuzima mitandao haisaidii bali huzidi kuongeza taharuki wakati wa matukio hayo na kuleta tafsiri za matukio ya kihalifu mfano wizi wa kura jambo ambalo huenda sio kweli.

Nawasilisha.
 
Upvote 1
Insha yako ina mawazo mazuri ya kusaidia kupunguza tatizo.

Lakini mitandao ya kijamii, ndiyo hivyohivyo ilivyo - ya kijamii. Ni lazima itaakisi akili ya jumla ya jamii inayoiunda tu.

Jamii forum itaakisi hapa kama ambavyo reddit na quora itaakisi jamii yake. Nasikia hata ukitazama tiktok ya bongo na ya china ni tofauti. Na sio algorithm au nini lakini ni kile hasa watumiaji wamejikita kusambaza.

Kwa kisema hivyo basi, pamoja na mbinu za kisheria na taratibu. Tuwekeze pia kwenye malezi ya jamio na falsafa bora kwa taifa kiujumla wake.
 
Back
Top Bottom