Yaani hii nchi imejaa matapeli watupu wa kimtandao halafu tunaishia kuua wadogo zetu wezi wa kuku tu ili ale!
Fikiria bahata nasibu ya ushindi wa kila baada ya dakika mbili wa Milioni Saba, kwa maana ya kwamba kila baada ya saa Moja Jamaa wanatoa Washindi 30 wa Milioni 7 yenye maana ya kwamba Washindi 180 wa Shilingi Milioni Saba Saba kila Baada ya Masaa Ishirini na Nne!
Baada ya Siku Tatu ama Nne ndio unasikia Baba Desi ameshinda shs Milioni Tatu!! Hii Milioni Tatu imekujaje wakati Ushindi wa Kwanza ni Milioni Saba na hailezwi kwamba kuna mshindi wa kwanza na wa Pili?
Ngoja tu niendelee kibahatisha siku moja moja na Sport Pesa! Angalau wao ninaona kinachoendelea!!!