Uchaguzi 2020 Mitandao ya kijamii Tanzania yawa restricted. YouTube, WhatsApp, Twitter, JamiiForums na Telegram zimeguswa - Oktoba 27, 2020

Kwani yule mwendawazimu bado anazuia hii mitandao!?
 

Salary Slip
 
Kwani yule mwendawazimu bado anazuia hii mitandao!?
Mimi ninashangaa yaani inazungusha tuu sipati kitu ingawa Nina Bando la kutosha. Nilidownload Twitter play Store nikawa naitumia. Kipindi cha Uchaguzi ikapotea. Baadaye ilirudi. Juzi Kati nikawa napata Post za Kizamani then imegoma haileti kitu. Anyway nitaweka hiyo VPN. Asanteni
 
Ni jambo la ajabu na ilianza kama utani kipindi cha uchaguzi, cha ajabu ile mitandao mingine imefunguliwa ila bado kuipata Twitter kwa bado la kawaida bila kutumia VPN imekuwa ni shida hadi leo ikiwa ni zaidi ya miezi mitatu baadaa ya uchaguzi.

Wengine hutumia Twitter kupata taarifa muhimu na inawezekana hatuko interested na Kigogo hata kidogo, we are just doing our business, sasa kwanini mtufanyie hujma?

Vifurushi vyenyewe vimepandaa bei, bado mnatuongezea route za Internet kwanini? Kweli unaweza athiri mamia ya watu kwa ajili ya mtu mmoja tu?

Sio fair, mtufungulie Twitter, mana wapenzi wa Kigogo kama ni kutafuta habari zake watazipata tu zaidi mnatutesa wote.

Busara itumike, hata kama alietoa order anaogopwa inabidi ajuzwe kuwa kuminya access ya internet hakumfanyi kuwa mwema zaidi na kupendwa.
 
Ni sawa na kutaka kuifungia JF kwasababu ya jukwaa moja tu nawakati 90% ya members sio wadau wa jukwaa hilo Jukwaa moja liathiri watu wa jukwaa kama 10
 
Kipindi fulani Jeshi la Polisi ndio liliandama badala ya wananchi yale maandamano ya Mange. Bongo ya Maramboso.
 
Imagine jitu lipo ikulu badala ya kuhangaika na mambo ya msingi ya nchi hii kama vile uchumi,siasa safi,ajira kwa vijana,e.t.c linahangaika na kimtu kama Kigogo!
 
Nikitumia VPN simu yangu inakula sana chaji, nimeamua tu nikae kimyaa niachane na mambo ya Twitter hadi pale watakapoamua wenyewe kutufungulia.
 
Ni sawa na kutaka kuifungia JF kwasababu ya jukwaa moja tu nawakati 90% ya members sio wadau wa jukwaa hilo Jukwaa moja liathiri watu wa jukwaa kama 10
Kwani mkuu umesahau vibano vya Clouds TV na Wasafi TV?
 
Nikitumia VPN simu yangu inakula sana chaji, nimeamua tu nikae kimyaa niachane na mambo ya Twitter hadi pale watakapoamua wenyewe kutufungulia.

Mkuu hili swala linanikera sana kwa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…